McLaren
JF-Expert Member
- Feb 19, 2025
- 889
- 2,863
Mbunge wa Jimbo la Ubungo ambaye pia ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Mipango na Uwekezaji, Professa Kitila Mkumbo (CCM) leo Novemba 22, 2025 ametimiza ahadi ya kukabidhi mashine za kushonea(cherehani) nne kwa mafundi waliopo mtaa wa Mwembeni, Kata ya Manzesse, jimbo la Ubungo.
Kitila amekabidhi cherehani mbili kwa mafundi wa kushona nguo na cherehani mbili kwa mafundi wa viatu ikiwa ni sehemu ya ahadi alizoahidi kwa wajasiriamali hao wakati wa kampeni za uchaguzi mkuu.
Ametumia wasaa huo kuwaahidi wananchi hao kuwa ataendelea kukutana na makundi mbalimbali jimboni hapo kutatua changamoto na kuendelea kutimiza ahadi alizoahidi