Kiungo wangu bora wa ' Ukabaji ' nchini Tanzania kwa sasa Jonas Gerald Mkude a.k.a Deco De Souza amuumbua ' Mpuuzi ' Amunike

Fact, case closed
 
Ila kiukweli kumlinganisha fei toto na mkude ni kumkosea sana heshima mkude. Fei toto alinganishwe na Ndemla na kwa jicho la kimchezo Ndemla yuko juu.
 
Hivi kikosi hiki TFF wamekitelekeza maana hiki ndiyo kingetupeleka world cup 2026
 
Mkude yuko vzr kwa viwango vya middle wetu hapa home... hao tunaowataja pia wako vzr ila tuwape muda.
Kuaminiwa kwenye vilabu vi3 vya Azam, Simba na Yanga then Taifa sio kazi ndogo.
 
Gentamycene katika ubora wako
 
Mkude ovyo tu..Mdathir akirudi hana namba Stars..alafu mechi ya CHAN na Kenya na hii ya Burundi sio kipimo..Akutane na waarabu na miwest Africa ya Ulaya ndiio uje hapa kuongea
 
Mkude ni mzuri timu inapokuwa na mpira kwani anaweza sana kuchezesha timu kutokea nyuma kwa pasi fupi fupi. Na uzuri wake ni kwenye pasi fupi fupi tu (square pass).

Udhaifu wa Mkude upo kwenye kwenye kupora mipira kwa adui na hii ndio kazi hasa ya kiungo mkabaji. Uwezo wake wa kupora mipira kwa adui au hata wakati mwingine kuharibu mipango ya adui hapa uwezo wake ni mdogo sana. Pungufu lingine kubwa ni jicho la kupiga pasi za mbali kwa washambuliaji pale timu inapokuwa imezuia shambulizi la adui na kwa haraka inataka kufanya counter attack. Mapungufu yote haya yalikuwa yanafichwa na Kotei na ndio maana sasa toka ligi imeaanza na CL kumekuwa na mijadala mingi magazetini na mitandaoni kuhusu uwezo wa Mkude kuliko kipindi kingine chochote kwa sababu sasa yule Mkude halisi ndio anaonekana alivyo tofauti na yule aliyekuwa anafichiwa baadhi ya mapungufu na Kotei.

Kibongo bongo bado Mkude anaonekana anaweza kwa sababu ya aina ya timu anazopambana nazo hazina wachezaji wa kumpa changamoto. Ila kwenye mechi zote mbili za CL ligi dhidi ya UD Songo Mkude alionekana kabisa mechi zilikuwa kubwa kuliko uwezo wake. Kwa mwenye uwezo wa kupata CD ya zile mechi zote mbili akaangalie taratibu aone jinsi gani wale jamaa walivyokosa umakini na bahati kwani wangeweza kutufunga goli nyingi kwani walimgezuza Mkude ndio njia ya kupita kuelekea golini kwa Simba kadri walivyotaka wao. Timu nyingi huwa zinapita pembeni lakini wao waliona shimo kati kwa Mkude wakawa wanapita hapo hapo.

Mpaka leo sijui ni kwanini Simba wanapotaka kushambulia au kuamua matokeo kwa kutumia counter attack hawamtumii Ndemla ambaye walau ukabaji wake ni wa nguvu kidogo na ana nguvu za miguu na jicho la kupiga pasi za mbali pale timu inaponyang'anya maadui mpira na kutaka kuanza kushambulia kwa ghafla kutokea kwenye zone yao. Any way hayo tuwaachie Kitambi na Ausems ndio wataalamu sisi wengine ni watoa maoni tu.

Jamani huu ni mtizamo tu maana naona hapa watu wana hasira sana kutokana na mpenzi yaliyopitiliza kwa Mkude pasipo kuona mapungufu yake na kumweleza ili aweze kujirekebisha uchezaji wake.
 
Kiungo gani hata pass hajui kazi yake kufau sema kwa sasa yule Dogo wa Azam hayupo tu ndio sababu anapata namba timu ya taifa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…