Kitu ambacho serikali inapaswa kujua. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kitu ambacho serikali inapaswa kujua.

Discussion in 'Great Thinkers' started by Shayu, Aug 27, 2016.

 1. Shayu

  Shayu Platinum Member

  #1
  Aug 27, 2016
  Joined: May 24, 2011
  Messages: 506
  Likes Received: 720
  Trophy Points: 180
  Kitu kimoja ambacho ninajua na serikali inapaswa kujua ni kwamba umoja wa nchi haupaswi kuchezewa. Nguvu ya taifa lolote lile inategemea sana umoja wa watu wake na sio ukubwa wa jeshi au silaha walizonazo.

  Katika nchi ikitokea kundi fulani linakandamizwa na kundi jingine linapewa upendeleo adui anapata urahisi sana kuingia na kupokewa na hata kuonekana shujaa na kundi linaloamini linakandamizwa.

  Naonya viongozi wawe makini sana. Taifa hili ni muhimu kuendeshwa kwa usawa na haki na kwa mujibu wa sheria na katiba ya nchi.

  Kama tunatendeana wenyewe kwa wenyewe kwa haki na usawa, hakuna taifa litakalo tugusa. Ila kama tunajigawanya kwa misingi ya uchama na kwa misingi ya ubinafsi tuhesabu taifa hili kuharibika.

  Wanasiasa naomba muwe makini sana. Msije mkapeleka mamilioni ya raia wa nchi hii katika matatizo. Lazima mfikiri mamilioni ya raia wa nchi hii kabla ya kujifikiria nyinyi.
   
Loading...