Kitu kisichoruhusiwa kwa wenye umri wa chini ya miaka 18

Trainee

JF-Expert Member
Sep 22, 2018
2,219
2,824
Habari

Naona wanajitahidi kuweka katazo kwa wenye umri wa chini ya miaka 18 kwenye matangazo ya michezo ya kamari na matangazo ya pombe

Hata hivyo unaposhika rasmi vitu hivyo kwajili ya kuvitumia hutakutana na onyo wala katazo lolote kwa mtu yeyote

Nimpongeze Azam kwa kuweka kibandiko chenye onyo zuri kwa mtumiaji wa energy yake japokuwa kinywaji hicho bado wanywaji wanaongezeka kila siku kwa kila rika kila jinsi na kila umri.

Napendekeza kuwepo na onyo/tahadhari kali kwa kila kisichokuwa ruksa kwa wenye umri chini ya miaka 18.

Mfano pombe zote ziwe na kibandiko cha wazi kabisa tena kiambatane na maandishi (ya Kiswahili ikiwezekana) ya kwamba ni marufuku kwa wenye umri chini ya miaka 18 kama vile tulivyozoea kuona kwenye muvi za kimarekani zamani wanaandika na namba 18 iliyozungushiwa inaonekana pale

Kwa michezo ya kamari nayo kuwe na onyo pindi mtu anapokuwa ameingia kwenye mchezo husika isiishie kwenye matangazo tu

Mwisho kwa sisi raia, nasi tupende kufuatilia vitu kabla ya kutumia maana tuna kawaida ya kulilia haki kisha tukitekelezewa hatuna mpango tunapuuza kuitumia.

Mfano mzuri ni hiyo energy ya azam sidhani kama kuna anayefuatiliaga kilichoandikwa mule!

Ikumbukwe kuwa kinachopigwa marufuku kwa walio chini ya miaka 18 (watoto) kwa lugha nyepesi zaidi tunaweza kusema kitu hicho ni dhambi kwahiyo kwenye makatazo yenu msiogope kuitumia kauli hiyo wakati mwingine itasaidia zaidi kuwanusuru watoto wetu

Nawasulisha
 
Back
Top Bottom