mushairizi
JF-Expert Member
- Nov 27, 2011
- 292
- 249
Ni kweli tatizo lipo. Na nadhani watimishi wa ardhi wanajiona wao ni final hakuna mwingine mwenye maamuzi. Hiyo inatokana na sheria za ardhi zilivyo kuna mapungufu mengi ambayo yanatoa mwanya kwa maafisa kufanya wanayofanya. Kimsingi hakuna sababu ya msingi kuchekewesha hati ya mtu na hasa kwenye maeneo ya urasimishaji kwa sababu ziko kamati za wananchi ambazo zinaratibu zoezi zima. Lakini pia kuna ucheleweshaji unaotokana na maeneo yaliyonyakuliwa na CDA kwa wazawa yakapimwa mashamba, mashamba hayo yakatelekezwa kwa zaidi ya miaka 20 na kuendelea na sasa hawataki kufuta umiliki wa mashamba hayo kwa vile wanataka nao kupata maeneo lakini ukiingia ndani unaona wazawa wameendelea kuyaendeleza na wametambuliwa kama wamiliki wa maeneo hayo na kamati zinazo husika kwa sababu wanajua historia ya wamiliki halali wa maeneo hayo. Kweli lipo tatizo.Wivu tu unakusumbua mleta mada