Kiungo wangu bora wa ' Ukabaji ' nchini Tanzania kwa sasa Jonas Gerald Mkude a.k.a Deco De Souza amuumbua ' Mpuuzi ' Amunike

An Eagle

An Eagle

JF-Expert Member
Joined
Feb 11, 2019
Messages
1,204
Points
2,000
An Eagle

An Eagle

JF-Expert Member
Joined Feb 11, 2019
1,204 2,000
Sijawahi Kupenda vibovu vibovu hata Siku moja na nilisema kuwa kwa sasa Tanzania bado sijaona Kiungo Mkabaji bora kama Mdogo wangu mwenyewe Jonas Gerald Mkude ila kuna Watu walinipuuza lakini kwa Kazi ya Mkude Uwanjani sasa amewajibu na wamenyamaza.

Ni Kocha ( Mwalimu ) Mpumbavu tu kama si Mpuuzi wa mfano wa yule Kocha ambaye alibahatisha Kutupeleka AFCON 2019 na kwa Msaada mkubwa wa Ujirani mwema wa Uganda na Tanzania lakini pia akatuwekea Rekodi ya pekee huko Misri kwa Tanzania kufanya vibaya mechi zote na kukosa hata Alama moja tu ndiyo hatoona Umuhimu wa Kiungo wangu Kipenzi na Fundi kabisa katika Dimba la Kati ( hasa upande wa Ukabaji ) kama Jonas Gerald Mkude.

Utasemaje Mkude hafai huku karibia Makocha wote wakubwa na mahiri ambao wamewahi Kuifundisha Simba SC na hata Timu ya Taifa walishasema kuwa kwa sasa Tanzania nzima hakuna Mchezaji wa Kiungo hasa cha Ukabaji na anayejua Majukumu yake vyema kama Jonas Gerald Mkude? Na ukiona Kocha anamchukia Mkude jua anamuonea Wivu tu au ana Chuki nae binafsi au ana ' Udalali ' na baadhi ya Wachezaji ili awauze Ulaya na apate 10% yake.

Namwomba aliyekuwa Kocha wa Taifa Stars Emanuel Amunike a.k.a Mpuuzi aje atuombe Radhi haraka Watanzania kwa Kitendo chake cha Kutudanganya juu ya Uwezo wa Kiungo Jonas Gerald Mkude huku akimtangaza vibaya kuwa ni Muhuni ( Mvuta Bangi ) wakati Mimi kama An Eagle nawajua zaidi ya Wachezaji wa Taifa Stars tena ' Waandamizi ' kabisa ambao ni Wavuta Bangi mahiri na wazuri kuliko hata huyu Mwanangu mwenyewe Mkude.

Kwa aina ya Mpira wa Kiwango cha juu ambao anaucheza sasa Mkude nina uhakika huyu Kocha ' Mpuuzi ' Emanuel Amunike huko aliko sasa anaona Aibu na anajisikia vibaya mno kwani ' Dogo ' Mkude anamdhihirishia kuwa alizaliwa kuja kuwa ' Kiungo Mkabaji ' na pia aliye na ' tuvituvitu ' vitamu vitamu Uwanjani huku akiichezesha Timu anavyotaka na akiwapa Likizo / Nafuu Mabeki ' Waandamizi ' wa Stars ambao pia ni Kaka zake Kiumri akina Yondani na Nyoni.

Ni Wachezaji Watatu tu kama si Wanne ambao tokea Timu hii Taifa iwe chini ya ' Mtaalam ' Kocha Ndayiragije ndiyo hawakubadilishwa au hata Kupumzishwa katika Mechi ambazo Timu imecheza na huyu ' Mwanangu ' mwenyewe Mkude nae akiwemo na hii inathibitisha kwamba Kocha na jopo lake wakiwemo akina Juma Mgunda na Kocha ambaye ndiyo alimuibua, amemtengeneza na kumpika Mkude hivi Suleiman Abdallah Matola a.k.a Veron a.k.a Mzambia hawana Mashaka nae na wanakikubali kile ambacho anakifanya hasa katika Dimba la Chini ( Kiungo cha Nyuma )

Na tokea Mkude arejeshwe Taifa Stars ndiyo nimekuwa na Mapenzi nayo sasa na huenda ndiyo maana inabarikiwa vile vile japo tusifichane wala kupeana Moyo kwa hatua hii ya Makundi ambayo tunaenda Kupangwa sasa ndiyo tukicheza tufanikiwe kwenda katika Fainali za Kombe la Dunia huko Qatar mwaka 2022 hapa ndiyo mwisho wetu kwani ili tufanikiwe tunahitaji Maandalizi makubwa na kabambe tena mengi ni ya Kiufundi zaidi kitu ambacho sidhani kama kwa sasa Tanzania tutakiweza ila tukianza Maandalizi sasa ya Kombe la Dunia la 2026 nina uhakika tunaweza Kushiriki.

Hongera sana ' Mwanangu ' mwenyewe Jonas Gerald Mkude kwani unalikamata Dimba la Kati kama vile ninavyotaka. Watakukoma!
 
monopoly inc

monopoly inc

JF-Expert Member
Joined
Dec 20, 2016
Messages
2,117
Points
2,000
monopoly inc

monopoly inc

JF-Expert Member
Joined Dec 20, 2016
2,117 2,000
Sijawahi Kupenda vibovu vibovu hata Siku moja na nilisema kuwa kwa sasa Tanzania bado sijaona Kiungo Mkabaji bora kama Mdogo wangu mwenyewe Jonas Gerald Mkude ila kuna Watu walinipuuza lakini kwa Kazi ya Mkude Uwanjani sasa amewajibu na wamenyamaza.
Mkude ni kiungo mzuri lakini kuna makosa mengi sana anayafanya kwenye jukumu la kukaba mpaka msimu uliopita alipewa msaada wa kotei,

Kitu pekee kinachombeba Mkude ni timu anayochezea ya Simba ina profile kubwa hivyo inamfanya aonekane kiurahisi

Mleta Mada ligi ishaanza naomba ukawachunguze hawa watu

1; Antony Majogoro
2;Freddy Tangaru
3;Alex massawe
4;Shabban Nditi
5;Awadh salum
6;Ally msengi
8;Jimmyshoji Mwaisondola
9; kuna dogo Yupo alliance uliempiga dole gadiel Michael nimemsahau jina
 
Mr Morogoro

Mr Morogoro

JF-Expert Member
Joined
Apr 23, 2019
Messages
926
Points
1,000
Mr Morogoro

Mr Morogoro

JF-Expert Member
Joined Apr 23, 2019
926 1,000
Mkude anamapungufu yake mara nyingi amekuwa off kwenye eneo lake angalia goli waliofunga Burundi yeye alikuwa wapi ,tuangalie mchezaji mmojammoja
Mkuu unaujua mpira??kwa hiyo goli lililofungwa jana lawama tumpe mkude 😂 😂 😂 😂 ...nimeamini kwenye mpira kila mtu anajicho lake
 
monopoly inc

monopoly inc

JF-Expert Member
Joined
Dec 20, 2016
Messages
2,117
Points
2,000
monopoly inc

monopoly inc

JF-Expert Member
Joined Dec 20, 2016
2,117 2,000
Mkude anamapungufu yake mara nyingi amekuwa off kwenye eneo lake angalia goli waliofunga Burundi yeye alikuwa wapi ,tuangalie mchezaji mmojammoja
Hata mechi na UD SONGO yeye ndie alifanya turn akapoteza mpira then akacheza rafu
 
herzegovina

herzegovina

JF-Expert Member
Joined
Oct 28, 2015
Messages
2,289
Points
2,000
herzegovina

herzegovina

JF-Expert Member
Joined Oct 28, 2015
2,289 2,000
Mkude is OVERRATED

OVER
 
An Eagle

An Eagle

JF-Expert Member
Joined
Feb 11, 2019
Messages
1,204
Points
2,000
An Eagle

An Eagle

JF-Expert Member
Joined Feb 11, 2019
1,204 2,000
Siku mpira ukiwakataa Mkude na Kaseja tutasema ndio maana Akili kubwa Amunike hakuwaita Timu ya Taifa
Namzungumzia Jonas Gerald Mkude na simzungumzii Juma Kaseja Juma tafadhali. Na bahati nzuri nimemuelezea vyema Kiufundi hasa nikiwa kama Mtu ambaye pia nimeucheza huo Mpira wenyewe japo sikufikia Viwango hivi vya Ligi kutokana na Majukumu mengine ya Kitaaluma na hata Kimaisha ila sijaanza Kumjua na Kumfuatilia Jonas Gerald Mkude leo na ndiyo maana hata hivi ninavyomjadili na kumuelezea hapa najiamini kabisa kwa 100% kuwa namkubali kwani ana 85% ya Sifa zote zote ambazo Kiungo bora na wa Ukabaji wa miaka ya sasa anatakiwa awe nazo japo nakiri kuwa ana Mapungufu yake hasa yaliyotokana na Makuzi yake na pia Tanzania kutokuwa na Mfumo mzuri wa Kuwaibua, Kuwatengeneza na Kuwakuza hawa Wachezaji wetu. Ila kwa sasa Mkude katika Kiungo cha Ukabaji ( Dimba la Chini ) hasa Namba Sita hana Mpinzani na nina Uhakika katika Mechi hizi alizocheza au hizo za Makundi ambazo atacheza na Taifa Stars anaweza Kuonekana na Mawakala wakubwa na hata Kuchukuliwa na Timu kubwa huko Ulaya na Klabu ya Simba ikafaidika nae Kimauzo na Timu yetu ya Taifa nayo ikafaidika nae zaidi kwakuwa atakuwa ameenda daraja lingine ambapo atakutana na Makocha wakubwa na watampika zaidi Kimataifa.

Yule ' Mpuuzi ' wenu Emanuel Amunike atuombe Radhi Watanzania kwa Kumchukia kuliko maelezo Kiungo huyo bora Mkude.
 
kimbendengu

kimbendengu

JF-Expert Member
Joined
Jun 7, 2013
Messages
2,993
Points
2,000
kimbendengu

kimbendengu

JF-Expert Member
Joined Jun 7, 2013
2,993 2,000
Santino mimi ni mwanamichezo wa kuangalia mpira timu yote kuanzia benchi la ufundi ,wachezaji wote Tanzania na Burundi hivyo sijadili mchezaji ametoka timu Gani naangalia uwezo wa mtu ,ubora wa kiungo mkabaji yeyote duniani tunampa alama kwa takolingi zake ,kiungo mchezesheji tunampa alama kwa kugawa au kusambaza mipira kwa wenzake sasa naomba mliokwenda uwanjani Jana mniambie mkude alifanya takolingi ngapi?
 
An Eagle

An Eagle

JF-Expert Member
Joined
Feb 11, 2019
Messages
1,204
Points
2,000
An Eagle

An Eagle

JF-Expert Member
Joined Feb 11, 2019
1,204 2,000
Mkude anamapungufu yake mara nyingi amekuwa off kwenye eneo lake angalia goli waliofunga Burundi yeye alikuwa wapi ,tuangalie mchezaji mmojammoja
Akili zako za ' Kipa Katoka ' hazipishani sana na za Emanuel Amunike. Umecheza Mpira wapi na wa Kiwango gani Ndugu? Hebu tuanzie hapa Kwanza.
 
kimbendengu

kimbendengu

JF-Expert Member
Joined
Jun 7, 2013
Messages
2,993
Points
2,000
kimbendengu

kimbendengu

JF-Expert Member
Joined Jun 7, 2013
2,993 2,000
Akili zako za ' Kipa Katoka ' hazipishani sana na za Emanuel Amunike. Umecheza Mpira wapi na wa Kiwango gani Ndugu? Hebu tuanzie hapa Kwanza.
😀😀😁 Umepanika mjomba Lete takwimu za mkude hasa za takolingi ,pia wewe amunike humjui
 
An Eagle

An Eagle

JF-Expert Member
Joined
Feb 11, 2019
Messages
1,204
Points
2,000
An Eagle

An Eagle

JF-Expert Member
Joined Feb 11, 2019
1,204 2,000
Mkude ni kiungo mzuri lakini kuna makosa mengi sana anayafanya kwenye jukumu la kukaba mpaka msimu uliopita alipewa msaada wa kotei,

Kitu pekee kinachombeba Mkude ni timu anayochezea ya Simba ina profile kubwa hivyo inamfanya aonekane kiurahisi

Mleta Mada ligi ishaanza naomba ukawachunguze hawa watu

1; Antony Majogoro
2;Freddy Tangaru
3;Alex massawe
4;Shabban Nditi
5;Awadh salum
6;Ally msengi
8;Jimmyshoji Mwaisondola
9; kuna dogo Yupo alliance uliempiga dole gadiel Michael nimemsahau jina
Hawa Wachezaji wako uliowataja hapa hawajafikia hata 15% tu Uwezo alionao Jonas Gerald Mkude labda uniambie kuwa hawa Wachezaji wako tajwa hapa wanatakiwa kila mara wakisikia Mkude ' anakiwasha / anacheza ' wawe wanamtizama ili waendelee Kujifunza Kwake.

Huyo James Kotei wako ( ambao wana Simba SC tulimbatiza Jina la Nyigu alilokuwa nalo Mchezaji wetu wa zamani Idi Selemani ) kila alipokuwa akiulizwa anapenda Kucheza na nani katikati mara zote alikuwa akimtaja Jonas Gerald Mkude kwa Hoja yake Kuu kuwa anapocheza nae huwa anamrahisishia Kazi kwani Mkude huwa ana Pasi zenye Macho ( wenyewe Wadau wa Mpira tunaziita Pasi Mpenyezo au Pasi Kofi ) na nakumbuka alishasema kuwa Mkude mara zote ndiye amekuwa Mpangaji wa Timu ichezeje huku Clatous Chota Chama akiwa na Jukumu la Kuamua Timu ifunge muda gani.

Sijaona kama Jonas Gerald Mkude kwa sasa iwe kwa Simba SC au hata kwa Taifa Stars. Anazidi Kumuumbua ' Mpuuzi ' Amunike.
 
An Eagle

An Eagle

JF-Expert Member
Joined
Feb 11, 2019
Messages
1,204
Points
2,000
An Eagle

An Eagle

JF-Expert Member
Joined Feb 11, 2019
1,204 2,000
Mkuu unaujua mpira??kwa hiyo goli lililofungwa jana lawama tumpe mkude 😂 😂 😂 😂 ...nimeamini kwenye mpira kila mtu anajicho lake
Ndugu acha Kupoteza muda na hao Watu ambao Kwanza Mpira wenyewe tu hawaujui na wala hawajaucheza pia. Watakusumbua bure! Wengi wao ni wale walioanza Kufuatilia Mpira miaka hii ya 2000 tena baada ya Kuja kwa Kocha Jose Mourinho. Na ukiwachunguza wengi wao utawakuta ni Mashabiki wa Chelsea ila ukikutana na Sisi Mashabiki wa Liverpool FC au wale wa Manchester United au Arsenal na kidogo na wa Tottenham Hotspurs unaweza ukatuelewa vyema kwani tulianza Kushabikia hii Mipira miaka mingi na Kuicheza katika Ngazi za Awali za Mashuleni hadi Vyuoni bila Kusahau Mitaani ( Ndondo ) tumeicheza sana tu.
 
Deo Corleone

Deo Corleone

JF-Expert Member
Joined
Jun 29, 2011
Messages
15,088
Points
2,000
Deo Corleone

Deo Corleone

JF-Expert Member
Joined Jun 29, 2011
15,088 2,000
Kwahiyo angekwepo mkude kule Misri tusingefungwa?
 
monopoly inc

monopoly inc

JF-Expert Member
Joined
Dec 20, 2016
Messages
2,117
Points
2,000
monopoly inc

monopoly inc

JF-Expert Member
Joined Dec 20, 2016
2,117 2,000
Hawa Wachezaji wako uliowataja hapa hawajafikia hata 15% tu Uwezo alionao Jonas Gerald Mkude labda uniambie kuwa hawa Wachezaji wako tajwa hapa wanatakiwa kila mara wakisikia Mkude ' anakiwasha / anacheza ' wawe wanamtizama ili waendelee Kujifunza Kwake.

Huyo James Kotei wako ( ambao wana Simba SC tulimbatiza Jina la Nyigu alilokuwa nalo Mchezaji wetu wa zamani Idi Selemani ) kila alipokuwa akiulizwa anapenda Kucheza na nani katikati mara zote alikuwa akimtaja Jonas Gerald Mkude kwa Hoja yake Kuu kuwa anapocheza nae huwa anamrahisishia Kazi kwani Mkude huwa ana Pasi zenye Macho ( wenyewe Wadau wa Mpira tunaziita Pasi Mpenyezo au Pasi Kofi ) na nakumbuka alishasema kuwa Mkude mara zote ndiye amekuwa Mpangaji wa Timu ichezeje huku Clatous Chota Chama akiwa na Jukumu la Kuamua Timu ifunge muda gani.

Sijaona kama Jonas Gerald Mkude kwa sasa iwe kwa Simba SC au hata kwa Taifa Stars. Anazidi Kumuumbua ' Mpuuzi ' Amunike.
Shaban Nditi ajifunze kwa mkude? Labda kama mimi siujui mpira
 
Forum statistics

Threads 1,336,612
Members 512,670
Posts 32,545,204
Top