GAZETI
JF-Expert Member
- Feb 24, 2011
- 5,292
- 6,773
Kwa sasa majukumu ya Polisi yamekuwa mengi sana, maana kuna wakati wanafanya kazi za watu wa maliasili, kazi za TRA pia kazi zao za kupambana na uhalifu. Mara wakimbize magunia ya mkaa, mara waulize risiti n.k
Kutokana na ugumu huo napendekeza kitengo hicho cha usalama barabarani kipelekwe jeshi la Magereza au JKT ili polisi wafanye kazi nyingine ambazo ni nyingi kwelikweli.
Pia kumekuwa na shutuma nyingi kwa jeshi la polisi hususani kitengo cha usalama barabarani, jeshi la Magereza na JKT halina shutuma kubwa katika uendeshaji wa mambo yao hivyo ni vema wakikabidhiwa majukumu haya au IUNDWE IDARA AU JESHI LA USALAMA BARABARANI AMBALO LITAKUWA LINAJITEGEMEA.
Ni mtazamo wangu tu wakuu, hata kama hakuna nchi inafanya hivyo si vibaya tukiwa wa kwanza.