Kituo cha kuuza mafuta cha bei nafuu ni bei gani?

Gloriamagret

Member
Jun 12, 2023
47
155
Nimekwenda sehemu za mkoa wa pwani bush kabisa nimekuta vijana wa bodaboda wananunua petroli ya.kulima kwa chupa.

Nomeshawishika niwajengee angalau kituo simple cha petrol.

Swali kituo simple kinagarimu kiasi gani? Pampu mojanya disel na petrol, vipi bei ya leseni, vibali nk.

Nina kiwanja eneo hilo barabarani na kina kibanda chenye umeme.tupeane maarifa
 
Nimekwenda sehemu za mkoa wa pwani bush kabisa nimekuta vijana wa bodaboda wananunua petroli ya.kulima kwa chupa.
Nomeshawishika niwajengee angalau kituo simple cha petrol.
Swali kituo simple kinagarimu kiasi gani.pampu mojanya disel na petrol.vipi bei ya leseni.vibali nk.
Nina kiwanja eneo hilo barabarani na kina kibanda chenye umeme.tupeane maarifa
Kijijini mkuu?. Naomba nikudm
 
Nadhani ufungue filing statio(kituo kidogo Cha kujazia mafuta) japo najua itacost chini kidogo tu ya hizo Petro station
 
Nenda EWURA ndo wanasimamia hayo mambo.

Wako jengo la PSSSF (br. ya Sam Nujoma njiapanda ya kwenda Sinza Makaburini) sakafu ya 4.

Ukifika pale ulizia kitengo cha mafuta halafu ukimpata afisa wa kitengo hicho mwambie unaomba kuongea naye baada ya mida ya kazi.

Ukiongea naye kikubwa utapata madesa yaliyokamilika ya pepa unalotaka kusovu.
 

TANGAZO LA FURSA YA MKOPO NAFUU - UJENZI NA UENDESHAJI WA VITUO VIDOGO VYA MAFUTA MAENEO YA VIJIJINI​



Serikali kupitia Wakala wa Nishati Vijijini (REA) imedhamiria kuanzisha mpango wa kuwezesha ujenzi wa vituo vipya vidogo vya mafuta (petroli na dizeli) vya gharama nafuu maeneo ya vijijini ili kuondoa madhara yatokanayo na njia zisizo salama.
Wakala unakaribisha waomabaji wenye vigezo kuomba mkopo ili kuwezesha ujenzi na uendeshaji wa vituo vipya vidogo vya gharama nafuu maeneo ya vijijini. Fomu ya Maombi pamoja na Mwongozo wa Maombi ya Mkopo vimeambatanishwa kwenye tangazo hili kwenye tovuti ya Wakala.
Maombi yote yawasilishwe kupitia barua pepe: vituovyamafuta@rea.go.tz na pia kupitia anuani ifuatayo:
Mkurugenzi Mkuu
Wakala wa Nishati Vijijini – REA
Jengo la PSSSF, Ghorofa ya 7
Barabara ya Makole
S. L. P 2153
Dodoma, Tanzania.
Juu ya bahasha baada ya anuani ya Wakala iandikwe ‘Maombi ya Mkopo kwa Ajili ya Ujenzi wa Vituo vya Mafuta Vijijini’

Mwisho wa kuwasilisha maombi ya mkopo ni tarehe 25/8/2023 saa tisa na nusu alasiri.
 
Back
Top Bottom