Kituo cha Mafuta cha TOTAL Mlimani City na unyanyasaji/udhalilishaji kwa wananchi

Kwahiyo waliokufa Morogoro walikuwa kwenye Kituo cha Mafuta (Sheli)?

Halafu neno ‘Sheli’ ni cover term tu na ndio maana umeelewa nilichoandika na ukajibu! Kuna kitu kinaitwa ‘colloquial language’ na ‘slang’ muwe mnavijua! Msikariri!
Bro bro always shortcut is wrong cut
 
Kwahiyo tupite Mbinguni/hewani?
Barabara mbona ipo piteni huko huwexi komaa kupita kiwanja cha nyumba ya mtu au kiwanja cha sheli ya mtu

Kile ni kiwanja chao wanalipa kodi za ardhi na wana leseni nacho ni mali yao wana haki zote ikiwemo nguvu ya kuamua nani apite hapo na nani asipite

Kama unadhani ni haki yako kupita hapo kwenye kiwanja cha watu nenda mahakamani
 
Habari kwenu Wadau!

Sheli ya Total ambayo ipo eneo la Mlimani City imekuwa na utaratibu wa hovyo wa kuwanyanyasa Watembea kwa Miguu kwa muda mrefu!

Utaratibu huo umeanza tangu kipindi cha sherehe za Christmas mpaka leo hii! Ukiwa unatembea kwa Miguu, unaendesha baiskeli au ukiwa Mazoezini hauruhusiwi kupita kwenye eneo la Sheli hiyo!

Wapo Walinzi wa Kampuni (nitaweka Jina soon) wenye Silaha ambao wamejipanga pande zote za Sheli kuzuia watembea kwa Miguu! Utaratibu huo haukuwepo miaka yote! Iweje leo unakuja utaratibu wa ovyo kiasi hiki?

Utaratibu huo wa hovyo umepelekea watu kutengeneza njia mbadala ya kuzunguka Sheli kitendo ambao kimeendeleea kuharibu Mazingira kwa Wananchi kujitengenezea njia zao wenyewe!

Tunataka kujuzwa kama utaratibu huu ni mpya kwa Sheli za Mkoa wa Dar es Salaam na kwingineko Nchini au ni Ubabe wa wenyefedha? Itakumbukwa Sheli hii bado ipo kwenye hifadhi ya Barabara na hivyo kuzuia Service Road inayotokea Mlimani City kuja roundabout ya kuelekea kwa Mama Kamche to Calabash! Kitendo cha kuzuia muendelezo wa service road ndio maana watu wamekuwa wakipita chini ya Paa la Sheli hiyo!

Lakini kwenye Sheli kuna huduma za Kibenki, Supermarket na Biashara ya Vilainishi vya Magari nk.

Tunaomba Mamlaka zinazohusika, ikiwemo Ofisi ya RC Kunenge kuingilia kati unyanyasaji na uzalilishaji unaoendelea kwenye Sheli ya Total pale Mlimani City!

Goodluck Mshana
Sheli ni kampuni tofauti na total tafadhali.
 
Hivi huwezi kuvuta sigara, kupiga simu ndani ya gari? Sheli hiyo ina miaka si chini ya 20 sasa! Hakuna matukio ya namna hiyo! Kwanza Watanzania wamestaarabika sana siku hizi! Zamani sio ajabu kukuta mtu amewasha sigara ndani ya Ngorika au Feri!

Eneo hilo limetumika kama njia kwa miaka nenda rudi! Japo ni vizuri kuchukua tahadhari kwa kuendelea kutoa Elimu kwa Umma! Sio kuzuia Watembea kwa Miguu! Otherwise wakubali eneo la Sheli likatwe kuruhusu service road inayotokea Mawasiliano ipite ili tuwaachie Sheli yao na huduma zao zote!
Kwa hiyo mkuu unamaanisha ukifika hapo usawa wa sheli hakuna service road na unalazimika uvuke barabara upande wa pili ili kuendelea na safari yako?
 
Barabara mbona ipo piteni huko huwexi komaa kupita kiwanja cha nyumba ya mtu au kiwanja cha sheli ya mtu

Kile ni kiwanja chao wanalipa kodi za ardhi na wana leseni nacho ni mali yao wana haki zote ikiwemo nguvu ya kuamua nani apite hapo na nani asipite

Kama unadhani ni haki yako kupita hapo kwenye kiwanja cha watu nenda mahakamani
Hapo kuna huduma nyingine zaidi ya kujaza mafuta kuna supermaket ATM sasa unapozuia watu wa miguu kupita bila kuwaambia sababu za msingi si unaona ni uonevu wa waziwazi
 
Niliwahi kuwahoji sababu ya kuzuia watembea kwa miguu kupita na kupata huduma zilizomo ndani ya kituo au kupita njia; wakasema ni sababu za kiusalama. Nilivyowadadisi wakasema mwekezaji aliyepanga supermarket hapo alikuwa halipi kodi na kuhama alikuwa hataki, yaani ni mbabe na mwenye vitisho. Sasa walipotumia nguvu kumtoa yule mpangaji alitishia atakuja kufanya kitu hicho kituo kitajutia. Sasa tangu hapo jamaa wanaishi kwa tahadhali asije akawatuma watembea kwa miguu wakafanya uharifu. Wa gari wanawaamini kwa kuwa magari yamesajiriwa hivyo pakifanyika tukio ni rahisi kutrace....
 
Unachoongea ni sahihi, lakini jiulize hiyo sheli inakosa gani? Yenyewe imepewa eneo la biashara na inalipa Kodi, mi nadhani ungefuatwa utaratibu mwingine ili barabara ipatikane. Mwenye sheli anayo haki na eneo lake la biashara.
Labda wahusika wataona huu uzi watashughulikia barabara ipatikane.
Kumlaumu mwenye sheli sio sahihi
Kapewa na nani? Eneo la service road, hapo kaingia ,hiyo ni barabara kongwe.
 
Haki bila wajibu ni ukichaa. Sheli haitembelewi na chombo au mtu anayetaka kununua mafuta. Wewe unafukuza upepo (baadala ya kuweka treadmill nyumbani), unawaghasi wanaofanya biashara!

Jifunze kuheshimu ofisi za wenzako ili wakuheshimu. Aidha acha kwenda pahala huhusiki napo. Hata gari kukatiza pale bila kununua mafuta ni kosa.

Heri ya mwaka mpya
Mbona una hasira kwanza wako njiani wao waondoke hapo wapishe barabara Mana kituo Kiko kwenye service road.
 
Ila jamani vitu vingine ni kujitaftia mengine sasa we unakatiza sheli kweli? kumbuka hayo maeneo ni hatari we unakatiza kufanya njia zako bythen mi naona ni halali wao kudhibiti movements zisizo za lazima kama izo za kukatiza katiza hovyo (nasema ivi mi mwenyewe ni mkatizaji mzuri sana wa ilo eneo).

Kudhibiti movements izo zitasaidia maana kuna watu wengine hawajui athari za kukatiza sheli hovyo na kuna wengine wanaweza pita na sigara zao, au vitu hatari kiasi cha kuhatarisha usalama wa eneo lao la kazi.

Imagine apite mtu apo alafu litokee jambo labda ni mlipuko au chochote kibaya waje waseme ulisababishwa na mpita njia kukatiza sheli we unafikiri kosa litakua la nani?

Huduma za kibenki zipo ila sio lazima ukatize sheli vile vile kuna sehemu kwa upande wa pili kuelekea Ardhi mtu anaweza pita kule na kutokea kule kule.

Ova.
Hujui nature ya hicho kituo Kiko kwenye service road na njia ya kuingilia mlimani city na kwenda mbele ka KWA kakobe kwahyo watumia miguu wapite hewani, au kwenye barabara ya magari, maana wakifanya hvo Raia na mtu anayefata bank au kuingia mlimani city kwa juu hawezi kupita
 
Back
Top Bottom