Mshana Jr
Platinum Member
- Aug 19, 2012
- 371,343
- 859,922
Bado binadamu si mkamilifu na mjuzi wa yote pamoja na ugunduzi na uvumbuzi kwenye nyanja za sayansi, teknolojia na ushirikina.
Kupitia nyanja hizi Dunia imekuwa kama Kijiji na magumu mengi yasiyowezekana yamewezekana
maendeleo ya kuweza kurusha chombo chenye uzito wa tani za kutosha na kikaruka mpaka anga tupu huko mbali kabisa na kuweza kuwasiliana nacho si jambo dogo hata kidogo.
Lakini vipi mwanga anaweza kuingia nyumbani mwako bila kuvunja hata kitasa na akafanya yake na kusepa bila wewe kujua?
Pamoja na yote hayo kuna hili dogo sana limeshindikana kabisa na siku hili likiwezekana. Dunia katika ulimwengu huu itakuwa kitu kingine kabisa, jambo hilo ni kurudisha wakati nyuma walau kwa Sekunde Moja Tu
Kwamba umeshafyatua risasi kwenye Bastola kisha ghafla ukaghairi! Uwezo wa kuirudisha nyuma risasi hatuna
Kwamba tumeshatamka neno lakini ghafla tukijua madhara yake tukataka kulirudisha mdomoni uwezo huo hatuna.
Mifano ni mingi ambayo matendo yake tungeweza kuyaghairi sekunde moja tu baada ya kutenda dunia hii tuliyonayo isingekuwa hivi ilivyo leo hii na saa hii
Just imagine ni kitendo cha sekunde moja tuu kizungu wanasema blink of an eye hubadilisha historia ya kila kitu sekunde ni kubwa sana. Ni kubwa kuliko saa moja yenye dakika 60.
Kwa uamuzi wowote unaotaka kuchukua katika zile sekunde za majeruhi. Tafakari tena na tena kabla hujaamua kutenda kwakuwa sekunde moja itakayofuata baada ya kitendo inatosha kubadili maisha yako milele
Kama uamuzi huo si wa kuumiza wala kuharibu basi una kheri milele lakini kama ni kinyume chake sekunde ile ya mwisho ndio imebeba furaha ama majuto yako mpaka kifo
Muda hauna kinyume hata kwa sekunde moja na muda huwa hausubiri mtu. Ukitenda tenda kwa tafakuri na ukiamua amua kwa hekima! Majuto yasijekuwa mjukuu
Vinyonga wote hawana Mama kwakuwa ili wazaliwe inabidi mama afe!