Kitengo cha Mawasiliano ya Umma CHADEMA, Kunani? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kitengo cha Mawasiliano ya Umma CHADEMA, Kunani?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by muhosni, Feb 27, 2011.

 1. muhosni

  muhosni JF-Expert Member

  #1
  Feb 27, 2011
  Joined: Feb 12, 2011
  Messages: 1,114
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Naomba kuweka masikitiko yangu kuhusu kitengo cha mawasiliano ya umma cha Chadema hapa janvini. Watu mbali mbali wamekuwa wakilalamika na kutoa ushauri kwa muda sasa, lakini nasikitika kwamba sijaona jitihada za kuboresha kitengo hiki.

  Masikitiko yangu yamejikita zaidi kwenye maandamano na matukio makuu ya Chadema hasa yale yaliyotokea kuanzia Desemba 2010 hadi leo.

  Tunaambiwa kwamba kikao cha uchaguzi wa Meya Arusha mjini kilikuwa na vurugu. Hatukupata picha hata moja hadi leo. Tukaambiwa kwamba katika kikao hicho Godbless Lema alipigwa na polisi. Picha pekee tuliyopata ni ile ya Godbless Lema akiwa amelazwa hospitalini

  Kukawa na maandamano tarehe 5 Januari, picha tulizopata ni zile za kuokoteza kutoka kwa washabiki tu. Polisi walichakachua picha zoa wakatuonesha lakini Chadema hawajawahi kutuonesha chochote. Kuna watakaodai kwamba TV za Tz hazikubali kurusha vipindi vya Chadema. Mimi nitasema kwamba teknolojia imekua, kuna YouTube, na pia blogs kama JF. Zisambazwe kwa CD.

  Tarehe 12 Januari kukawa na mazishi ya waliouawa na polisi. Hadi leo hatujapata picha rasmi kutoka chadema.

  Kumekuwa na maandamano yaliyoanzia Mwanza na jana yalikuwa Mara. Hali ni ileile.

  Wakati wa tukio, tunapewa taarifa na members pengine na viongozi kama Regia kwamba ni nini kinachoendelea. Lakini hatupati picha za kuanzia mwanzo wa tukio hadi mwisho. Na hatuoni jukumu la kitengo cha mawasiliano ya umma katika hili.

  Sipingi wakereketwa na wapenzi kuturushia picha moja au mbili (baada ya kuchelewa na kuomba sana). Sipingi wakereketwa na wapenzi wa Chadema kutupa updates za kinachoendelea kwenye tukio fulani. Tungeweza kupata zaidi kama kuna kitengo rasmi kilichopewa vifaa na kina watendaji waliofuzu kutumia teknolojia ya kisasa.

  Kama tungekuwa tunapata picha na taarifa za tukio kadri linavyotokea, polisi na ccm wasingeweza kudanganya wananchi kirahisi. Lakini sasa hivi jambo kubwa linatokea halafu kinachofuata ni malumbano ya maneno kati ya serikali/ccm/polisi na Chadema. Kama vile bado tunaishi katika karne ya 17.

  Kuna swala la kutunza kumbukumbu pia, sijui matukio haya makuu yenye historia ya nchi yetu yatakuwa yamehifadhiwa vipi.
   
 2. M

  MsandoAlberto JF-Expert Member

  #2
  Feb 27, 2011
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 1,019
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  I have taken note of your contribution. I will personally forward it to those responsible.

  Thank you for such progressive thoughts.
   
 3. Nanyaro Ephata

  Nanyaro Ephata Verified User

  #3
  Feb 27, 2011
  Joined: Jan 22, 2011
  Messages: 979
  Likes Received: 182
  Trophy Points: 60
  Wazo zuri,litafanyiwa kazi ASAP
   
 4. Goldman

  Goldman JF-Expert Member

  #4
  Feb 27, 2011
  Joined: Dec 10, 2010
  Messages: 1,261
  Likes Received: 852
  Trophy Points: 280
  Umenena ni mambo ya msingi na nataka viongozi wa cdm waliosikia na walitendee kazi asap.
   
 5. Gurudumu

  Gurudumu JF-Expert Member

  #5
  Feb 27, 2011
  Joined: Feb 5, 2008
  Messages: 2,350
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  Hivi mbona inaonekana ni tatizo sana hiki kitengo kusikia maoni ya watu na kuboresha huduma zake. Ukienda kwenye website yao imelala doro kabisa wakati matukio yanatokea kila siku. Au Chadema hawana kitengo kama hiki? Kama hawana basi waanzishe ASAP!
   
 6. Crashwise

  Crashwise JF-Expert Member

  #6
  Feb 27, 2011
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 22,172
  Likes Received: 862
  Trophy Points: 280
  Matatizo haya hajaanza jana hata kipindi cha kampeni kuna kipindi nilikuwa nagundua kuna mkutano wa chadema mchana kupitia JF.. Mfano siku Dr Slaa alipokuja Arusha watu wengi walipata taarifa akiwa ameshafanya mkutano wa kwanza ambao ulifanyika mbauda kisha kuelekea Monduli na baadae kurudi tena Arusha ndipo watu walijitokeza kwa wingi na wengi wakilaumu kutokupewa taarifa mapema, ikafatiwa na mkutano uliofanywa na Mbowe kwenye viwanja vya NMC siku chache kabla ya uchaguzi walitangaza saa 5 asubuhi na mkutano ukafanyika saa 8 mchana, Gari la matangazo lilipita baadhi ya mitaa, kuna kipindi picha za mgombea uraisi zilikuwa hazipatikani hata madiwani hawakuwa na picha za mgombea, tatizo hilo lilikuwa linajitokeza pia kwenye upatikanaji wa bendera za chama...niliamini ilikuwa ni hali ya uchumi kwani chama kilikuwa na mambo mengi sana ukilinganisha na mapato waliyo kuwa wakipata kipindi kilicho pita lakini nitaomba lifanyiwe kazi maana angalau kwasasa mfuko umetuna kidogo.
   
 7. Crashwise

  Crashwise JF-Expert Member

  #7
  Feb 27, 2011
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 22,172
  Likes Received: 862
  Trophy Points: 280
  Ni swala la kutoa kipaumbele tu, wameshindwa kuajiri webmaster kwa ajiri ya ku-update website ya chama...ni kitu cha kushangaza sana kuona website ya chama iko doro wakati ile wabsite ni dynamic ni rahisi tu ku-update....
   
 8. T

  TwendeSasa Senior Member

  #8
  Feb 27, 2011
  Joined: May 24, 2008
  Messages: 128
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Naunga Mk0‹2no kwa asilimia zote..katika hali ya sasa Cdm lazima wakiwezeshe kitengo cha habari na kiweze ku updates kila kitu na kwa wakati..tunataka tujue Dr slaa anafanya nini,maandamano yanaendeleaje viongozi wanasemaje, makongomano ,mipango na kila information kwa ajili ya kutupa nguvu na moyo.ukitegemea magazeti na Tv ni rahis kuzichakachua ..Naunga Mkono Hoja
   
 9. PrN-kazi

  PrN-kazi JF-Expert Member

  #9
  Feb 27, 2011
  Joined: Feb 5, 2011
  Messages: 2,890
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 135
  Kwa kidogo kilichopo kitumike vizuri ili atimae kilete faida. Kitengo cha habari na mahusiano ya umma kwa CDM inabidi kiboreshwe ili kila tukio linalotokea wadau walipate kwa ufasaha.
  naunga mkono hoja.
   
 10. sijuikitu

  sijuikitu JF-Expert Member

  #10
  Feb 27, 2011
  Joined: Feb 8, 2011
  Messages: 286
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  naunga mkono hoja...CDM, shughulikieni hili jambo ASAP
   
 11. b

  bagamoyo JF-Expert Member

  #11
  Feb 27, 2011
  Joined: Jan 14, 2010
  Messages: 4,534
  Likes Received: 2,114
  Trophy Points: 280
  Ni wazo zuri lakini kwa vile SISIEMU na serikali yake bado ni 'wababe', kuwawekea kila kitu hadharani officially vitu vinaweza ku-'back-fire' maana CCM hawachelewi 'kuchakachua' wacha tuendelee 'kuwastukiza na nguvu ya umma' .

  Hivyo 'nguvu ya umma' kupitia JF ndiyo mojawapo ya source ya mawasiliano kwa sasa, maana kwa njia hii ya 'ushirikishwaji wa nguvu za umma' katika kueneza sera na habari za CHADEMA, chama kina uhakika kuwa huu moyo wa kujitolea kutoa habari za matukio toka mashinani ni dalili tosha CHADEMA inakubalika na 'kikishaeleweka' baadaye ktk KATIBA MPYA YA TANZANIA basi mambo yatakuwa more official. kwa sasa acha nguvu ya umma iburuzane na SISIEMU iwe maandamano, forums n.k

  Mtindo wa mpaka 'katibu mkuu ofisi ndogo ya CCM Lumumba' kuwa njia pekee ya kutoa habari ni sawa na kupora haki za 'nguvu ya umma' kuwasiliana wenyewe kwa wenyewe bila kutegemea mfumo rasmi.
   
 12. Kurunzi

  Kurunzi JF-Expert Member

  #12
  Feb 27, 2011
  Joined: Jul 31, 2009
  Messages: 4,006
  Likes Received: 328
  Trophy Points: 180
  Nani mkurugenzi ya hii idara?
   
 13. TUNTEMEKE

  TUNTEMEKE JF-Expert Member

  #13
  Feb 27, 2011
  Joined: Jun 15, 2009
  Messages: 4,582
  Likes Received: 55
  Trophy Points: 145
  ndugu yangu CHADEMA kinakuwa tu kwa nguvu za mungu..wala hakuna kitengo idara wala hata dawati la mawasiliano ya umma...kuna idara ya habari na uenezi ambayo wamemuweka jamaa mmoja aliyewahi kuwa mbunge wa kisesa miaka ya nyuma na akashindwa shindwa baadaye mtu ambaye hana uwezo hata kidogo..mawazo yake yeye ni NGONO masaa 24..
  SIKU WATANZANIA WAKIIJUA CHADEMA HALISI NDIO MWISHO WA UPINZANI NCHINI
   
 14. muhosni

  muhosni JF-Expert Member

  #14
  Feb 27, 2011
  Joined: Feb 12, 2011
  Messages: 1,114
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Mkuu, ama akili yangu ni ndogo sana sijaweza kukuelewa ama wewe hujaelewa mada vema
   
 15. muhosni

  muhosni JF-Expert Member

  #15
  Feb 27, 2011
  Joined: Feb 12, 2011
  Messages: 1,114
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Kama hayo ndiyo matatizo, kwa nini wasishutuke watu wanapolalamika tangu wakati wa kampeni za uchaguzi hadi leo? Kuna mada nyingine ilikuwa hapa wiki iliyopita mzemaji mmoja akasema kama chadema inashindwa kusikiliza kilio cha wananchi juu ya hili kwa muda wote huu basi haina tofauti na ccm
   
 16. muhosni

  muhosni JF-Expert Member

  #16
  Feb 27, 2011
  Joined: Feb 12, 2011
  Messages: 1,114
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Hatukujua leo wana ratiba gani hadi Regia alipotuambia wanatembelea nyumbani kwa Nyerere. Hatujui kesho watakuwa wapi wala siku zingine wiki ijayo watakuwa wapi
   
 17. raybse

  raybse Senior Member

  #17
  Feb 27, 2011
  Joined: Oct 22, 2010
  Messages: 104
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Na website ya CDM haiko updated Ina habari za siku nyingi sana. Nadhani tukubali hiki kitengo kina matatizo na kinahitaji kurekebushwa Haraka iwezekanavyo tafadhari wanahusika tunaomba ili lifanyiwe kazi Haraka....sitaki kuamini kwamba chama hakina Uwezo wa Kuendesha kitengo hiki kwa Kisasa zaidi.....ni Kama kimekufa kwa sasa......PLZ TUNAWAOMBA JAMANI TUACHE KURIDHIKA!!
   
 18. kipipili

  kipipili JF-Expert Member

  #18
  Feb 27, 2011
  Joined: Jul 29, 2009
  Messages: 1,499
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 145
  naunga mkono hoja
   
 19. K

  Kakalende JF-Expert Member

  #19
  Feb 27, 2011
  Joined: Dec 1, 2006
  Messages: 3,259
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 135
  Tusiwalaumu CDM kwa hili kwani chama kimepanuka kwa haraka mno katika kipindi cha kuelekea na baada ya uchaguzi 2010. Hizi zinaitwa growing challenges na taasisi zote zinazokuwa huyapitia haya. Matarajio ya watu kwa Cdm ni makubwa na kuyatimiza ni changamoto kubwa. Naamini wahusika wameyaona maoni yenu na muda si mrefu tutaona mabadiliko.
   
 20. muhosni

  muhosni JF-Expert Member

  #20
  Feb 27, 2011
  Joined: Feb 12, 2011
  Messages: 1,114
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Mkuu sidhani kama kukua ni tatizo. watu wanazungumzia umuhimu wa kitengo cha mawasilianao kwa umma na ushauri huu umetolewa tangu wakati wa uchaguzi walipoluwa wanapata michango yetu mingi sana kupitia friendsofslaa na sasa wana ruzuku. Propaganda na mawasilianao kwa chama chochote cha siasa ni lazima. Ilitakiwa washindwe kufanya lingine lolote lakini wahakikishe mawasiliano kwa umma ni imara na ya kisasa kabisa
   
Loading...