Mkuu Smartphones zinatofautiana mambo mengi si kidogo. Na hayo mambo mengi ndio yanasababisha kuwepo na bei tofauti kati ya simu na simu.
Ila mimi naona vinavoleta utofauti ni:
-Durability. Kuna baadhi ya simu ni more durable kwaasababu materials yaliyotumika kuitengeneza ni ya kiwango cha juu. Utakuta simu ata ukiidondosha ikatulia kioo cha mbele, haipasuki just inaweka scratches au cracks kidogo. Mfano hai ni simu zenye Gorilla Glass technology kama Samsung Galaxy S series.
Material pia yaliyo tumika katika cover la simu (ata kama ni plastick au la bati) ni imara sana. Yanaisaidia simu kuimili mikiki mikiki ya dunuani.
-Unique features. Kuna baadhi ya smartphones zinakua na unique features ambazo wengine (makampuni mengine) hayana. Mfano: Wireless charging (Nokia Lumia), Water and Dust resistant (Xperia), Unique OS ya Apple, iOS (iPhones),etc. Hizi features hayo makampuni yanakua yamewekeza sana katika ku-innovate. Hivyo lazima wajidaie.
-Advanced features. Pia smartphones zinatofautiana features kama processor kubwa na nzuri, RAM kubwa, Screen kubwa na kiwango cha juu, internal memory kubwa etc. Namaanisha nini, utakuta simu mfano zote zina RAM ya 1.5GHz na zote ni Dual Core. Lakini, hizo hizo RAM zinatofautiana, nyingine ni more quality na nyingine less. Kwahiyo wewe kama mteja, usipagawe tu na kuangalia ukubwa wa RAM, angalia aina ya hiyo chip pia. Au pia katika screen, utakuta kuna za aina nyingi, kama AMOLED, TFT, LCD, Retina Display etc. zote hizo zina quality tofauti.
Mtazamo wangu hapo tu nimekwama.