Binafsi ninakerwa na serikali hii inavyofanya mambo yake. Kuna mambo yanahitaji diplomacy kidogo tu ila cha kushangaza serikali inatumia nguvu kupitiliza hadi inaamsha hasira za wananchi. Kuna ishu zinahitaji tu maneno sio lazima kutumia bunduki. Msemaji wa serikali na katibu mwenezi wa CCM ni kama wameshindwa kazi zao. Wanaomshauri Rais na mwenyekiti wa CCM ni watu wanaomhujumu badala ya kumsaidia.
Lakini siungi kabisa mkono wanaodhani USA na ndugu zake wa Ulaya watatusaidia. Hawa mabeberu hujali maslahi yao tu hata kama mtakufa na njaa. Hawana huruma zozote. Historia ni shahidi mzuri wa matendo yao maovu. Hayati Patrick Lumumba aliuwawa kikatili na hawa mabeberu. Mifano ni mingi kuhusu wazalendo waliouwawa na hawa mabeberu. Hawa ni mambwa yanayojali maslahi na sio ustawi wa watanzania. Kamuzu Banda alikuwa kipenzi chao wakati wa ubaguzi wa rangi Afrika kusini kiasi kwamba kulikuwa na direct flights Malawi hadi Ulaya na USA ila mara baada ya ubaguzi kwisha mashirika yote yakasitisha kwenda Malawi na hadi leo Malawi ni nchi maskini kwenye tatu bora za maskini wa dunia.
Watanzania sidhani kama mnasahau mikataba ya kihuni migodini tuliyosainishwa na hawa wahuni. Wanajichotea natural resources za mabilioni huku wakitudanganya na vijisenti. Kwa mfano European Union imesitisha msaada wa Bilioni 400 tu ambayo ni hela kiduchu sana. Bilioni 400 ni punje kwenye mapato ya madini peke yake. Mbaya zaidi misaada yao huwa na masharti ya kisenge sana. Kwa mfano USAID ikikupa msaada wa fedha za kununulia vifaa tiba itakulazimisha ununue hivyo vitu kwa manufacturers wa USA au UK ambapo kwa lugha rahisi pesa yote hurudi kwao.
Ninashauri kama nchi tukae chini kwa maridhiano na kukubaliana twende vipi kwa pamoja badala ya kuwahusisha hawa washenzi wa USA na Ulaya.
Mheshimiwa Dr Samia, Rais na mwenyekiti wa chama pendwa CCM ninakusihi fanya jambo kwa kushirikiana na wenye busara serikalini kutuliza hii hali iliyopo. Njia za kidiplomasia ni njema kuliko nguvu nyingi kutumika.