Kuelekea 2025 KITETO: Kata ya Engusero yapokea ambulance mpya, wananchi wamshukuru Rais Samia

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
May 16, 2020
2,077
1,001

Wananchi wa Kata ya Engusero Jimbo la Kiteto wamemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuwapatia Gari jipya la wagonjwa ambalo litawaondolea adha ya Usafiri wa wagonjwa katika Kata hiyo na Tarafa nzima ya Matui.

Pia, Mbunge wa Jimbo la Kiteto, Mhe. Edward Ole Lekaita amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa Gari jipya la wagonjwa ambalo litawasaidia Wananchi wa Kata ya Engusero na maeneo ya jirani na kwa miradi mingine mingi ambayo Kiteto imepata kwa kipindi kifupi


Mhe. Edward Ole Lekaita ametumia hadhara hiyo kuhutubia Mamia ya Wananchi wa Kata ya Engusero waliojitokeza kumpokea na kupokea Ambulance mpya ambapo amewataka kulitunza gari hilo ili liweze kusaidia Tarafa nzima ya Matui
 
Watanzania wakiona hivi, roho kwaaatu kabisa, ukiwaeleza kwa nini hujaongeza mshahara halafu unawaonyeaha mambo kama haya, SGR, Mwalimu Nyerere, barabara, mashule, vituo vya afya na zahanati, Kigongo Busisi, Jangwani, kwa kweli vifua vyetu sisi watumishi vinatabasamu na kuelewa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…