Kiuno kinanitesa, napata maumivu makali

Yes iam

JF-Expert Member
Oct 4, 2018
258
370
Habari zenu watabibu,

Nina miaka 27 sasa, mimi ni dereva wa gari. Nahisi ndiyo tatizo langu lilipoanzia, seat ya hili gari inagonga sana ukijumlisha na njia ninayoendeshea. Twende kwenye maada sasa.

Yapata mwezi sasa kiuno kinauma sana nikiwa nimekaa kwa mda mrefu nikiinuka tu kiuno kinakaza sana kinauma hadi nashindwa kusimama inabidi nikae tena.

Nilienda Pharamcy kuna vidonge walinipa nimeze lakini havijasaidia. Je, nifanyaje? Nitumie dawa gani niondokane na hili tatizo nina siku ya 5 sasa sijafanya kazi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Pole sana ndg kwa sababu unachekesha kweli kweli. Ati unaumwa halafu badala ya kwenda hosp unaenda pharmacy. Ulipofika ukamwambia; Nipe vidonge vya rangi mbili. Ukapewa ukameza kwa ajili ya kiuno kinauma!!!! Maajabu gani haya?? Leo karne hii hakuna tena watu wa jinsi yako ndg. Nenda hospitali, eleza hoja zako, upatiwe vipimo na matibabu sahihi.

Huenda una pingili ya uti wa mgongo imekaa vibaya. Matokeo yake ni kusagika na kuleta madhara zaidi.
Huenda kiti cha gari lako ni kama cha tractor na au hakinesi hivyo ule ugumu unapoingia kwenye shimo unagonga kwa nguvu kiti na kujiletea maumivu.

Ushauri: Nenda haraka hospital ukapate vipimo sahihi kwa matibabu sahihi. Acha kujinunulia vidonge
 
Yes iam,

Achana na kutumia dawa bila vipimo na maelekezo ya wataalamu. Nenda hospitali ukapatiwe vipomo, then utapwewa ushauri ni nini cha kufanya
 
Unaendesha gari la aina gani??
Unaendesha kwenye barabara gani?
Unaendesha umbali wa kilometers ngapi kabla hauja pumzika?

Sent using Jamii Forums mobile app
fuso tipper ya mchanga naamka saa 10 alfajil naandesha kutwa nzima had nimalize trip zangu 4 saa 1 usiku, napumzika kama dk20 tu pale nikiwa nakula.

Mwendo ni km 100 kwend na kurud Mbez-Kibaha barabara rami kidgo na rafu road kwa sana.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Pole sana ndg kwa sababu unachekesha kweli kweli. Ati unaumwa halafu badala ya kwenda hosp unaenda pharmacy. Ulipofika ukamwambia; Nipe vidonge vya rangi mbili. Ukapewa ukameza kwa ajili ya kiuno kinauma!!!! Maajabu gani haya?? Leo karne hii hakuna tena watu wa jinsi yako ndg. Nenda hospitali, eleza hoja zako, upatiwe vipimo na matibabu sahihi...
ahsante sana kiongozi kwa ushauri ntaenda hosptalI

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwa huo umri mkuu umetuangusha sana... kwenda pharmacy badala ya hospital..!! Duh
 
Habari zenu watabibu,

Nina miaka 27 sasa, mimi ni dereva wa gari. Nahisi ndiyo tatizo langu lilipoanzia, seat ya hili gari inagonga sana ukijumlisha na njia ninayoendeshea. Twende kwenye maada sasa..
Pole Sana Kwa Changamoto yako ya viungo na Mifupa.


Ushauri Wangu.
Naomba Ufanye Uchunguzi wa Kitaalam ili kubaini Tatizo, hii itakuwa njia rahisi ili Kupata matibabu sahihi,

BF SUMA tunavyo virutubisho lishe kwaajili ya matibabu kwa Changamoto yako.

1•ArthroXtra; Hii itakusaidia kuhuisha Cartridge/Disk (Kiswahili Gegedu) zilizokwisha na kusaidia kurudia hali yake ya kawaida.

2•Gluzojoint; Hii itakusaidia Kurudisha Uteute ( Synovial Fluid) Uliokwisha Kwenye Maungio na kusababisha Gegedu kuisha na mifupa kusuguana.

3•Zaminocal; Hii ni Maalum Kusaidia mifupa ambayo imelika au kusagika, Sababu imetengenezwa Kwa Formula ya Zink,Amino na Calcium.

4•Micro²Cycle; Hii itakusaidia kusafisha mfumo wa Mzunguko wa Damu, kuondoa maumivu na Kufanya damu iendelee na mzunguko wako wa Kawaida Hivyo ni Msaada mkubwa kwa wenye Changamoto ya miguu kuwaka moto, ganzi na maumivu ya misuli na viungo.

Kwa Ushauri Zaidi tupigie kupitia 0765114316.
 
Back
Top Bottom