Kivuko kipya cha Kigamboni kubeba abiria 2,000, gari 60 | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kivuko kipya cha Kigamboni kubeba abiria 2,000, gari 60

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by JuaKali, Nov 15, 2008.

 1. JuaKali

  JuaKali JF-Expert Member

  #1
  Nov 15, 2008
  Joined: Nov 14, 2007
  Messages: 785
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Kivuko kipya cha Mv Kigamboni II kinatarajiwa kuingizwa majini leo tayari kwa majaribio ambayo mwishowe yatakiwezesha kuvusha abiria 2,000 na magari 60 kwa safari moja.

  Zoezi hilo linatarajiwa kufanyika sasa baada ya kukamilika kwa kazi ya kukiunganisha iliyofanyika kwa zaidi ya miezi kumi sasa.

  Kivuko hicho kimeigharimu Serikali zaidi ya Sh. Bilioni 9 na kazi hiyo ilikuwa ikifanywa na Kampuni ya NRSW ya Ujerumani, baada ya kufanikiwa kushinda mchakato wa zabuni uliokuwa chini ya Ofisi ya Katibu Mkuu wa Wizara ya Miundombinu.

  Akizungumza na waandishi wa Habari Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni hiyo, Bw. Shaffiq Dhalla, amesema tayari kivuko hicho kimekamilika katika hatua zote muhimu za ujenzi na kwamba hivi sasa, kinatarajiwa kusogezwa jirani na maji tayari kwa majaribio yanayotarajiwa kufanyika siku ya Jumanne ya wiki ijayo.

  Dhalla akasema kuwa kivuko hicho kipya kitakuwa na uwezo wa kubeba tani 500 ikiwa ni pamoja na kusafirisha zaidi ya abiria 2000 na magari 60 kwa wakati mmoja.

  ``Tunamshukuru Mungu kazi hii ambayo kwa hakika wakati wote ilikuwa ikitunyima usingizi, imemalizika kwa ufanisi mkubwa, tunasubiri kuanza majaribio na kuikabidhi serikali tayari kwa kazi ya kuhudumia jamii ya wananchi wa Kigamboni na Jiji la Dar es Salaam kwa ujumla,`` akasema Bw. Dhalla.

  Akizungumzia kukamilika kwa kivuko hicho cha kisasa ambacho, Mkurugenzi wa Ufundi na Umeme katika wizara ya Miundombinu Mhandishi John Nduguru, akasema kuwa kazi hiyo imekamilika kwa wakati kulingana na makubaliano baina ya wizara na kampuni ya NRSW.

  ``Ni kweli kazi ya uunganishaji wa kivuko hiki imekamilika, tayari tumekwenda kwa ajili ya ukaguzi na kujiridhisha kuwa kazi hiyo ya ujenzi wa kivuko kipya na cha kisasa imekamilika,`` akasema Mhandisi Ndunguru.

  Kwa muda mrefu sasa, abiria na wananchi wa kigamboni wamekuwa na matatizo ya usafiri wa uhakika kutokana na kuharibika mara kadhaa kwa vivuko vilivyopo sasa.
   
Loading...