KITILA: Bajeti ya Maji Inatosha

KITILA: Bajeti ya Maji Inatosha

Kauli ya Kitila Mkumbo naiunga mkono. Fedha inatosha. Hizo hoja za Wabunge za kutaka kuongeza tozo tsh 50 kwenye nishati itasababisha mfumuko wa bei na wananchi watazidi kusoma namba. Wabunge wetu ni Wavivu kufikiri na wanatanguliza maslahi yao binafsi wanang'ang'ania hii option bila kuangalia athari yake ndani ya Jamii. Wabunge walitakiwa kuumiza vichwa na kuja na mapendekezo ya vyanzo vipya vya mapato.
 
Wasambaze Maji watapata fedha za kutosha.katibu kitilya analijua hilo
 
KATI YA BILIONI 900 ZILIZOTENGWA KTK BAJETI YA 2016/17, ZILIZOTOLEWA NI BILIONI 150 TU
HIZI BILIONI 650 ZIKITOLEWA ZOTE ZITATOSHA.-----MSUKUMA.

NGOJA NINUNUE GAZETI NIONE KITILA KWANINI KASEMA ZINATOSHA NDIYO NIWEZE FAHAM KUWA ZINATOSHA AU VIPI.
 
Huyu naye anajipendekeza. Alipokuwa nje ya system alikuwa anapost post kwenye mitandao. Leo vipi tena?
Mkuu...wazungu wa wingereza wana methali yao, wakisema "the lips of righteous teaches many, but fools die for want of wisdom"..
Kina sie, wapenda kujifunza, halitushangazi hili la Kitila...wa, kinyume na kujifunza, watasumbuka na hili, na mengine mengi...
Rais wa awamu ya 3, wakati mmoja akihutubia bunge alitoa kisa cha mlevi, aliekosea,akaingia sehemu ya nyuma ya gari, na kwa vile nyuma hakuna usukano, wala vikanyagio vya kuongeza mwendo, na kusimamisha gari, nakulainisha kubadilisha gea, mlevi aliamini kaibiwa, na akapiga simu polisi akitaarifu juu ya wizi ktk gari lake, na akiomba msaada wa polisi....wakati polisi wakijiandaa kwenda eneo la tukio, wakapokea simu toka kwa mtu huyo huyo, akiwaomba msamaha kwa usumbufu, na kuwataarifu kuwa alipokuwa akipiga simu ya kwanza alikuwa nyuma, sasa kaingia mbele, ameona kila kitu kiko sawa na salama....
..kuishi kwingi(huku ukijifunza),ni kuona mengi na kujua mengi...
Na tumuombee Kitila ktk majukumu yake mapya, na kulijengà taifa
 
Hata kama kwa namba inatosha ila nchi hii ina utaratibu wa kutokamilisha kabisa kiasi cha pesa kinachotengwa kama bajeti kwenye wizara husika, sijui kuna haja gani ya kwenda kukaa bungeni kutumia hela kupitisha bajeti zisizo tekelezwa mwaka baada ya mwaka?! upuuzi tu.
 
Huyu naye anajipendekeza. Alipokuwa nje ya system alikuwa anapost post kwenye mitandao. Leo vipi tena?
HISTORIA, MNAKUWA WEPESI KUSAHAU HISTORIA. AMETOKA CDM KWA USALITI, HUYU NI MSALITIT TU! AMEANZA KUTUSALITI ETI BAJETI INATOSHA. MSALITI NI MSALITI TU. CDM WALIKUWA NA HAKI YA KUMFUKUZA
 
Inawezekana kweli inatosha endapo itatumiwa kwa nidhamu ya hali ya juu pasipo na ufujaji...

hahahahahahhahaahah....seriously..hii comment ni toka kwako...hahahahahahha...kweli 2015 imevuruga watu
 
Huyu naye anajipendekeza. Alipokuwa nje ya system alikuwa anapost post kwenye mitandao. Leo vipi tena?
Ni rahisi kumabadilisha shetani akawa mwema akikaa na Malaika kuliko kumpeleke Malaika kwenye kundi la Mashetani, naye atakuwa shetani!
 
KATI YA BILIONI 900 ZILIZOTENGWA KTK BAJETI YA 2016/17, ZILIZOTOLEWA NI BILIONI 150 TU
HIZI BILIONI 650 ZIKITOLEWA ZOTE ZITATOSHA.-----MSUKUMA.

NGOJA NINUNUE GAZETI NIONE KITILA KWANINI KASEMA ZINATOSHA NDIYO NIWEZE FAHAM KUWA ZINATOSHA AU VIPI.
Yeye anasema Zinatosha kama zikitolewa zote...
 
Mi naona wabunge wanapiga kelele tu, bajet mkulu ndo anapanga
 
Ukitaka kuipima hii Wizara ya Maji fanya analysis hii ndogo..

Bajeti ya 2016/17 ilikuwa Tsh 900+Bil zilizotolewa ni around 192 Bil Tu.
Maana yake miradi mingi haikutekelezwa kwenye mwaka wa fedha unaoisha kwasababu Hazina ilitoa fedha kidogo sana.

Haya sasa Bajeti hii ya 2017/18 ni Tsh 600+ Bil, sijui zitatoka ngapi.
Ukumbuke kuna viporo kibao huko nyuma.

Halafu Mnafiki anakwambia hela Zinatosha.
 
Naona laana ya kula rambi rambi bado inawaandama watu huko Kibiti
 
Ukitaka kuipima hii Wizara ya Maji fanya analysis hii ndogo..

Bajeti ya 2016/17 ilikuwa Tsh 900+Bil zilizotolewa ni around 192 Bil Tu.
Maana yake miradi mingi haikutekelezwa kwenye mwaka wa fedha unaoisha kwasababu Hazina ilitoa fedha kidogo sana.

Haya sasa Bajeti hii ya 2017/18 ni Tsh 600+ Bil, sijui zitatoka ngapi.
Ukumbuke kuna viporo kibao huko nyuma.

Halafu Mnafiki anakwambia hela Zinatosha.
Kwa maelezo yake kama zitatolewa zote.
ila nionavyo kama kwa utaratibu wa kutoa asilimia 10 ya kile kilichopangwa, tatizo litaongezeka zaidi...
 
New-Doc-2017-05-15_21.jpg


-amesema endapo pesa zote Bil672 zinatosha kutekeleza mipango yote ya mwaka huu.
-Amesema pamoja na kujitosheleza kwa miladi hiyo, bado wizara hiyo imepata mkopo wa Dola 500 Mil kutoka Exim Bank India, ambayo itatolewa kwa muda wa miezi 30 itakayosaidia miradi katika miji 16 Tanzania bara na mmoja Zanzibar.
-Wakipata fedha hizo zitasiaidia zaidi katika kutekeleza miradi yao.

Maelezo zaidi:http://www.mwananchi.co.tz/habari/K...-mwaka-huu/1597578-3927304-yypslwz/index.html

Ndiyo maana kila siku huwa nasema humu kuwa kuna Watu wanajiita ' Maprofesa ' huku wengine wakiwa na wana PhD zao lakini sidhani kama kweli ziliwastahili na pengine hawa hawa ndiyo wanatukatisha ' tamaa ' hata sisi wengine kuendelea kusoma ili tufikie hizo ngazi zao kubwa za Kitaaluma.

Technically tu hadi Mtu kuja kuijua Ofisi na hasa kujua ' Utendaji ' wake inaweza kumchuku kati ya miezi sita hadi tisa na ikiwezekana hata mwaka sasa cha kushangaza zaidi huyu Professor hana hata miezi mitatu Ofisini leo ' anaibuka ' tu na ' kukurupuka ' kusema ' Bajeti ' ya Wizara yake ya Maji inatosha.

Tuache Sifa za ' Kijinga ' na kuwa na ' Viherehere ' na ukweli ni kwamba Professor Kitila Mkumbo bado hajaijua vilivyo hiyo Wizara ila kama angeitoa kauli hii katika Bunge la Bajeti la mwakani ningeweza kukubaliana nae. Eti huyu nae ndiyo mmoja wa Wasomi ambao Tanzania tunaweza ' Kujivunia ' nao. Shabaaaaaash!
 
Back
Top Bottom