Kiumbe kinachoitwa ‘mke’ kiogope

umenena vema sana
 
Mpaka nasema kuachiwa majukumu means natumia pesa yangu kulea watoto wakati pesa yake haiwajibiki.....Ukitaka kuwa mwanaume wajibika mkuu
Sasa tuongelee mwanaume ambaye amekwama kifedha ambaye mlianza vizuri tu. Ikitokea hali yake haipo vema ndio iwe sababu ya wewe kukorofishana nae?!
 

Hivi katika viumbe wanaojua kulalamika wanawake umeshindwaje kuwaona?! Shida ni hawanaga hoja za msingi. Ni watu wa kutengeneza sababu.

Mwanamke anaweza kuwa hajaridhika na jambo akatengeneza mazingira mgombane mkikorofishana anasingizia jambo lingine kabisa na kutaka wewe uonekane ndie msababishaji wa huo ukorofi.
 
Mpe matumizi mazuri
Mpe nyumba nzuri
Mpe gari nzuri
Mpe mapenzi ya kutosha
Mpe pesa ya kutosha- hata awe anakutunzia tuu impe uhakika wa maisha



Halafu Rudi utuambie kama bado ana kiburi
Mama yako alipewa vyote hv? Na baba yako.
 
Tunakosa uhalisia sabbu tunaona malalamiko ya upande mmoja lkn sijamaanisha kuwa natetea wanawake lakini pia tujitathimini matendo yetu pia huenda yanaturudia lkn tunasahau tulofanya huko nyuma
 
Hapo umetaja wanaume karbia sita tofauti

Hapana mkuu, huyo ni mwanaume mmoja tuu mwenye malengo yake
Yaani kila baada ya muda anapiga hatua moja mbele inavyozidi kuweka familia yake imara
 
Sasa tuongelee mwanaume ambaye amekwama kifedha ambaye mlianza vizuri tu. Ikitokea hali yake haipo vema ndio iwe sababu ya wewe kukorofishana nae?!
Hapana,baba huyo anasababu zake ivo ukiingiza ugomvi kisa ameshuka bas huko ndo tunaita roho mbaya sasa
 
Mpaka nasema kuachiwa majukumu means natumia pesa yangu kulea watoto wakati pesa yake haiwajibiki.....Ukitaka kuwa mwanaume wajibika mkuu

Kanuni ya kuwajibika haimlengi mwanaume tu hata mwanamke pia. Ndoa ni kuwajibika kwa kila mtu. Ukiingia kwenye ndoa kila mtu azidishe haso zake mara mbili ili kuendesha ndoa yenu. Ndoa si sehemu ya mmoja kupumzika na kuvuna na mwingine ahenye kwa dhana kuwa"- YEYE NI PROVIDER. Ikiwa umeolewa na hauna chochote unachochangia katika huo muungano wenu zaidi ya sehemu zako za siri huo ni ulaghai.

Mimi nimezaliwa katika family ya wazazi wawajibikaji (sio MUAJIBIKAJI kwa maana ya upande mmoja) wote. Mimi naenda kuchunga Baba na Mama wapo shambani asubuhi na jioni. Wanatoka shambani mama ana kuni kichwani wameambatana na Mme wake.. Hayo ndiyo yalikuwa maisha yao ya kila siku.
Policy ni ile ile:KABLA YA KUJIULIZA MMEO KAKUFANYIA NINI CHA MAANA TOKA UMEISHI NAE JIULIZE KWANZA WEWE UMEMFANYIA NINI.

Dhana ya kuwa Mwanaume ni provider na mke ni mpokeaji tu"chake chenu, chako chako" inapigiwa zumari zaidi na mananake mafeminist. Yale Madada yenye makucha marefuuu ndio uimba huo wimbo mara zote.

Mwanamke njoo kwangu kama aset na sio liability. Njoo tuwajibike tutengeneze regency yangu na wewe.
Nimekupata huna kitu"sawa" ilo ni jukumu langu la kukuwezesha na kukufanya uwe aset kwangu si liability.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…