Kitisho cha Dr. Slaa si zaidi ya Mrema - Kinana

Kitisho cha Dr. Slaa si zaidi ya Mrema - Kinana

MUSHI UDOM 08

Member
Joined
Apr 10, 2011
Posts
10
Reaction score
16
Nimesikitishwa sana na vijana wenzangu kutumika kisiasa kiasi cha kuudhalilisha utu wao. Kijana aiitwaye EDO MWAMA LALA, aliyekuwa katibu wa BAVICHA mkoa wa Mbeya na Adam CHEGULANI (diwani wa jiji la mwanza aliyenyang'anywa kadi),wote hawa walifukuzwa Chadema kwa kutokuwa waadilifu. Wapo kwenye kibarua haramu cha kuhakikisha wanawashawishi vijana (hasa BAVICHA)kutoa matamko ya kumhujumu Dr. Slaa kisiasa kupitia vyombo vya habari.

Na wameanza mpango wao na kwa kiasi kikubwa wameanza kufanikiwa, kwani wamefanikiwa kumshawishi katibu wa BAVICHA mkoa wa MWANZA, ndugu SALVATORY SHUKURU MAGAFU kutoa tamko kwenye vyombo vya habari kuomba chama kimfukuze Dr. Slaa chamani. Pia leo hii tayari wanaye kijana mwingine maarufu wa chadema, atakae toa tamko muda wowote kuanzia sasa, kijana huyu wamemlipia hoteli moja maarufu iliyopo hapa jijini na kumpa fedha za kutosha ili atoe tamko kali la kumlaani Dr. Slaa.

Kwa huu mpango (walioupa jina la MWISHO WA SLAA) ulivyo watajitokeza vijana wengi sana watakaotoa matamko kumlaani Dr. Slaa kwa kutumia mwavuli wa BAVICHA imesema. Kwa akili zao zilivyofupi kama maisha ya funza wanadai wanadhamiria kumuua kabisa Dr. Slaa kisiasa. Na vijana wengi wamekuwa wakishawishika na upumbavu huu wa EDO na ADAM kwasababu ya fedha nyingi wanazopewa baada ya kukamilisha kazi hiyo.

Mpango huu unaofanywa na EDO MWAMALALA na CHAGULANI nyuma yake unafadhiliwa na BERNARD MEMBE, MWIGULU NCHEMBA, NAPE NNAUYE, kwa taarifa nilizo nazo na za kuaminika vijana hawa wanalipwa fedha nyingi sana na viongozi hao waandamizi wa CCM na SERIKALI ambao wamekosa sera na kuamua kuingia kwenye siasa za taarabu.

Kwa Binafsi yangu napenda nitoa tamko rasmi la kulaani kwa nguvu zote vijana wote wa BAVICHA wanaoendekeza njaa mbele na kuweka masilahi ya chama kando kuacha mara moja mchezo huu mchafu. Waache kuwa na akili za Samaki na hatimaye wajitegemee kisiasa. Na niwaombe viongozi hawa wa CCM waache kutumia tatizo la umasikini wa vijana hawa kuwarubuni na kuwatumia wenzao kama mipira ya mapenzi.

Ili kuepuka siasa hizi zisizo na tija kwa jamii niwaombe viongozi wenzangu wa BAVICHA kuachana na kujibizana na hawa wapumbavu, kwani ukijibizana na mpumbavu na wewe pia utakuwa mpumbavu, dhumuni lao tutumie muda mwingi kujibizana nao na tupuuze kujadiliana mambo ya msingi kwa mustakabali wa TAIFA.

CHADEMA tutaendelea kuwa na nguvu na kamwe hatuwezi kupunguzwa nguvu na siasa laini kama hizi. Kinachoshangaza ni kuona anayefadhili ushenzi huu ana ndoto za kuwania Uraisi katika nchi yetu, kweli kwa siasa laini hivi uraisi atauweza?

Imekuwa ni kama tabia yake ya kuwatumia vijana kutimiza malengo yake, kwani ni wazi katika mkutano mkuu wa CCM uliofanyika mkoani Dodoma alituhumiwa na wajumbe wenzie kutumia vijana kusambaza vipeperushii vilivyokuwa vikiwaomba wajumbe wa mkutano huo kumkataa Mwenyekiti wao kwa kisingizio cha kumpunguzia majukumu.

Sasa kashindwa huko anakuja kuingilia siasa za CHADEMA kwa kuwatumia vijana wetu wasiokuwa waadilifu; nimwambie kwa upendo tu kwamba CHADEMA TUKO IMARA KAMA CHUMA.

Na. Alex Nicholaus Thomas MUSHI,
Mjumbe wa Baraza kuu la CHDEMA-Taifa,
Mjumbe wa kamati tendaji BAVICHA-Taifa.
 
Maslahi ya nchi ni zaidi ya karatasi chafu ya ccm. DR. Slaa kurudisha kadi ya walaaniwa ccm siyo mada kwangu mimi.
Kwanza ccm waturudishie fedha zote zilizoporwa na waturudishie maeneo yaliyoachwa mashimo, waturudishie fedha za Uswis, meno ya tembo, magogo ya misitu, fedha anazosafiri nazo kikwete as if ni mfalme, waturudishie..... kadi ya ccm kitu gani bwana?

Hii biashara ya kuhangaika na karatasi ya ccm ni upuuzi.
 
mkuu watanzania wasasa niwaelewa izi kelele za bavicha zitajadiliwa kwa wauza gahawa ila hazina effect yeyote kwa cdm.go go go cdm .njaaaaaaaaaaaa mbayaaaaaa sanaaaaaaa tena kwa mwanaume unaweza kupumuliwa kisigoni
 
CCM, (waasisi wa ufisadi, rushwa, mauaji ya watetezi wa umma,na makabaha wa kisiasa, wadini, wanaowauwa wazanzibar wasio na hatia) mwisho wao ulitabiriwa na sasa umefika.
Mithali 24: 24-25
" Amwambiaye mtu mwovu, wewe una haki;
Kabila za watu watamlaani, taifa watamchukia.

Bali kwao wakemeao furaha itakuwako,
Na baraka ya kufanikiwa itawajilia.
"
 
Walikuja kale ka single kao slaa kachukua mke wa mtu kasingle hakajahit fresh now kametoka kengine ngoja 2one nan bingwa sijui katapotea kama cha awali
 
Haya ni mapambano na hakuna kumdharau adui. Lazima tupambane nao kwa silaha stahiki. Tunavitaka vyombo vya chama vinavyohusika kuchukua hatua mara moja kukomesha upuuzi huo.

Si lazima kujibishana nao, lakini ikiwa katiba ya chama inazuia uasi wa namna hiyo, basi tusichelewe kuwafungia kazi hawa jamaa. Tuwakatae mara moja kwamba si wenzetu katika safari hii ya mageuzi. Let us deprive them of the ground on which they are standing. Let us refuse them our identity and make them swim in the air.

UFANYIKE UCHUNGUZI NA SEKRETARIATE YA BAVICHA AU YA CHAMA ITANGAZE KUTOWATAMBUA WATU HAWA MARA MOJA.

Change is always painful and expensive, but he who accepts to pay its price is awarded endlessly.
 
Nawachukia na nawalaani wooteee wanaopambana na juhudi za kumkomboa mtanzania maskini katika lindi la ufukara kwa kuogofya, kutisha, kuhofisha, kudharau, kupumbaza na hata kudumaza akili na fikra za tunaoteswa kwa dhiki itokanayo na demokrasia tete ndani ya nchi yetu ya kuwachagua watu wa jamii yetu wenyewe kuwa viongozi wetu na mara wapatapo madaraka wanatugeuka na kuwa watawala, wakandamizaji, makaburu, mabepari, wabaguzi na wanyonyaji wa rasilimali na haki zetu watanzania badala ya kuwa viongozi wetu ili watutumikie kwa dhamira ya dhati, utashi, uaminifu na uadilifu mkubwa kwa kutuondelea maadaui wakubwa watatu; umaskini, ujinga na maradhi katika nchi yetu.

NAWACHUKIA NA NINAWALAANI SANA WATU HAWA NA LAANA HII IKA KAE JUU YA VICHWA VYAO WAO NA VIBARAKA WAO.
 
Kwanini na wewe usiwe umepewa Hela ili umchafue Membe na wenzake uliowataja?kwa ni unafikiri maaadui wa Slaa ni hao tu ?,What about the Guy aliyeporwa Mke na Slaa hivi na a deserve kuwa Adui wa Slaa?.
 
Wachawi huwajuwa wachawi wnzake, Wewe umelipwa shilingi ngapi kujidhalilisha na uharo huu hapa??? Kwanini msimshauri arudishe tu kadi ya magamba!?????yaishhe jamani? Ukivuliwa taulo chutama babu!!
 
Maslahi ya nchi ni zaidi ya karatasi chafu ya ccm. DR. Slaa kurudisha kadi ya walaaniwa ccm siyo mada kwangu mimi.
Kwanza ccm waturudishie fedha zote zilizoporwa na waturudishie maeneo yaliyoachwa mashimo, waturudishie fedha za Uswis, meno ya tembo, magogo ya misitu, fedha anazosafiri nazo kikwete as if ni mfalme, waturudishie..... kadi ya ccm kitu gani bwana?

Hii biashara ya kuhangaika na karatasi ya ccm ni upuuzi.
Ndiyo maana kuna tetesi kuwa Salvatory Magafu alinunuliwa na NGELEJA wakati wa uchaguzi mkuu 2010 kumbe naye ni mtu wa kutumika kama condomu.Ngoja nimtafute nimuulize kwa nini anarudisha nyuma harakati za ukombozi wa nchi na watanganyika.
 
dhambi ya usaliti ni mbaya saana, chagulani hata kule Igoma, Mwanza hawamtaki tena, kila akipita anazomewa kwa kifupi amefulia, wauza nyanya, vitunguu waliochanga 50 na mia zao kapata uongozi kawasaliti,
Tatizo lenu vijana Njaa inawasumbua.
 
mwaka wenu huu. lazima mtafute maji gari 100 za fire kuzima moto unaowaka. Sisi wengine tuna ajenda nzito kuhusu kiwanja chetu cha markazi kilichonunuliwa na MZUNGU KUJENGA BAA
 
hawamuwezi slaa kamwe.
hapa duniani umeshawai kusikia mtu kaanguka bafuni alafu hajafa??
 
Edo na ndugu zako hao, your days are numberd. Slaa for presidence 2015
 
Edo na ndugu zako hao, your days are numbered. Slaa for presidence 2015
 
Hata mi nawalani nakuwachukia sana watu wa namna hiyo, wanastahili kufungiwa jiwe la kusagia shingoni na kutoswa baharini, wapotee kabisa.
Lakini ninachowaomba viongozi (BAVICHA) makini na wenye mapenzi ya kweli kwa chama chetu, NI VEMA MKAJITOKEZA HADHARANI NA KUWAKANA HAO PIMBI ili umma wa watanzania utambue ya kuwa ni kweli wanatumiwa kudhoofisha harakati za ukombozi wa taifa letu.
 
Dr.Slaa tupo nyuma yako usikate tamaa...Kikwete pamoja na taasisi yake ya uraisi alipigwa majungu ili avuliwe uenyekiti lakini ikashindikana itakua CHADEMA...hawa vijana wanaotumika siku zao za mwisho zaja.
 
Dr Slaa ni habari ingine hivyo mtapambana naye sana lakini mwisho wa siku lazima ashinde vita hii.
 
Hao vijana wenzangu wametudhalilisha sisi vijana, yaani ndo sisi vijana tunadai tupewe fursa za uongozi kwa kutoa matamko ya kijinga kama hilo lililotolewa na wasaliti huko mwanza?

Mimi nadhani kwa mwelekeo huo hata umri wa urais tuongeze,yaani kijana mzima unatoa matamko kisa karatasi ambayo imebwaga pembeni kwa miaka 15 iliyopita? Mimi nadhani kama kuna lingine Bavicha waseme sio hili. Cdm ondoeni wasaliti hao mara moja. Eti kadi ya ccm?
 
Back
Top Bottom