Kituo cha Mafuta cha TOTAL Mlimani City na unyanyasaji/udhalilishaji kwa wananchi

Walipojenga zile nyasi zao waruhusu wapita miguu aisee
Kuna ofisi pia mjini nyingine za serikali,zile pedestrian walkway wamezungushia minyororo matokeo yake watu wanapita barabarani.
 
Kuna ofisi pia mjini nyingine za serikali,zile pedestrian walkway wamezungushia minyororo matokeo yake watu wanapita barabarani.
Na hapo mtu kupita njiani ni kutafta kugongwa, yapasa town planner's waweke consideration ya mahitaji ya wote kutumia barabara, bila hivo kutesana tu sasa
 
Kwenye nchi za watu walioelimika na wanaojua haki zao mwekezaji hawezi kufanya huo upumbavu,raia wanamtia hasara ndani ya nusu saa tu.
Huku Bongo watu wamezubaa sana,ishu kama hiyo kwa nchi za wenzetu inashughulikiwa na raia wanne tu bila ya kushitaki mahali popote.
Huyo mwezekaji kasikitisha mbona tumepita miaka na miaka nothing happened there why nowdays.
 
sawa siku moja nitakutembelea huko halafu unioneshe hiyo sehemu iliyozibwa halafu tutajua cha kufanya
Yes huwa nayatumia Sana hayo maeneo hasa evening work au kwenda kula pronze na pweza tamu maeneo ya mlimani city upande wa ddc sasa kuzuia naona ni ukatili mkubwa Sana aisee
 
cariha my dear...nikushukuru mnoo pamoja na Wadau wengine kuniasaidia kupaza sauti juu ya unyanyasaji unaoendelea pale Total! Ni wajibu kwa wenye Mamlaka kulitafutia ufumbuzi swala hili mapema iwezekanavyo!
 
Ile ni property ya mtu na ana haki kamili nayo
Pale kuna biashara tena sensitive.
Kwanza nilishangaa kwa nini watu wanapita tu pale kama njia!? Nasema wana haki ya kuzuia kupita tena waweke trespass tapes kabisa yaingie magari tuuu.
 
Habari kwenu Wadau!

Sheli ya Total ambayo ipo eneo la Mlimani City imekuwa na utaratibu wa hovyo wa kuwanyanyasa Watembea kwa Miguu kwa muda mrefu!

Utaratibu huo umeanza tangu kipindi cha sherehe za Christmas mpaka leo hii! Ukiwa unatembea kwa Miguu, unaendesha baiskeli au ukiwa Mazoezini hauruhusiwi kupita kwenye eneo la Sheli hiyo!

Wapo Walinzi wa Kampuni (nitaweka Jina soon) wenye Silaha ambao wamejipanga pande zote za Sheli kuzuia watembea kwa Miguu! Utaratibu huo haukuwepo miaka yote! Iweje leo unakuja utaratibu wa ovyo kiasi hiki?

Utaratibu huo wa hovyo umepelekea watu kutengeneza njia mbadala ya kuzunguka Sheli kitendo ambao kimeendeleea kuharibu Mazingira kwa Wananchi kujitengenezea njia zao wenyewe!

Tunataka kujuzwa kama utaratibu huu ni mpya kwa Sheli za Mkoa wa Dar es Salaam na kwingineko Nchini au ni Ubabe wa wenyefedha? Itakumbukwa Sheli hii bado ipo kwenye hifadhi ya Barabara na hivyo kuzuia Service Road inayotokea Mlimani City kuja roundabout ya kuelekea kwa Mama Kamche to Calabash! Kitendo cha kuzuia muendelezo wa service road ndio maana watu wamekuwa wakipita chini ya Paa la Sheli hiyo!

Lakini kwenye Sheli kuna huduma za Kibenki, Supermarket na Biashara ya Vilainishi vya Magari nk.

Tunaomba Mamlaka zinazohusika, ikiwemo Ofisi ya RC Kunenge kuingilia kati unyanyasaji na uzalilishaji unaoendelea kwenye Sheli ya Total pale Mlimani City!

Goodluck Mshana
Acha uongo hapo kuna supermarket na ATM na wapita miguu wanaopita hapo wapo kibao,kama unafanya jogging pita pembeni.
 
Mkuu umechanganya sana madesa,Shell na Total ni Company mbili tofauti kabisa! Ukisema Shell ni Kampuni,Ukisema Total pia ni Kampuni,sasa hapa sema unazungumzia Kampuni ipi???
Umeeleweka ndugu but issue hapa sio shell au filling station issue ni kuwazuia watu kupita kwa miguu eneo hilo bila taarifa wakati walishazoea kupita hilo eneo miaka nenda rudi
 
Na hapo mtu kupita njiani ni kutafta kugongwa, yapasa town planner's waweke consideration ya mahitaji ya wote kutumia barabara, bila hivo kutesana tu sasa
Kuna maeneo waenda kwa miguu marufuku kuishi kinachowapeleka huko nini? Kama sio uchokozi ni nini?
 
Imagine unaenda calabash au kwa mama kamche mpaka uzunguke mbali huko loh.
Anyway Wenzetu wa Sinza mnaofanya Jogging eneo hilo, jichangeni mpate pessa kama Laki 2, iteni waandishi matata sana wawili wa TV na Wale mattata wawili wa Redio wapigeni posho wamulike hiyo kadhia kwenye media zao. Hakika hiyo Shell itaenda na Maji kwa jinsi Mhe.Rais wetu anavyopenda Wananchi Wanyonge.
Mission accompolished!
 
Anyway Wenzetu wa Sinza mnaofanya Jogging eneo hilo, jichangeni mpate pessa kama Laki 2, iteni waandishi matata sana wawili wa TV na Wale mattata wawili wa Redio wapigeni posho wamulike hiyo kadhia kwenye media zao. Hakika hiyo Shell itaenda na Maji kwa jinsi Mhe.Rais wetu anavyopenda Wananchi Wanyonge.
Mission accompolished!
Acha tunateseka bure tu kwanza hilo eneo ni hifadhi ya barabara why ui block kwa wapita miguu, Ina maana hawana haki, ningekuwa na mamlaka ningeamuru ivunjwe tu, sasa na pale Kuna ATMs plus supermarket za nini sasa.
 
Yaani haiingii akilini eti unaruhusu watu wenye magari wanapaki maeneo yale yale wanajaza mafuta ila kupita kwa miguu eti ni hatari nadhani CRDB na Absa na NBC kama sikosei wanazo ATM zao hapo wanapozuia watu wasipite waingilie kati kuna mtu anawahujumu na hana taarifa za msingi. Juzi nusra nilianzishe na masecurity coz haina mantiki me sijui nani anahusika wapi na nini nachojua hapo sehemu kuna huduma za kifedha na fuel filling
 
Back
Top Bottom