Kitu gani kinakupa kiu ya Katiba Mpya?

mr yamoto

JF-Expert Member
Oct 2, 2016
923
1,393
Tangu tupate Uhuru Desemba 9, 1961 hadi sasa, Tanzania imepata kuwa na Katiba mpya tano ambazo katika uhai wake zimeweza kufanyiwa marekebisho mara kwa mara kwa kuzingatia mazingira ya kisiasa, kijamii na kiuchumi ya nchi.

Ofisi ya ukaguzi wa mahesabu ya Serikali imekua ikimbana na changamoto ya kuingiliwa na mhimili mwingine na kulazimisha matakwa yao, uimara na msimamo wa CAG ndio unafanya ripoti isibadilishe

Katiba mpya inahitaji kuipa nguvu ofisi hii ichukue maamuzi.

Moja ya kauli Askofu Severin Niwemugizi alisema 27/Sept/2017 ni “yuko tayari kuitwa mchochezi endapo juhudi za kudai nyaraka hiyi zitatafisiriwa tofauti” hii ilinifikirisha sana, lakini kama Katiba Yetu lazima tukubali mawazo tofauti hata kwa ambayo hatutaki kusikia.

Lakini pia aliyekuwa waziri ndugu Lazaro Nyalandu aliwahi kusema “kwa sasa nchi inachokihitaji ni katiba mpya” sitaki kusema mawazo yake ni bora sana lakini ni bora kwa hali ya sasa Katiba Yetu sote kwa manufaa yetu wote, tukubali mabadiliko!

Kitu gani kinakupa kiu ya Katiba Mpya?

Mimi Uhuru wa mihimili ya Mahakama na Bunge.

Mr yamoto
 
katiba ya sasa ibara ya 3 kifungu cha kwanza inasema “Jamhuri ya Muungano ni nchi ya kidemokrasia na ya kijamaa, yenye kufuata mfumo wa vyama vingi vya siasa”

Kwa sasa nchi yetu inafata mfumo wa soko huru, kwa hiyo ni vema hilo neno kijamaa liondolewe

Ujue sisi tumapenda sana kujidanganya.
Hivi sisi tupo kwenye Ujamaa???
Nchi ya Ujamaa viongozi wake kwenye mishahara hukatwa KODI.
UJAMAA NI USAWA.
 
Wanasiasa Ndio Wenye Ushawishi Mkubwa Kwenye Masuala Ya Katiba Kwa Wananchi.

Lakini Inasikitisha Wanasiasa Wao Ndio Watu Wa Kwanza Kuharibu Mchakato Huu Sababu Ya Maslahi Ya Vyama Vyao, Kama Tunataka Mabadiliko Yoyote Yale Katika Nchi Katiba Mpya Lazima
 
"Katiba hii, hairuhusu kufungua kesi mahakamani kuhusu jambo lolote alilolitenda au alilokosa kulitenda yeye binafsi kama raia wa kawaida ama kabla au baada ya kushika madaraka ya Rais.”
Hii ni moja ya sababu nataka katiba, yani raisi akipiga dili hashtakiwi
 
Pengine Viongozi Wataona Umuhimu Wa Elimu Kwa Wananchi Wote Hasa Masikini Ikiwa Na Wao Watapeleka Watoto Wao Katika Shule Ambazo Masikini Walipa Kodi Wanapeleka Watoto Wao.

Ikiwa Katiba Mpya Itaweka Hili Kwamba kila Kiongozi Mtoto Wake Asome Kwenye Shule Za Umma
 
Heshima Zote Ziende Kwa JK Kuona Na Kusikia Kelele Za Watu Binafsi, Taasisi Zisizokua Za Kiserikali Pamoja Na Baadhi Ya Wanasiasa Kupiga Kelele Kuhusu Katiba Mpya.

lawama Zote Ziende Kwa Watu Hasa Wanasiasa Wote Waliokwamisha Mchakato Ule Kwa Maslahi Yao Binafs.
 
Mistake Kubwa Ambayo Imewahi Kufanyika 1992 Kipindi Mfumo Wa Vyama Vingi Tanzania Unaanzishwa.

Pale Ambapo Viongozi Wa Vyama Vya Siasa Hasa Upinzani Hawakukaa Pamoja Na Kuangalia Mapungufu Ya Katiba Ambayo Iliundwa Mwaka 1977 Ambayo Kimsingi Inakibeba Chama Kimoja.
 
Kama utafanyika utafiti wa siri kuwahoji waliokuwa wabunge wa bunge la katiba walioikataa Katiba ya warioba,hivi sasa watasema wanaitaka Katiba hiyo.unajua kwa nini?hivi sasa akili zao zitakuwa zimekaa sawa.hata kule msoga
 
Kwanini mkuu?

Mijadala kama hii ishaletwa na watu huchangia sana... ila hakuna badiliko zozote zile zaidi ya kuchorana...

Cc: mahondaw
 
Kama utafanyika utafiti wa siri kuwahoji waliokuwa wabunge wa bunge la katiba walioikataa Katiba ya warioba,hivi sasa watasema wanaitaka Katiba hiyo.unajua kwa nini?hivi sasa akili zao zitakuwa zimekaa sawa.hata kule msoga
Ni kweli ndugu nimeshuhudia hilo
 
1 Uhuru wa mahakama - Jaji mkuu na wenzake wasiteuluwe na raisi, nafasi iombwe kama ilivyo Kenya. 2.Matokeo ya urais yapingwe mahakamani. 3.Tume ya uchaguzi isichaguliwe na rais kuwe na utaratibu maalumu na mwenyekiti wake awe anapatikana kwa nafasi kutangazwa. 4.Futa kabisa ofisi nzima ya DC, kazi zote zifanywe na DED na baraza la madiwani. 5.Spika wa bunge asiwe mwasiasa wa chama chochote na nafasi yake na ya katibu wa bunge itangazwe wenye sifa waombe. 6.Viti maalumu viwe na ukomo wa miaka 5 tuu. 7.Rais ashitakiwe pale itakapobainika kavunja katiba au sheria za nchi. Isisubiri muda wake uishe. 8.Linapitokea jambo kubwa au tukio la kupotea au kuuawa raia na ndani ya muda maalum polisi wakashindwa kutoa majibu iundwe tume kuchunguza ikiwemo kutumia vyombo vya nje. 9.Iwe lazima bunge lunapoazimia jambo serikali itekeleze, tena ndani ya muda husika, vinginevyo waziri husika ashitakiwe...
 
Du! Kiongozi hii ni Africa,hizo katiba unazotaka nenda ulaya utazipata ila sisi huku Africa mtuache na katiba yetu hii hii ya kuunga unga maana yasije yakatukuta ya Libya.bora tule ugali na chumvi ila Amani yetu ipo kuliko kula nyamachoma vitani
1 Uhuru wa mahakama - Jaji mkuu na wenzake wasiteuluwe na raisi, nafasi iombwe kama ilivyo Kenya. 2.Matokeo ya urais yapingwe mahakamani. 3.Tume ya uchaguzi isichaguliwe na rais kuwe na utaratibu maalumu na mwenyekiti wake awe anapatikana kwa nafasi kutangazwa. 4.Futa kabisa ofisi nzima ya DC, kazi zote zifanywe na DED na baraza la madiwani. 5.Spika wa bunge asiwe mwasiasa wa chama chochote na nafasi yake na ya katibu wa bunge itangazwe wenye sifa waombe. 6.Viti maalumu viwe na ukomo wa miaka 5 tuu. 7.Rais ashitakiwe pale itakapobainika kavunja katiba au sheria za nchi. Isisubiri muda wake uishe. 8.Linapitokea jambo kubwa au tukio la kupotea au kuuawa raia na ndani ya muda maalum polisi wakashindwa kutoa majibu iundwe tume kuchunguza ikiwemo kutumia vyombo vya nje. 9.Iwe lazima bunge lunapoazimia jambo serikali itekeleze, tena ndani ya muda husika, vinginevyo waziri husika ashitakiwe...
 
MAPENDEKEZO YA KATIBA MPYA

1)RAISI AWE NA HAKI YA KUGOMBEA MIHULA 3

2)MUHULA MMOJA WA UWONGOZI UWE NI MIAKA 15

3) RAISI AWE NA MAMLAKA YA KUTEUWA WENYEKITI WA VYAMA VYA UPINZANI

4)MIFUMO YOTE YA KI BENKI INATAKIWA IMILIKIWE NA SERIKALI(MABENKI,SEHEMU ZA KUBADILISHA PESA,)

5)WAPINZANI WAWEZE KUTEULIWA KUWA MAWAZIRI

6)WAJUMBE,WENYEKITI WA MITAA,MADIWANI WAKE WAWAKILISHI WETU KATIKA UCHAGUZI MKUU.KUSIWEPO UCHAGUZI MKUU KWA WATANZANIA WOTE

7)MTANZANIA YOYOTE HARUSIWI KUMILIKI ACOUNT NNJE YA NCHI

UKITAKA KUNUNUA GARI AU KIWANJA NI LAZIMA UPATE KIBALI KUTOKA SERIKALINI

8)
 
UMESAHAU (1) RAIS ASIFE AU KUFARIKI
(2)UONGOZI DUNIANI MPAKA MBINGUNI
 
Back
Top Bottom