Kituo cha Mwendokasi Karume kinajengwa juu ya makaburi

Kituo cha Mwendokasi Karume kinajengwa juu ya makaburi

Panga Makalikuwili

JF-Expert Member
Joined
Aug 30, 2016
Posts
301
Reaction score
439
Eneo lile lilikuwa na makaburi kabla ya kupitisha Barabara pale. Magari yanapita juu makaburi. Kwa kipande kidogo tulichochimba kwa ajili ya kujenga kituo tumekuta makaburi mengi tu. Mifupa na mafuvu tumeacha mlemle chini na ujenzi unaendelea.
 
Kazi wanayo abiria watakapo anza kufanyiwa ndivyo sivyo kwa kuingilia bustani za mapumziko yavwatu
 
Binadamu ni mavumbi na mavumbini tutarudi, hakuna athari yeyote muhimu ni staha kuhifadhi vema masalia ya binadamu.
 
Mwanzo wanapitisha barabara hapo mwanzoni mwa miaka ya 2000 waliyahamisha makaburi barabara ipite, kwani wameshindwa nini safari hii kuyahamisha na kutaka kujenga kituo juu yake? Au wameshindwa kulipa fidia kwa ndugu wa marehemu? Imeshakuwa kawaida kufukuafukua makaburi na kuyahamisha pindi mradi unapochukua eneo la makaburi
 
Kama wamefanya hivyo kweli wamekosea sana, Waislamu wakilalamika wataitwa magaidi wawauwe.
 
Yawezekana wenye makaburi ya ndugu zao waliishayahamisha.

Pengine ndugu hawakufahamika.

Yote kwa yote huu mwili ni mavumbi tu hata siku ya ufufuo tutapewa miili mingine.

Roho zao zipo mahali salama huko Mbinguni.
 
Hata hapo unapoishi huenda kale kulikuwa na makaburi..., hii petroli inayochimbwa sasa ni viumbe hai vilivyokufa karne na karne...

Hili dude tunaloliita dunia lina muda mrefu sana ndugu yangu....
Nmecheka saaanaa
 
Wew unashangaaa apo mkuu sikuu hiz watu wanazikana juu ya makabur yaN kabur linavunjwa shimo linachimbwa apo
 
Mwanzo wanapitisha barabara hapo mwanzoni mwa miaka ya 2000 waliyahamisha makaburi barabara ipite, kwani wameshindwa nini safari hii kuyahamisha na kutaka kujenga kituo juu yake? Au wameshindwa kulipa fidia kwa ndugu wa marehemu? Imeshakuwa kawaida kufukuafukua makaburi na kuyahamisha pindi mradi unapochukua eneo la makaburi
Mkuu ,kituo kinajengwa kati ya barabara moja na nyingine, kwenye tuta linalotenganisha barabara ya kwenda na ile ya kuludi.Sehemu hii tulizani hakuna makaburi cha kushangaza kila tukichimba tunatoa masalia ya watu. Yaani hata yanapopita magari sasa hivi, chini kuna makaburi hayajaondolewa.
 
Eneo lile lilikuwa na makaburi kabla ya kupitisha Barabara pale. Magari yanapita juu makaburi. Kwa kipande kidogo tulichochimba kwa ajili ya kujenga kituo tumekuta makaburi mengi tu. Mifupa na mafuvu tumeacha mlemle chini na ujenzi unaendelea.
Waachemi wayachafue na yao siku ikifika yatafamywa hvyhvy

Sent from my A71 using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom