Kituo cha Discovery Channel kimebadilika kutoka Elimu hadi Burudani za kuhadaa

Kituo cha Discovery Channel kimebadilika kutoka Elimu hadi Burudani za kuhadaa

Damaso

JF-Expert Member
Joined
Jul 18, 2018
Posts
6,132
Reaction score
10,514
Kuna kipindi fulani, hasa miaka ya 1990 hadi mwanzoni mwa 2000, jina Discovery Channel lilikuwa alama ya heshima kwa yeyote aliyependa kujifunza kupitia runinga. Ilikuwa ni “chuo cha nyumbani,” chenye vipindi vya kuvutia juu ya sayansi, historia, teknolojia, safari na siri za ulimwengu ambazo hazikuwa rahisi kufikika kwa macho ya kawaida.
Waterstudio-news-discoverychannel1.png

Watazamaji walifurahia makala kama MythBusters, Future Weapons, Shark Week na How It’s Made – vipindi vilivyopanga akili na kuamsha shauku ya kujua zaidi.
0_UxBDcIM2GW1WSOUq.jpg

Lakini sasa, ukifungua kituo hicho, mara nyingi utakutana na maigizo ya “reality shows” yasiyo na kina, mada za njama zisizo na ushahidi, au maudhui ambayo hayana tofauti kubwa na maigizo ya kibiashara. Swali kubwa ni: nini hasa kilitokea kwa Discovery Channel?
B3-BH458_JohnHe_M_20180802000223.jpg

Mwanzilishi wa kituo hiki, John Hendricks, alikuwa na ndoto kubwa – kutoa nafasi ya kujifunza kupitia televisheni. Discovery Channel ilizaliwa kwa lengo la kuwapa watu maarifa ya kweli kwa njia ya kuvutia na ya burudani. Kwa muda mrefu ndoto hii ilifanikiwa, hususan barani Afrika ambako majukwaa ya Free to Air Satellite dish na huduma za mitaa kama Ghana Cable na Barmedas zilihakikisha kuwa familia nyingi ziliweza kufurahia elimu hiyo kwa gharama nafuu.
images (63).jpeg

Lakini kadri miaka ilivyozidi kusonga, tasnia ya televisheni ilianza kusukumwa zaidi na mtazamo wa kibiashara kuliko wa kielimu. Vipindi vilivyokuwa na taaluma nzito vilionekana havivutii matangazo ya kibiashara ikilinganishwa na maigizo ya “reality shows” yenye drama na mvuto wa haraka. Hapo ndipo muundo mzima wa Discovery Channel ulipogeuka.
expertcont.jpg

Mwishoni mwa miaka ya 2000, ushindani wa vituo vya burudani uliongezeka duniani kote. Watazamaji walipendelea vipindi vya haraka haraka, vya kuchochea hisia kuliko vya kukazia ubongo. Kwa lugha rahisi, soko lilitaka burudani, si elimu tena. Discovery Channel, ili isibaki nyuma, ikaingia katika mtego wa kibiashara.
MV5BMTU5OTAxNDkwNl5BMl5BanBnXkFtZTgwNjc3MzIzMjE@._V1_.jpg

Hatimaye vipindi vya kuelimisha vilianza kupotea taratibu. Badala yake tulianza kuona “reality shows” za wachimbaji dhahabu, wawindaji wa samaki wakubwa, au wasafiri wanaoishi porini kwa mazoea ya kiajabu. Bila shaka vipindi hivi vina hadhira, lakini swali ni je, vinaelimisha kwa kiwango kilekile cha Cosmos au Planet Earth?
Discovery-Shows.jpg

Mwandishi mmoja aliwahi kusema: “Unapobadilisha elimu kuwa biashara katika jamii yenye ujinga mwingi, elimu hubadilika kuwa mzaha.” Kauli hii inaakisi hatima ya Discovery Channel. Badala ya kuendeleza hadhi yake kama chombo cha maarifa, kituo hicho kimekubali “kuburudishwa na ujinga,” kikiendeleza maudhui mepesi ambayo mara nyingine yanapotosha.
masters_of_disaster_group_copy.jpg

Kwa watazamaji wa Afrika Mashariki na Kati, hususan Tanzania, kumbukumbu za siku hizo za Barmedas au Ghana Cable bado ni tamu. Familia ziliketi sebuleni, wakijifunza kwa pamoja juu ya anga za juu, historia ya Misri ya kale, au sayansi ya teknolojia mpya. Ilikuwa ni shule isiyo na ada.MythBusters, How It’s Made, Beyond 2000 / Beyond Tomorrow, Extreme Engineering, NextWorld hivi vilikuwa ni vipindi bora sana kutoka Discovery Channel.
images (64).jpeg

Hapo haujatazama vipindi maridadi kama vile*Paleoworld, Ancient Egyptians / Egypt Week, Unsolved History, Walking with Prehistoric Beasts, Discovery Sunday / Discovery Specials*, midanya jioni baada ya taarifa ya habari unakutana na NASA’s Greatest Missions, Cosmic Collisions, The Universe. Mars: The Quest for Life vipindi ambavyo ulikuwa unajifunza kwa makini sana.
maxresdefault.jpg

Leo hii, bado Discovery Channel inabeba jina kubwa, lakini heshima yake imepungua. Hata hivyo, inabakia kama ishara muhimu ya jinsi vyombo vya habari vinavyoweza kubadilishwa na nguvu za soko. Ndoto ya John Hendricks haijafa kabisa – kwa sababu vipindi vya elimu bado vinapatikana, lakini mara nyingi vinapewa nafasi ndogo au vinahamishiwa kwenye vituo tanzu kama Discovery Science au Animal Planet.
images (66).jpeg

Swali la msingi ni kama kizazi kipya kitaweza kufurahia thamani ile ile tuliyoiona sisi wa mwanzoni mwa 2000s. Au labda huu ndio mwisho wa enzi ya televisheni ya kielimu, na mwanzo wa enzi ya burudani inayojificha chini ya kivuli cha “maarifa.”
 
Ni mambo ya kawaida tu katika biashara. Ni lazima uendane na wakati au uwe obsolete! Ni Gen Z gani atakaa kuangalia kipindi cha kuelimisha sijui Ancient Egypt wakati ChatGPT inaweza kumpa jibu ndani ya sekunde nne? Hali hii haikuishia kwenye TV tu bali hata magazeti, radio na kwingineko. Kabla ya Shigongo kuingia na ujinga wake wa magazeti ya udaku, magazeti yalikuwa tofauti sana. Makala zilizoshiba. Uandishi makini (Mwanahalisi, Rai, Raia Mwema)...leo hii ni udaku tupu, uchawa na michezo basi. Ndicho watu wanataka. Hata hapa JF unafikiri ni sawa na zamani?

Ni mambo ya kawaida tu. Ni kila zama na kitabu chake!
 
Ni mambo ya kawaida tu katika biashara. Ni lazima uendane na wakati au uwe obsolete! Ni Gen Z gani atakaa kuangalia kipindi cha kuelimisha sijui Ancient Egypt wakati ChatGPT inaweza kumpa jibu ndani ya sekunde nne? Hali hii haikuishia kwenye TV tu bali hata magazeti, radio na kwingineko. Kabla ya Shigongo kuingia na ujinga wake wa magazeti ya udaku, magazeti yalikuwa tofauti sana. Makala zilizoshiba. Uandishi makini...leo hii ni udaku tupu, uchawa na michezo basi. Ndicho watu wanataka. Hata hapa JF unafikiri ni sawa na zamani?

Ni mambo ya kawaida katika jamii!
Well said mkuu!
 
Kila zama na zama zake
Tatizo sio zama mkuu ila mpaka umesikia wameanzisha Discovery+ na Animal+ ujue watu wenye mapenzi ya kufuatilia hizi mambo ni wale Old school! Hawa watoto Gen Z umkalishe chini atazame Food Factory halafu baadaye atazame Roll with Grizzly Bears? Ni changamoto
 
Back
Top Bottom