Mi kwangu huu si ushamba aisee, naona hii inaweza kumtokea karibu kila mtu!
dah.... kuna hivi vioo ambavyo vinachukua nafasi ya milango ya mbao, vile vioo vigumuuuu!
Basi bwana, lile likioo lilikuwa limesafishwa vizuri haswaaa!! linang'aa effectively!
Kuna wakati ilikuwa ukiangalia kwenye kioo pale unaona kama vile hamna kioo! kumbe wapi!...
Haya! mi na ugeni wangu, nikakurupushwa kutoka recreation centre na kuambiwa kuwa muda wa kazi ushafika!! unacheza pool mpaka saa hizi?
kusikia hivyo, wacha nikimbie kuokoa kibarua! lahaulaaaa! mtoto wa watu nikaruka na kuparamia kioo kile nikidhani ni empty space ambayo naweza kupita!!!!!
dah! mpaka leo nikikumbuka ile hali, inabidi nicheke, kiukweli niliumia sana paji la uso pamoja na baadhi ya viungo vya mwili!
enzi hizo ndo kwaanza naanza na kukutana na automatic doors! kabla hujafika tu, usha-sense na kufunguka wenyewe! hm! ushamba mzigo..!
ni hayo tu!