Mshangai
JF-Expert Member
- Feb 16, 2008
- 468
- 1,086
Moja ya vitengo vilivyo sahauliwa na kuleta mateso kwa watumishi wa Umma waliotumikia nchi hii kwa uadilifu mkubwa ni PENSION SECTION pale Wizara ya Fedha.
Kitengo hiki ukianzia pale Registry hadi katika kuandaa malipo ni kero kubwa sana. Watu hawawajibiki na wamejawa na dharau kwa vile wanahudumia wazee ambao wanaona hawana uwezo wa kuwafanya kitu tena.
Registry kuna wamama pale wanaweza kupokea claim za watu na kukaa nazo hata miezi miwili eti faili halionekani na hawajali kitu. Jee huo ndio utendaji wa awamu ya tano? Au ni kwa vile waziri Mpango ni mpole sana hivyo hajihusishi na yanayoendelea kitengo hicho?
Au Katibu mkuu wa Fedha naye anaona kitengo hicho ni kama kushughulikia maiti? Ikumbukwe hao wanaodharauliwa kama maiti ndio walio jitoa kutumikia nchi hadi kuifikisha hapa ilipo na wengi wao hawakuwa mafisadi ndio maana kwao pension wanaiona ni heshima kwao japo ni ndogo.
Majuzi nimeenda pale kushughulikia mzee wangu mgonjwa sasa lakini nikajiuliza mbona Magufuli alikomesha utendaji wa aina hii Muhimbili na idara zingine kwa nini hapa Pension Hazina mambo ni kama yale ya zamani?
Umefika wakati sasa tuwataje kwa majina watumishi wa pale Pension ambao wanasumbua wazee na kuwataka wengine watoke huko mikoani kuja hapo kufuatilia visenti vyao ilihali kila kitu kipo na kingeweza kufanyika bila ya wao kuja.
Dr Mpango kama umeshindwa basi tumuite Magufuli atembelee hapo ajionee jinsi pending za kazi zilivyo na UTUKUFU wanaojifanya wanao watumishi husika.