Kitengo chetu cha maafa kilikuwa hewa?

Kitengo chetu cha maafa kilikuwa hewa?

Mshana Jr

Platinum Member
Joined
Aug 19, 2012
Posts
360,596
Reaction score
830,270
Kitengo hiki muhimu sana cha taifa kinaweza kuwa kashfa nyingine kubwa! Hatukuona makali yake hakikusikika popote mpaka waziri mkuu alipoamua kutembeza bakuli kusaidia wahanga wa tetemeko la ardhi lililotokea Bukoba na maeneo mengine ya Tanzania
Hiki kitengo kilipata umaarufu mkubwa enzi za Mzee Mkapa labda kutokana na majanga mengi ya wakati ule lakini pengine na mahitaji ya kisiasa
Kuna maswali mengi kukihusu hiki kitengo
Kiko chini ya wizara gani?
Wafanyakazi wake wanapatikanaje?
Mkurugenzi wake ni nani?
Ofisi zake ziko wapi?
Akaunti zake zikoje? Zinasimamiwa na nani?
Hili tukio la tetemeko linaweza kufumua makaburi yaliyokwisha sahauliwa lakini pia litukumbushe kuwa Tunahitaji kama taifa sasa kuwa na hiki kitengo kinachojitegemea bila mikono ya wanasiasa
1473850851742.jpg
1473850857389.jpg
1473850864549.jpg
1473850869449.jpg
1473850874911.jpg
 
1473851797349.jpg
tuna pa kuanzia kumbe! Tuna pa kuhoji kumbe! Wakati serikali ikitembeza bakuli nina hakika hawa nao walikuwepo lakini hawakujitambulisha! Kwanini wasijitambulishe? Au walikuwa eneo la maafa wakiendelea na majukumu? Je wameshasema chochote? Je zile takwimu za vifo majeruhi na uharibifu wa mali zinatoka kwao?
 
Hivi ni wangapi wanajua tuna hiki kitengo Tanzania?

nimejiuliza sana hilo swali sikupata jibu......wakati wa ajali ya train na majanga mengine enzi zile kitengo kilisikika na kilikuwa na pesa sikumbuki kama walengwa walipata kinachowastahili.......nadhani kinakuwa chini ya waziri mkuu ? hivi na Tanzania Red Cross nayo si inahusika kwa janga kama hili au hawajapa funds kutoka kwa wajomba?
 
Hiki kitengo kipo ila walikuwa wamezidisha kupiga pesa. Mkuu mpaka sasa kuna watu wa Kitengo cha Maafa wako mung'anda kwa kuiba masufuria ya wahanga.
WATUMISHI OFISI YA WAZIRI MKUU KIZIMBANI KWA TUHUMA ZA WIZI WA SUFURIA NA MIKEKA - ZOTE KALI BLOG
Duu mikeka mabati na masufuria thamani yake milioni mia moja waliamini hakuna majanga yatakayotokea tena (hii ilikuwa 2014)na pengine waliamua kufanya hivyo baada ya wakubwa wao kugawana mafungu manono ikiwemo magari pengine
Nina uhakika hii kesi haipo tena lakini kwa mwendo huu inaweza kufufuka
 
Mkuu nimehoji sana kwenye uzi ulioletwa na Lizabon lakini sikupewa majibu. Kitengo kipo na kila mkoa nadhani kina ofisi kama nilivyosoma kozi fulani "disaster management and. ......." sasa sijui kwa hili imekuaje.
Nimeenda mbali nikahoji upande wa vyombo vyetu vya usalama vile pendwa "JKT na JWTZ", Maana baadhi ya taarifa kuna mama mmoja niliona analalamika kuhusu usalama wao dhidi ya vibaka pia nikasema Kwanini vyombo hivi visingetusaidia kuwajengea vibanda vya muda ili wajihifadhi?

Hasira.
 
Hivi ni wangapi wanajua tuna hiki kitengo Tanzania?
HIKI KITENGO KIKO KIUPIGAJI....MAAFA MENGI YALIYOKUWA YANATOKEA ILIKUWA HAIFANYI LOLOTE.....PITIA HISTORIA TU MAAFA MENGI YALIYOKUWA YAKITOKEA MPAKA LEO HAKUNA WAKICHOFANYIWAAAA...MFANO WALE WA MAFURIKO KILOSA MPAKA LEO NI WANAISHI VIBANDANI AHADI ZILE WALIZOPEWA KIMYAA MPAKA LEO

OVA
 
Vyombo Hivi vinatumika TU katika maonesho ya siku maalum Zile....kwa kutuonesha mazoezi yaooo

Ova
Mkuu nimehoji sana kwenye uzi ulioletwa na Lizabon lakini sikupewa majibu. Kitengo kipo na kila mkoa nadhani kina ofisi kama nilivyosoma kozi fulani "disaster management and. ......." sasa sijui kwa hili imekuaje.
Nimeenda mbali nikahoji upande wa vyombo vyetu vya usalama vile pendwa "JKT na JWTZ", Maana baadhi ya taarifa kuna mama mmoja niliona analalamika kuhusu usalama wao dhidi ya vibaka pia nikasema Kwanini vyombo hivi visingetusaidia kuwajengea vibanda vya muda ili wajihifadhi?

Hasira.
 
Duu mikeka mabati na masufuria thamani yake milioni mia moja waliamini hakuna majanga yatakayotokea tena (hii ilikuwa 2014)na pengine waliamua kufanya hivyo baada ya wakubwa wao kugawana mafungu manono ikiwemo magari pengine
Nina uhakika hii kesi haipo tena lakini kwa mwendo huu inaweza kufufuka
Mkuu kesi hii imefunguliwa mwaka huu. Kama unakumbuka kuna yale majanga ya mafuriko Dar mwaka 2014. Jamaa walilamba hivyo vifaa na manusura waliambulia patupu!
 
Mkuu nimehoji sana kwenye uzi ulioletwa na Lizabon lakini sikupewa majibu. Kitengo kipo na kila mkoa nadhani kina ofisi kama nilivyosoma kozi fulani "disaster management and. ......." sasa sijui kwa hili imekuaje.
Nimeenda mbali nikahoji upande wa vyombo vyetu vya usalama vile pendwa "JKT na JWTZ", Maana baadhi ya taarifa kuna mama mmoja niliona analalamika kuhusu usalama wao dhidi ya vibaka pia nikasema Kwanini vyombo hivi visingetusaidia kuwajengea vibanda vya muda ili wajihifadhi?

Hasira.
Masikio yao yametiwa nta halafu wamevaa miwani ya mbao inawezekana kabisa kuna sensitive organ (chama cha siasa? ) inahusika na kifo cha hiki kitengo!
Kama kweli kimekufa huu unaweza kuwa upuuzi wa kiwango cha lami, upuuzi wa karne
Kuna hiyo link hapo juu ikielezea watendaji wake kugawana mali za kitengo cha maafa mwaka 2014! Kwanini waliamua kugawana mali? Jibu ni moja tu kilikuwa kinazikwa rasmi...sasa hawa waligawana vitu vipi kuhusu akaunti za benki? Vipi kuhusu magari majengo nk ?
 
Mkuu hao waliyogawana malí inabidi wakamatwe na wafungwe jiwe siyo na kutumbukizwa nalo baharini au ziwani

Nimeanza kuhisi vibaya na Mwenyezi Mungu aniepushe kuwaza haya.
Lile jimbo linaongozwa na chama gani? Naanza kuelewa maana ya mafiga matatu.
Ngoja nisiende huko, naamini watatusikia ili kitengo kirudi maana nilichokisikia kutoka kwa WM ni kuwa kuna kitengo cha tathimini, ngoja kifanye tathimini alafu tuone impact yake kwa wahusika.
 
Nasikia mwaka huu wametiwa nguvuni ila wako nje kwa dhamana
 
Nimeanza kuhisi vibaya na Mwenyezi Mungu aniepushe kuwaza haya.
Lile jimbo linaongozwa na chama gani? Naanza kuelewa maana ya mafiga matatu.
Ngoja nisiende huko, naamini watatusikia ili kitengo kirudi maana nilichokisikia kutoka kwa WM ni kuwa kuna kitengo cha tathimini, ngoja kifanye tathimini alafu tuone impact yake kwa wahusika.
Mmh kweli kabisa! Siasa zimehusishwa hapa....najaribu kulinganisha dhana ya kunyimwa mkono na dhana ya kunyimwa kura na matamshi ya visasi
 
Back
Top Bottom