Kituo cha Mikutano AICC Arusha Matatani kwa kunyanyasa wapangaji Matatani

Waziri2025

Senior Member
Sep 2, 2019
148
379
Kituo cha kimataifa cha mikutano Arusha, AICC kimetuhumiwa kwa kuendeleza kukwamisha juhudi za serikali za uwepo na uanzishaji wa viwanda nchini baada ya kuweka urasimu wa Kodi kubwa na mianya ya rushwa kwenye manunuzi ya umma kwa wapangaji wake kwenye Maghala yake yalipo eneo la Esso kata ya Unga Ltd jijini Arusha .

Hatua hiyo imepelekea baadhi ya wapangaji kuyakimbia majengo ya kituo hicho cha aicc ,vikiwemo vyumba vya ofisi katika makao makuu ya aicc na kubaki magofu wakiishi vyura na popo kutokana na kupandisha kodi mara dufu.

Akiongea na waandishi wa Habari mara baada ya kutembelea kiwanda hicho kinachotengeneze bidhaa mbali mbali ikiwemo rangi za viatu aina ya Kangaroo.

Mkurugenzi wa kiwanda hicho Heladius Kanje alisema kuwa kutokana na ufinyu wa eneo analotumia aliomba kuongezewa eneo na ndipo alipoomba uongozi wa kituo hicho kupangisha katika Maghala mawili yaliyopo eneo hilo , lakini bei aliyopewa ni mara mbili ya mpangaji aliyekuwepo aliyekuwa akilipa kiasi cha sh,590,000.

Alisema kuwa maghala mawili yenye mita za mraba 384 anatakiwa kulipia kiasi cha tsh.590,000 pamoja na VAT kila moja kama bei elekezi lakini cha kushangaza nimetakiwa kulipia milioni moja laki tatu na elfu hamsini na tisa pamoja na VAT jambo ambalo linaweza kuua kiwanda chake.

Kwa mujibu wa Kanje alisema kuwa akiwa na Kampuni ya Kangaroo aliingia mkataba wa upangaji na kulipia kiasi cha milioni 1,000,057 lakini wenzangu walikuwa wakilipa kiasi cha 590,000, nilipoomba kupunguziwa walikataa na kupandisha bei iliyofikia sh, milion 1,359,000 pamoja na VAT huku wakinitishia niondoke iwapo sitaweza kulipa.

“Tokea niwe mkurugenzi hapa nimeanza na kampuni ya Ndesoma Indursty Ltd nimekuwa nalipia bei elekezi ya manunuzi ya umma kiasi cha 590,000 lakini cha kushangaza mara baada ya kuomba nalipia bei mpya kwa mwezi milion 1,359 Sisi tumewekeza karibu milion mia tano kwenye biashara huu ni urasimu mkubwa tunaomba serikali kuingalia hili kwetu sisi wajasiriamali tuliwekeza”alisema Kanje

Hata hivyo ameleeza kuwa aliomba kuongeza bei kutoka laki 5 hadi sita lakini amegundua sio fedha hizo wanaotaka bali kumekuwa na watu wenye urasimu wanaoishi kwa ten per senti jambo linalokwamisha kufikia malengo yetu na serikali kwenye uchumi wa kati wa viwanda.

Akamuomba waziri wa viwanda na biashara kufika kwa haraka kujakuona jinsi wadau wa serikali katika kufikia Tanzania ya viwanda wanavyokwamishwa kuwekeza na viongozi waliopewa dhamana ndani ya serikali wakati mh.Rais anapiga kelele hapendi kutawala watanzania wanaolia kila uchwao.

Waandishi wa habari walishudia eneo hilo la uwekezaji ambalo mwekezaji mzawa anataka kuwekeza lipo kwenye hali mbaya ya uchakavu na kuvuja jambo ambalo halipo kwenye taswira ya uwekezaji inayotakiwa na inahitajika kulifanyia ukarabati.

Ends………………………….
IMG-20190908-WA0004.jpeg
IMG-20190908-WA0006.jpeg
IMG-20190908-WA0005.jpeg
 
Ends………………………….View attachment 1201745View attachment 1201746View attachment 1201747
Labda mdau wa kiwi nae ni mpiga deals
 
Back
Top Bottom