Kitimtim Bungeni: Wenje atolewa nje ya Bunge

DU!
Mbona leo Bunge linakwenda kimzobemzobe hivyo?
Napenda kujua huyo mwenyekiti ni nani haswa!...i
 
Jaman hebu tujuzen zaidi maana sisi huku umeme hakuna kwa kanuni gani ya bunge katumia kumtoa.
 
Mwongozo wa Spik, soryyy, mwenyekitii..Bunge livunjwe kwa hoja ya dharura...i mean, emergency...kanuni ya 68(4) hooo sory 68(8) Mwenyekiti...mwenyekiti sio mwongozo bali hoja binafisi...Kaa chini..sajenti mtoe nje huyo...mh, nani atoke, usimtoe bwana..., mwongozo wa mwenyekiti kanzwa...tuendelee.Mhe. Waziri wa Mifugo: David Mathayo David..tuendeleee..
Hawa muda si mrefu watachapana makonde humo bungeni!
 
Wabunge wa Chadema wamezidi uhuni, muda wa ziada wa nini wakati Tundu Lisu alisema yuko tayari kutoa sasa hivi. Wanaharibu sana quality ya mijadala.
 
Mwongozo wa Spik, soryyy, mwenyekitii..Bunge livunjwe kwa hoja ya dharura...i mean, emergency...kanuni ya 68(4) hooo sory 68(8) Mwenyekiti...mwenyekiti sio mwongozo bali hoja binafisi...

Kaa chini..sajenti mtoe nje huyo...mh, nani atoke, usimtoe bwana..., mwongozo wa mwenyekiti kanzwa...tuendelee.
Mhe. Waziri wa Mifugo: David Mathayo David..tuendeleee..

nduuu haya mambo ya magamba
 
Kwenye blog ya Michuzi leo hii kuna habari na picha za wanafunzi wanaovua samaki baada ya kufukuzwa shule kwa kushindwa kulipa michango. Huyo Waziri mdogo anayesema hakuna michango anaongelea nchi ipi?
 
Alimwomba Mwenyekiti ili atoe taarifa kwa masilahi ya taifa, akaambiwa atoke nje kwa kuchukuliwa na Surgent of Arm wa Bunge. Wabunge wengine hupewa nafasi ya kutoa taarifa lakini yeye amenyimwa nafasi hiyo.
 
kuna malumbano kuhusu hoja ya tundu lissu kutakiwa awasilishe ushahidi wa waziri kusema uongo. Aliyeanzisha vita ni moses machali aliyehoji inakuwaje lissu awasilishe ushahidi saa tano asubuhi hii wakati yeye ni mbunge na kikao cha bunge kinaendelea, kwa nini asipewe muda awasilishe baadaye. Mwenyekiti kakomaa lissu awasilishe ushahidi saa tano. Baadae kaibuka wenje kuomba kutoa hoja ya kuahirisha mjadala wa bajeti ili bunge lijadili jambo la dharura ambalo yeye amesema lina maslahi kwa taifa. Mwenyekiti amegoma na kusema mjadala wa bunge unaweza kuahirishwa tu pale nchi inapokuwa kwenye vita na kwa sasa nchi haiko kwenye vita. Pamoja na hayo wenje aliendelea kusimama na kutaka kutoa hoja yake lakini mwenyekiti akamtishia kumtumia askari kumtoa wenje nnje. Wenje hakusikia kaendelea kudai ni jambo la dharula ambalo lina maslahi kwa taifa. Baadae mwenyekiti kamuagiza surgent akamtoe wenje nje, sajent akiwa njiani kuelekea kumtoa wenje nje ya ukumbi wa bunge tanesco wakachukua umeme wao huku mitaa ya mabibo, hivyo sijui kilichoendelea baada ya hapo, naomba anayeendelea kutazama bunge atujuze nini kimeendelea.
 
Jazba ilipanda kama ambavyo inaweza kumpanda binadamu yeyote mwenye utashi. Mwenyekiti alikosa busara ya namna ya kuhandle ishu nzima hata kama Tundu Lissu alikubali, kumbuka awali alinyimwa kumalizia kuongea ambapo alitaka kutoa ushahidi pale pale bungeni.
 
Ushahidi ulikuwa mzito sana!Kama kawa usalama ulikuwa matatani!Dunia imewageukia magamba wanamalizana wao kwa wao!Hii haitaachwa hivihivi tunaitaji tujue!
 
Ndugu zangu lile zogo la tundu lisu kudai naibu waziri kadanganya bunge limeendelea ambapo ilifikia hatua ya mwenyekiti wa bunge kutoa amri ya kutolewa nje ya ukumbi wa bunge kwa nguvu na askari wa bunge, lakini kabla hatujashuhudia wenje akitolewa nje, tanesco wakatukkatia umeme. ni siku ambayo mbunge wa zamani wa nyamagana ccm, bw. lawrence masha alikuwa mgeni ndani ya bunge na alitambulishwa. mlioshuhudia kizaa zaa hicho hadi mwisho tusaidieni kutujuza..
 
Leo na siku nyingine zijazo wabunge watajulikana ajenda zao,kama ni taifa ama ni chama!
 
Samirnasri, pole kwa umeme kuchukuliwa..ila nafikiri ilikuwa ishu ya transmission...watakuwa walikuwa wanakata ili watazamaji tusione...walianza kukata Star, then Mlimani...ila Baba lao TBC hawakukata.....mwisho, Wenje katolewa nje na baadhi wabunge wengine (watakuwa wa chadema nafikiri) walifuata njia. Halima Mdee naye alitaka kutoa taarifa, Mwenyekiti akamkatalia.....Bunge linaendelea kwa hotuba ya Waziri.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom