Kivuko cha magogoni-kigamboni nauli juu

Mughwira

Senior Member
Jun 10, 2008
109
34
Uongozi wa Kivuko cha Magogoni/Kigamboni umepandisha nauli kwa 100% kuanzia mwaka mpya 2012, wakati wakazi wa Misungwi wanavuka bure Watanzania wengine wanavuka kwenda Kigamboni au kuja mjini kwa shughuli za kujenga Taifa wanapandishiwa nauli kwa 100%. Kwa hali hii wananchi watakuwa na hali ngumu ya maisha mara 500 zaidi ukizingatia Tanesco noa wanapandisha umeme kuanzia tarehe I January 2012. Mapinduzi yananukia Tanzania.
 
Hali ya maisha ilivyongumu inasikitisha nauli ya watu wa kigamboni kupandishwa..haya ndio madhara ya kuchagua watu wabinafsi wanaojali masilahi yao tu.Serikali chini ya chama tawala imeshindwa kusaidia wananchi wake katika kujiondoa na hali ngumu ya maisha nafikiri ni muda wa Watanzania sasa kugomea baadhi ya mambo yanavyoendeshwa katika nchi hii.
 
Back
Top Bottom