Kituko cha mchana wa leo

Kituko cha mchana wa leo

naamini weekend inaenda poa.

Leo nikiwa katika hoteli fulani nikikutana na rafiki yangu katika mambo ya kazi,mimi nilitangulia kufika hotelini hapo kisha akafuata rafiki yangu aliyekuja na gari yake,tukazungumza mambo yetu wakati anataka kuondoka akatokea mwanamke mmoja akiyemuuliza rafiki yangu anaenda wapi? Jamaa yangu akamjibu kuwa analelekea ngaramtoni,yule mwanamke akakurupuka mbio na kushuka toka kwenye balcony ya hoteli hiyo na kumuacha mpenzi wake waliye kuwa wameketi wote wakipunga upepo.

Rafiki yangu alimsubiri ashuke na kuondoka naye,sasa najiuliza yule mwanamke kashobokea gari au ni kitu gani?
Nina uhakika wa asilimia zote kuwa hawajuani na rafiki yangu,maana naye alishangaa kuona mtu akiomba lifti kwa nguvu.

Hivi inakuwa wanawake wengi kuwa udhaifu kwenye magari??

Mchana mwema.!

hahahahahaa mbuyi, jaribu kumtafuta kwenye cm tena muda huu usikute huyu jambaz wa kike kisha fanya yake.
 
Haya tukuulize rafiki yako ana gari gani hilo la kushobokewa?
White-2014-Range-Rover-Sport.jpg
 
Back
Top Bottom