Kituo gani kizuri kwa QT hapa Dar?

Nimesoma hadi level ya degree ya kwanza.
kwanza ongera kwa hilo

ajira auna sio?

chengine bahat naweza nikasoma nabado mambo yakawa magumu najua ila sito kata tamaa kwasasa nimekosa fulsa nyingi sababu sina vyeti ngoja nivitafute nione kwan akuna anaye ijua kesho itakuaje
 
daaaa nikweli mawazo yako ni sahihi

ila bora ufe ukiwa una vyeti kuliko hiv maana maumivu ninayo yasikia kukosa kwenda shuleee achaaa!
apa nilipo nishapiga boda boda nasasa niko kwenye shuhuri za uwakala ilaa nataka nisome nipate ata kazi ya ualimu maana umri ndio unaenda naona mudaa upoo

Kama upo serious na shule narudia tena kasomee fani hutojutia. Hayo mambo ya kutegemea uajiriwe utakuja kujutia time yako na pesa yako ulioipata kwa shida na kisha kuiteketeza kwenye ada. In fact elimu yetu ya secondary haikupi mwanga wowote wa kubobea katika field fulani.

Kwa taarifa tu, ukimaliza kidato cha 4 ukapata alama za kuendelea mbele utapaswa uwe na pesa ya kuingia advance level ukasome kidato cha tano na sita. Hapo utakua huna sifa za kusoma shule ya serikali maanake ukajilipie private school.

Ukifanikiwa kutoboa kidato cha 6 utatakiwa kwenda chuo kikuu. Kama unavyoona ulivyo utawala wa sasa hivyo basi kupata mkopo wa chuo ni sawa biashara ya bible uarabuni. Wataànza kukuchunguza umesoma QT ambayo ni private, a level nayo ni private wata conclude unajimudu pasipo kujua umepitaje pitaje, hapo sahau kabisa mkopo. Swali je utakua na pesa ya kujiendeleza?

Au tuseme umemaliza kidato cha nne ukapata alama nzuri labda uende chuo cha ualimu ukasomee ualimu wa shule ya msingi ila pia huko utatakiwa kujilipia.

Faida ya kwenda kusomea ufundi ukitoka hapo wewe ni fundi tayari. Ukichagua fani nzuri na ukiwa mbunifu basi huwezi kulala njaa mtaani. Huko kwingine kuna kufeli pia hilo liweke akilini.

Anyway just ushauri tu ila mwenyewe utakua una mikakati yako.
 
Sidhani kama utaeleweka kwa wepesi ushauri mzuri ila si rahisi kueleweka.
Mkuu vigumu sana kunielewa labda huenda ile status ya nimesoma ina mpa simanzi mleta uzi.

Ila kwa miaka 21 kuanza sec ni gamble. Wengine tumesoma coz tulikua katika umri wa kusoma na pia ilikua ni sehemu moja wapo ya ukuaji. Kwa zama hizi ukimaliza darasa la saba unajikuta una miaka 13,14 ikizidi sana 15 bado ni mtoto so kwenda sec school ni sahihi kabisa kujikomaza kiakili.
 
Kama upo serious na shule narudia tena kasomee fani hutojutia. Hayo mambo ya kutegemea uajiriwe utakuja kujutia time yako na pesa yako ulioipata kwa shida na kisha kuiteketeza kwenye ada. In fact elimu yetu ya secondary haikupi mwanga wowote wa kubobea katika field fulani.

Kwa taarifa tu, ukimaliza kidato cha 4 ukapata alama za kuendelea mbele utapaswa uwe na pesa ya kuingia advance level ukasome kidato cha tano na sita. Hapo utakua huna sifa za kusoma shule ya serikali maanake ukajilipie private school.

Ukifanikiwa kutoboa kidato cha 6 utatakiwa kwenda chuo kikuu. Kama unavyoona ulivyo utawala wa sasa hivyo basi kupata mkopo wa chuo ni sawa biashara ya bible uarabuni. Wataànza kukuchunguza umesoma QT ambayo ni private, a level nayo ni private wata conclude unajimudu pasipo kujua umepitaje pitaje, hapo sahau kabisa mkopo. Swali je utakua na pesa ya kujiendeleza?

Au tuseme umemaliza kidato cha nne ukapata alama nzuri labda uende chuo cha ualimu ukasomee ualimu wa shule ya msingi ila pia huko utatakiwa kujilipia.

Faida ya kwenda kusomea ufundi ukitoka hapo wewe ni fundi tayari. Ukichagua fani nzuri na ukiwa mbunifu basi huwezi kulala njaa mtaani. Huko kwingine kuna kufeli pia hilo liweke akilini.

Anyway just ushauri tu ila mwenyewe utakua una mikakati yako.
pesa kwa kiasi furani sio tatizo kuna baba na kaka mkubwa ndio waliuza nn nataka kusomea na mwaka 2014 nli enda kusomea udeleva nkapata resen ilaa mambo yalele 2
 
samahan ww umesoma mpaka level gan?
Nenda Kyomo Adult Secondary School,kama unatokea Tegeta au Mwenge shuka kituo cha Africana au Rafia,uliza njia inayoelekea Salasala,ukioneshwa,ifuate mpaka utakapoona kiwanda kidogo cha ku'treat nguzo na mbao kipo mkono wa kushoto.songa mita 50 mbele utaona vijana wanafyatua tofali,waulize hao!
 
ok sema mimi niko mbagala
 
Back
Top Bottom