Kitu gani kinafanya wanawake kuitwa hivi?

dmkali

JF-Expert Member
Nov 17, 2014
11,543
22,050
Tangu zamani nimekuwa nikisikia majina haya yakimaanisha mwanamke;
1. Demu

2. Manzi

3. Mrupo

4. Dogo

5. Kimwana

6. usingizi

7. Farasi

8. Shori

9. Kahaba

10. Shangingi

11. Twiga

12. Na sasa CHURA
Je kitu gani kinasababisha wapewe majina haya, tatizo nini? Na je ni kweli wanawake wanayafurahia majina hayo?
 
Kwa ufahamu wangu,majina yanamhusisha mwanamke na mtoto yanaletwa na dhana kuwa wanahitaji kutendewa kwa upendo na kudekezwa. Hilo demu linatokana na neno la kiingereza DAME ambalo bila kujua wanawake wengi wanalichukia lkn lina maana nzuri tu ktk asili yake. Naomba kuwasilisha
 
Mkuu kama pesa vile ilivyo na majina mengi

Au wali....

Kila jina huambatana na fikra Fulani au dhana Fulani huenda ikawa mbaya au nzuri....

Ila hii ya chura duuuuuuuh......

Chura ndio Nini braza
 
Mengine mnajiita wenyewe wana wake so muulizeni snura aliwaza nn kuwafananisha na Chura??
 
Kwa ufahamu wangu,majina yanamhusisha mwanamke na mtoto yanaletwa na dhana kuwa wanahitaji kutendewa kwa upendo na kudekezwa. Hilo demu linatokana na neno la kiingereza DAME ambalo bila kujua wanawake wengi wanalichukia lkn lina maana nzuri tu ktk asili yake. Naomba kuwasilisha
Ooh sasa na hili la CHURA nalo mkuu? maana nimepita sehemu nikakuta jamaa anamtambulisha mwanamke wake kwa rafiki zake kwamba ..HUYU NDO CHURA WANGU...nimejiuliza sana, sasa hii ipoje
 
majina hayo yamejikita katika kushusha heshima na kudhalilisha utu Wa mwanamke..awe anatumia mwanamke mwenyewe ama mwanaume
 
Back
Top Bottom