Kiwanda cha kutengeneza magari nchini Kenya,chatengeneza gari la MOBIUS,

hao ni vilaza pia.. sasa kuna faida gani ya kuanzisha kiwanda africa na ukauza gari lako kwa mil 28.. wangetengeneza gari la milioni moja na nusu hapo tungewaelewa
 
Kiwanda Cha Kuunda Magari Cha Mobius Motors Cha Jijini Nairobi, Nchini Kenya Kimeliingiza Sokoni Gari Lake Jipya Aina Ya Mobius II Ambalo Limetengenezwa Kwa Kuzingatia Ubovu Wa Barabara Za Afrika Na Linauzwa Tsh. 28 Milioni.

Hongera Kenya Kwa Hatua Hii Mliofikia, Haya Ndio Maendeleo Ya Kweli.

Wito Kwa mwijage, anzisheni viwanda vya namna hii
Mwijaghe gani uliemtaja hapa??
Yule aliesema Cherehani 4 nazo ni Kiwanda??
 
That's the smartest move hasa ukizingatia landrover 110 inasitisha uzalizashaji na hii gari ukiiangalia kabisa ni replacement ya 110 and retailing at cheaper price na bado imebuniwa kwa ajili ya soko la Africa, nawashauri waje na gari za African safariS tuachane na cruiser.
Bila shaka kwa Mwana EA hiyo gari atainunua bila kodi nyingi ukizingatia makubaliano ya EA.
 
Mwijaghe gani uliemtaja hapa??
Yule aliesema Cherehani 4 nazo ni Kiwanda??
Kiwanda cha toothstick ti shida.....
Wabunifu wakitokea wamegundua vitu kwa juhudi binafsi wanaletewa siasa ...

Ova
 
Mods mnazingua kuna uzi unahusiana na huu kuna jamaa alitoa leo alfajir naona wameufuta wacha nondo nitahamishia humu. ni kweli WAKENYA WAKO JUU.
 
Kiwanda cha toothstick ti shida.....
Wabunifu wakitokea wamegundua vitu kwa juhudi binafsi wanaletewa siasa ...

Ova
Ha ha haa,
Ndio unamwambia eti alete Kiwanda cha Magari, huo ni Mzigo Mkubwa sana kwake
 
Sijui shida iko wapi hapa kwetu, sisi tuna utulivu wa kisiasa kuliko wao, tumeongozwa na chama kimoja muda wote, wao kila siku vyama tofauti lakini wanazidi kupaa. Sasa hivi mambo mengi ya msingi wako juu yetu. Kwenye uchumi wako mbali, kielimu pia, kidemokrasia ndio usiseme, hata kimichezo wanatufunika sana.
Soma historia. Baada ya uhuru sisi tuliamua kujenga uchumi shirikishi wa kijamaa, uchumi unaofaidisha wananchi wote kwa usawa. Wazungu wote tuliwatimua katika umiliki wa uchumi wetu ulioongozwa kwa misingi ya Azimio la Arusha.

Kenya baada ya uhuru waliendelea na mfumo wa kikoloni kuendesha uchumi wa nchi yao. Wazungu waliendelea kuishi na kumiliki uchumi wa nchi kama ilivyokuwa awali. Uchumi wa kibepari unaomilikiwa na watu wachache. Uchumi usio shirikishi hadi leo.

Wala hili hatujakosea. Uchumi wetu uko vizuri sana kuliko wa Kenya kwani ni uchumi shirikishi. World Economic Forum ime rank Tanzania nafasi ya kwanza Afrika kwa kuwa the best inclusive economy.
 
Unaongea nini dogo? Kwa hiyo viwanda vya Azam vinamilikiwa kwa ushirika wa Bakhresa na Humphrey Polepole? Uchumi unasema sisi tuko vizuri kuliko Kenya, endelea kulala hapohapo.
 
Inaonekana bado mdogo sana mtoa maada, Tanzania ilshawahi kuunda magari wakati wewe hujazaliwa wala Kenya haijafikiria, tembelea shirika la Nyumbu pale Kibaha ujionee. Ingawaje kwa sasa wamesimaa kuunda magari kwa sababu zilizo nje ya kampuni.
Mkuu hicho ndicho kitu cha kujisifia!! wenzetu wakianza wanaendeleza,wewe unajisifia unjinga,hii inaonyesha vipi Tanzania inashindwa kusimama mambo yake...,

"Chenga twawala lakini kutufunga wametunnga":D:D
 
Unaongea nini dogo? Kwa hiyo viwanda vya Azam vinamilikiwa kwa ushirika wa Bakhresa na Humphrey Polepole? Uchumi unasema sisi tuko vizuri kuliko Kenya, endelea kulala hapohapo.
Wewe ndiye dogo, hujui tulikotoka. Muulize babu yako atakueleza. Muulize hata Babu Bakhresa atakusimulia.
 
Back
Top Bottom