Kiwanda cha viuatilifu Kibaha kimefungwa mwaka sasa, Waziri wa Afya majibu alitoa wapi?

Retina

JF-Expert Member
Mar 6, 2015
1,038
1,154
Nasikitika mno kiwanda cha viwatilifu vya kuulia mbu hakifanyi kazi, licha ya kufunguliwa na kutolewa maelezo kwa mbwembwe na wanasiasa wa VYEO vya juu nchini.

Juzi Kati katika bunge hili la bajeti 2021/2021, kwenye kipindi cha maswali na majibu, Waziri wa afya aliulizwa swali na mbunge asiye na Chama kuhusu viwatifu vya kuulia mbu na mwendelezo wa kiwanda. Katika majibu ya wizara alijibu kama hakuwa na ufahamu kama Kuna viwatilifu vinazalishwa na kiwanda na umuhimu wake.

Nimepita maeneo ya kibaha, kiwanda kimefungwa muda mrefu, hakuna mlinzi huku nyasi zimeota ndani na nje ya kiwanda.Taa haziwashwi jioni ni giza totoro.

Jibu alilotoa Waziri wa afya, halikuakisi hali ilivyo kwenye uzalishaji, umuhimu na uhalisia wa uwepo wa viwatilifu hivyo nchini. Majibu ya wazir wa afya aliyatoa wapi. Kuna haja ya kufuta kipindi cha maswali na majibu bungeni, majibu ya mawazir hayana uhalisia.
 
Hapo wizara haina majibu kwa sababu ni sehemu ya ufisadi wa kuharibu kiwanda kwa kupewa pesa na USAID. Tuna watu wa bei ndogo sana wiazara ya afya. Ndo maana siwaamini kama kweli kinachokuja ni chanjo au dawa ya kutia watu uhanisi.

Hicho kiwanda kilijengwa na Cuba kwa niya njema. Miaka ya 2018 nilifika hapo nikakuta tatizo hilo. Nchi za west Afrika zilikuwa zinaangiza kinga hiyo ya mbu toka Kibaha, lakini wizara yetu ya afya ilikuwa haitaki kabisa! Sababu kubwa kulikuwa na US wakigawa vyandarua na hawakupenda kuingiliwa na Cuba ktk kupambana na tatizo la malaria. Hapo ndo maafisa wa wizara walikuwa wakidakishwa pesa na wao kukiangusha kiwanda.
 
..kiwanda kimefungwa wakati wa shujaa au baada ya mama kushika usukani?
Ninavyofahamu, kilianza kuanguka pole pole tangu enzi za Kikwete. Sababu ikiwa ni NDC ambao ndo wamiliki kwa msaada wa Cuba, kukosa nguvu ya kuilazimisha wizara ya afya kuona umuhimu wa product zao. NDC tatizo haikuwa na CEO mwenye msukumo. Kwa ujumla Wizara ya afya imejaa madili!

Kuna taasisi za serikali zimesahaulika kabisa!
 
Daah! Hicho kiwanda kilijengwa na kampuni ya Labiofam ya Cuba kwa pesa mingi. Kama kimeshindwa kuwa sustainable, Labiofam waitwe wakigeuze kitumike kuzalisha pestcide na herbicides.
 
Hapa nime google. Kumbe hiki kiwanda kina uwezo wa kuzalisha hadi chanjo za Covidiii 😀😀😀

Screenshot_20210625-153135.jpg
 
Ninavyofahamu, kilianza kuanguka pole pole tangu enzi za Kikwete. Sababu ikiwa ni NDC ambao ndo wamiliki kwa msaada wa Cuba, kukosa nguvu ya kuilazimisha wizara ya afya kuona umuhimu wa product zao. NDC tatizo haikuwa na CEO mwenye msukumo. Kwa ujumla Wizara ya afya imejaa madili!

Kuna taasisi za serikali zimesahaulika kabisa!
Kwa hiyo hata shujaa hiki kiwanda kilimshinda kuendesha?

Hakuna kiongozi wa ethiopia aliyetembelea hicho kiwanda? Ilikuwa awamu gani?
 
Tatizo siyo wewe kununua, shida ni wizara kuikubaki na kuitumia ktk kampeni zake. Maana wewe ukitumia na jirani hatumii, itakuwa ni useless.
Mbona wizara ilishaelekeza hakmashauri zinunue na linafanyika?
mleta mada ni kiwanda cha uongo
 
Hapo wizara haina majibu kwa sababu ni sehemu ya ufisadi wa kuharibu kiwanda kwa kupewa pesa na USAID. Tuna watu wa bei ndogo sana wiazara ya afya. Ndo maana siwaamini kama kweli kinachokuja ni chanjo au dawa ya kutia watu uhanisi.
Duh! Mbaya sana. Misaada haifai hasa ya mabeberu
 
cc @Kilatha

Back
Top Bottom