Kiungo wangu bora wa ' Ukabaji ' nchini Tanzania kwa sasa Jonas Gerald Mkude a.k.a Deco De Souza amuumbua ' Mpuuzi ' Amunike

Mbona mechi ya UD Songo hakusababisha Simba ishinde na kuzuia lile goli au hakucheza?
 
Mkude hamna kitu humo, butua butua tu.
 
Muongeze
Ismail Gambo
 
Mudahir yahya abas akiwa fiti mkude hagusi pele subirini apone kama mtamuona mkude kwenye kikosi cha ndairagije
 
Sema wanasimba nao ni waseenge sometime... Ni watu wa kupagawa na wasio ni fikra pembuzi za uchambuz wa mpira... Ukifanya kizuri mara moja au kibaya.. Iwe kwa kukosea au makusudi.

Uo ndio utakuwa mnwanzo wa shutuma au kusifiwa... Na mengine na wengine woote watasahaulika.

Leo hii kweli useme mMkude ni Bora kuliko KOTEI.

Aiseee
 
Soka la bongo na wabongo wenyewe... Teteteteeeh,... Eti mkude ni kiungo bora wa ukabaji... Mkude ni Kati ya viungo wabovu na wavivu kwenye ukabaji,.. Kotei alifanya kazi na kumfichia aibu mkude,... Mechi ya UD SONGO alikua chochoro na mipira mingi sana wale jamaa hawakuitumia pembeni, ilikua mfereji wa mkude... Mechi ya Burundi nimeziona fyongo nyingi saaana kwa mkude,... Ila bongo tuna ule ualikiba na udiamond mpk kwenye mpira,.... Usimba na uyanga... Ila Amunike alikua na jicho sahihi kwa upande wangu... Sio bora.
 
Uyu jamaa ata simba kwasasa atufai kwanza ana pas acurensi jamaa ni mzito kwenye matukio awe anamchek obi mikael alikuwa anafany nini ajifunze
 
Embu jitathmini,wachangiaji wangapi wameyaona mapungufu ya mkude na wameweka wazi hapa
Lkn pia wangapi wamempa credit za kutosha nditi.

Alafu nani kakwambia kipa atakiwi kutoka golini ww mjomba kaka,,,?
Akili yako ya ' Kipa Katoka ' ni kama aliyokuwa nayo Mwenzako ' Mpuuzi ' Kocha niliyekuwa namchukia mno Emanuel Amunike.
 
Mkude jana mpira ulimkubali ameanz kurudisha kiwango chake cha zamani kwa kiasi kikubwa alitumika kusambaza mpira ila mkude wa sasa ana mapungufu ya kukaba huwa hakai sehemu sahihi Mkude anahitaji kucheza akiwa na mtu mwenye aina ya uchezaji wa James Kotei
 
Sijawahi kumuona Mkude kama Kiungo Mkabaji, ni kwamba anacheza eneo LA ukabaji lakini hajawahi kucheza kama kiungo mkabaji, Mkude ni mzuri sana timu inapokuwa na mpira, hapo utampenda sana, anajua kujiposition na kutoa pasi kwa wenzake, uwezo wake wa kunyang'anya mpira bila kucheza faulo ni mdogo sana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…