Kiungo wangu bora wa ' Ukabaji ' nchini Tanzania kwa sasa Jonas Gerald Mkude a.k.a Deco De Souza amuumbua ' Mpuuzi ' Amunike

Huenda angeyapunguza Magoli na hata Kusababisha Washambuliaji wetu nao Wafunge Magoli hasa kutokana na Uwezo wake wa Kujua Kuwachezesha na Kuichezesha Timu. Mtu yoyote ambaye anaujua vyema Mpira na pia amebahatika Kuucheza vile vile hatonishangaa An Eagle kwanini namsifia na namkubali kuliko Maelezo ' Mwanangu ' mwenyewe Jonas Gerald Mkude a.k.a Deco De Souza.
Mbona mechi ya UD Songo hakusababisha Simba ishinde na kuzuia lile goli au hakucheza?
 
Sijawahi Kupenda vibovu vibovu hata Siku moja na nilisema kuwa kwa sasa Tanzania bado sijaona Kiungo Mkabaji bora kama Mdogo wangu mwenyewe Jonas Gerald Mkude ila kuna Watu walinipuuza lakini kwa Kazi ya Mkude Uwanjani sasa amewajibu na wamenyamaza.

Ni Kocha ( Mwalimu ) Mpumbavu tu kama si Mpuuzi wa mfano wa yule Kocha ambaye alibahatisha Kutupeleka AFCON 2019 na kwa Msaada mkubwa wa Ujirani mwema wa Uganda na Tanzania lakini pia akatuwekea Rekodi ya pekee huko Misri kwa Tanzania kufanya vibaya mechi zote na kukosa hata Alama moja tu ndiyo hatoona Umuhimu wa Kiungo wangu Kipenzi na Fundi kabisa katika Dimba la Kati ( hasa upande wa Ukabaji ) kama Jonas Gerald Mkude.

Utasemaje Mkude hafai huku karibia Makocha wote wakubwa na mahiri ambao wamewahi Kuifundisha Simba SC na hata Timu ya Taifa walishasema kuwa kwa sasa Tanzania nzima hakuna Mchezaji wa Kiungo hasa cha Ukabaji na anayejua Majukumu yake vyema kama Jonas Gerald Mkude? Na ukiona Kocha anamchukia Mkude jua anamuonea Wivu tu au ana Chuki nae binafsi au ana ' Udalali ' na baadhi ya Wachezaji ili awauze Ulaya na apate 10% yake.

Namwomba aliyekuwa Kocha wa Taifa Stars Emanuel Amunike a.k.a Mpuuzi aje atuombe Radhi haraka Watanzania kwa Kitendo chake cha Kutudanganya juu ya Uwezo wa Kiungo Jonas Gerald Mkude huku akimtangaza vibaya kuwa ni Muhuni ( Mvuta Bangi ) wakati Mimi kama An Eagle nawajua zaidi ya Wachezaji wa Taifa Stars tena ' Waandamizi ' kabisa ambao ni Wavuta Bangi mahiri na wazuri kuliko hata huyu Mwanangu mwenyewe Mkude.

Kwa aina ya Mpira wa Kiwango cha juu ambao anaucheza sasa Mkude nina uhakika huyu Kocha ' Mpuuzi ' Emanuel Amunike huko aliko sasa anaona Aibu na anajisikia vibaya mno kwani ' Dogo ' Mkude anamdhihirishia kuwa alizaliwa kuja kuwa ' Kiungo Mkabaji ' na pia aliye na ' tuvituvitu ' vitamu vitamu Uwanjani huku akiichezesha Timu anavyotaka na akiwapa Likizo / Nafuu Mabeki ' Waandamizi ' wa Stars ambao pia ni Kaka zake Kiumri akina Yondani na Nyoni.

Ni Wachezaji Watatu tu kama si Wanne ambao tokea Timu hii Taifa iwe chini ya ' Mtaalam ' Kocha Ndayiragije ndiyo hawakubadilishwa au hata Kupumzishwa katika Mechi ambazo Timu imecheza na huyu ' Mwanangu ' mwenyewe Mkude nae akiwemo na hii inathibitisha kwamba Kocha na jopo lake wakiwemo akina Juma Mgunda na Kocha ambaye ndiyo alimuibua, amemtengeneza na kumpika Mkude hivi Suleiman Abdallah Matola a.k.a Veron a.k.a Mzambia hawana Mashaka nae na wanakikubali kile ambacho anakifanya hasa katika Dimba la Chini ( Kiungo cha Chuma )

Na tokea Mkude arejeshwe Taifa Stars ndiyo nimekuwa na Mapenzi nayo sasa na huenda ndiyo maana inabarikiwa vile vile japo tusifichane wala kupeana Moyo kwa hatua hii ya Makundi ambayo tunaenda Kupangwa sasa ndiyo tukicheza tufanikiwe kwenda katika Fainali za Kombe la Dunia huko Qatar mwaka 2022 hapa ndiyo mwisho wetu kwani ili tufanikiwe tunahitaji Maandalizi makubwa na kabambe tena mengi ni ya Kiufundi zaidi kitu ambacho sidhani kama kwa sasa Tanzania tutakiweza ila tukianza Maandalizi sasa ya Kombe la Dunia la 2026 nina uhakika tunaweza Kushiriki.

Hongera sana ' Mwanangu ' mwenyewe Jonas Gerald Mkude kwani unalikamata Dimba la Kati kama vile ninavyotaka. Watakukoma!
Mkude hamna kitu humo, butua butua tu.
 
Mkude ni kiungo mzuri lakini kuna makosa mengi sana anayafanya kwenye jukumu la kukaba mpaka msimu uliopita alipewa msaada wa kotei,

Kitu pekee kinachombeba Mkude ni timu anayochezea ya Simba ina profile kubwa hivyo inamfanya aonekane kiurahisi

Mleta Mada ligi ishaanza naomba ukawachunguze hawa watu

1; Antony Majogoro
2;Freddy Tangaru
3;Alex massawe
4;Shabban Nditi
5;Awadh salum
6;Ally msengi
8;Jimmyshoji Mwaisondola
9; kuna dogo Yupo alliance uliempiga dole gadiel Michael nimemsahau jina
Muongeze
Ismail Gambo
 
Mudahir yahya abas akiwa fiti mkude hagusi pele subirini apone kama mtamuona mkude kwenye kikosi cha ndairagije
 
Sema wanasimba nao ni waseenge sometime... Ni watu wa kupagawa na wasio ni fikra pembuzi za uchambuz wa mpira... Ukifanya kizuri mara moja au kibaya.. Iwe kwa kukosea au makusudi.

Uo ndio utakuwa mnwanzo wa shutuma au kusifiwa... Na mengine na wengine woote watasahaulika.

Leo hii kweli useme mMkude ni Bora kuliko KOTEI.

Aiseee
 
Soka la bongo na wabongo wenyewe... Teteteteeeh,... Eti mkude ni kiungo bora wa ukabaji... Mkude ni Kati ya viungo wabovu na wavivu kwenye ukabaji,.. Kotei alifanya kazi na kumfichia aibu mkude,... Mechi ya UD SONGO alikua chochoro na mipira mingi sana wale jamaa hawakuitumia pembeni, ilikua mfereji wa mkude... Mechi ya Burundi nimeziona fyongo nyingi saaana kwa mkude,... Ila bongo tuna ule ualikiba na udiamond mpk kwenye mpira,.... Usimba na uyanga... Ila Amunike alikua na jicho sahihi kwa upande wangu... Sio bora.
 
Uyu jamaa ata simba kwasasa atufai kwanza ana pas acurensi jamaa ni mzito kwenye matukio awe anamchek obi mikael alikuwa anafany nini ajifunze
 
Embu jitathmini,wachangiaji wangapi wameyaona mapungufu ya mkude na wameweka wazi hapa
Lkn pia wangapi wamempa credit za kutosha nditi.

Alafu nani kakwambia kipa atakiwi kutoka golini ww mjomba kaka,,,?
Akili yako ya ' Kipa Katoka ' ni kama aliyokuwa nayo Mwenzako ' Mpuuzi ' Kocha niliyekuwa namchukia mno Emanuel Amunike.
 
Mkude jana mpira ulimkubali ameanz kurudisha kiwango chake cha zamani kwa kiasi kikubwa alitumika kusambaza mpira ila mkude wa sasa ana mapungufu ya kukaba huwa hakai sehemu sahihi Mkude anahitaji kucheza akiwa na mtu mwenye aina ya uchezaji wa James Kotei
 
Sijawahi kumuona Mkude kama Kiungo Mkabaji, ni kwamba anacheza eneo LA ukabaji lakini hajawahi kucheza kama kiungo mkabaji, Mkude ni mzuri sana timu inapokuwa na mpira, hapo utampenda sana, anajua kujiposition na kutoa pasi kwa wenzake, uwezo wake wa kunyang'anya mpira bila kucheza faulo ni mdogo sana
 
8 Reactions
Reply
Back
Top Bottom