Petro E. Mselewa
JF-Expert Member
- Dec 27, 2012
- 10,346
- 26,143
- Thread starter
-
- #81
Nisamehe Mkuu kama nimekukwaza. Ni mawazo yangu binafsi Mkuu sana MAGALEMWAMsahihisho mkubwa
1. Sitarajii kuwa toka kwako kuwa Lowasa hana haki kikatiba kujiunga na chama chote isipokuwa CCM.
2. CHEDAMA inaendeshwa kwa katiba yake na itikadi zenye sera madhubuti kwa kila jambo kwa hiyo kufikiri kuwa inaendeshwa kwa ajenda nikushauri tu labda huko kwenye chama dola. Labda ungenilinganishia agenda ya chama dola ni nini?
3. Mimi ni kama wewe sina chama ila naipenda CHADEMA kwa katiba yake itikadi yake na misimamo yake iliyotofauti na chama dola cha dikteta uchwara. Sababu moja kuu ni kuwa chama dola hakina sera wala mwelekeo (Kolimba). Kinaishi kwa matakwa ya vyombo vya dola. Hakina ushiriki wa wananchi tulio wengi zaidi ya ubabe na ukandamizaji.
4. Nakuheshimu kama msomi tena "Learned Brother " ila nakusitikia kuchambua kwako kunakoelemea personalities badala ya issues. Sioni tofauti yako na akina Lisaboni na wale wachangiaji wa Lumumba bk 7.
5. Jiulize tungekuwa na sera inayokubalika kitaifa (kupitia sanduku la kura huru)na uongozi shirikishi tungekuwa wapi baada ya zaidi ya miaka 50 ya kujitawala.
Zidumu fikra duni za chama dola
Sawa,nitajitahidiMkuu huna haja ya kuomba msamaha naheshimu maoni yako ila matarajio yangu toka kwako ni hoja bora kuliko uliyoandika.
No wonder Rais hataki kufukua Makaburi ........ akiyafukua anaweza akawa ndiyo anamsafisha Lowasa!!Msema ukweli ni mpenzi wa Mungu. Humu humu JF nimewahi kuandika hivi: Sikubaliani na hoja ya Lowassa Kujiengua CCM na Kujiunga CHADEMA/UKAWA. Andiko langu hilo, nikiwa kama mtanzania nisiye na chama chochote cha siasa, lililenga kukosoa kujiunga kwa Lowassa huko CHADEMA.
Maneno hayo sasa yanakuwa ya uhalisia. Tangu Lowassa ajiunge CHADEMA, pamoja na kinachosemwa kuwa CHADEMA/UKAWA imeongeza idadi ya Wabunge na kuminywa kwa demokrasia, wanaCHADEMA kindakindaki wamekuwa kama 'wamejitenga' na chama chao. Wanakosa hoja za kukosoa masuala ya ufisadi kwakuwa waliyekuwa wakimsema sasa wanaye.
Tangu Lowassa kujiunga na CHADEMA, CCM imeibeba ajenda ya kupambana na ufisadi. Haikuwahi kutokea CCM kutamka hadharani kupambana na ufisadi kwenye kampeni zake au hata kwenye utawala wake kwa kujiamini kuliko kuanzia siku Lowassa alipojiunga na CHADEMA. Ufisadi, kama hoja ya kujidai kwa wananchi, umepokwa na CCM toka CHADEMA!
Kimsingi, hata kama ni kimya kimya, Lowassa anaitesa CHADEMA. Anawabana wasipate cha kusema kuhusu ufisadi. Imekuwa rahisi kwasasa kwa wanachama wa CCM kupindisha kila hoja ya ufisadi toka kwa CHADEMA kwa kusema kuwa hata Lowassa aliyesemwa miaka nenda miaka rudi naye yuko CHADEMA.
Msahihisho mkubwa
5. Jiulize tungekuwa na sera inayokubalika kitaifa (kupitia sanduku la kura huru)na uongozi shirikishi tungekuwa wapi baada ya zaidi ya miaka 50 ya kujitawala.
Zidumu fikra duni za chama dola
LumumbaKwa hiyo nani ayafanye hayo yote uliyoyataja? Au ndiyo kama yule anayemlaumu baba yake kwa kushindwa kwake maisha ?
Rasimu/Katiba ya Warioba ndio jibuKwa hiyo nani ayafanye hayo yote uliyoyataja? Au ndiyo kama yule anayemlaumu baba yake kwa kushindwa kwake maisha ?
Weye wapewa bk 7, wenzio wala 10m.Ni shabiki wa kutupwa wa cdm na msimamo wangu uko wazi. Walichokifanya cdm ni kama kuwa vitani halafu unamchukua kamanda wa wapinzani wako na kumpa ujemadari kupambana na huko akikotoka. Kibaya zaidi huyo kamanda mamluki hana uwezo wa kujenga hoja zaidi ya siasa za chini ya meza. Hv viongozi wa cdm hamuoni haya malalamiko yetu kila siku kwamba hapo tumelamba galasa?
Rasimu/Katiba ya Warioba ndio jibu
Kwani huko lumumba, lugumi keshakuwa fisadi?Huitaji hata cheti cha darasa la 7, kumpa ushauri lugumi, juu ya njia rahisi na nyepesi ya kujisafisha ktk jamii ya watanzania kutokana na tuhuma zinazomuangukia, bila kujali kama ni kweli, au la....
...ni kujiunga na chadema tu, kama alivyofanya lowassa!
Weye wapewa bk 7, wenzio wala 10m.
Kama hamuiogopi, kulikuwa na haja ya kupigisha kura mpaka marehemu?Hata Katiba ikibadilishwa na kuwekwa mnayoitaka nyie bado CCM itashinda uchaguzi tena kwa tofauti kubwa sana tu na mtarudi hapa na malalamiko yale yale tu, tunayaona Kenya!
PoleSijawahi kuishabikia ccm na wala sidhani kama nitawahi, ikiwemo huyo Lowassa. Kwa hiyo hizo unazoziita bk 7 sijui 10m sizitambui, ila nakuambia ukweli ni kuwa hyo Lowassa kwa cdm ni kama wali umeingia mawe.
Kama hamuiogopi, kulikuwa na haja ya kupigisha kura mpaka marehemu?
Mkuu Bujibuji sijawahi kujiunga na CHADEMA wala chama chochote ndani au nje ya Tanzania. Anayeweza kuniumbua aniumbue kwa ushahidi.Wee Peter a.k.a Petro E. Mselewa unasema huna chama chochote? Wee si mnazi wa Chadema wewe!!!! MUNGU hampendi mnafiki wacha unafiki
Pole