Kitengo cha Ardhi jiji la Dodoma kimeoza

Kitengo cha Ardhi jiji la Dodoma kimeoza

wangwafi

Senior Member
Joined
May 21, 2020
Posts
141
Reaction score
70
Inasikitisha sana kitengo hiki watu wanajifanya miungu watu na hawawezi kuguswa na mtu yeyeote, sasa Mheshimiwa Rais tunakuomba sana sie wakazi wa Dodoma jiji utusaidie sana maana watu wanaporwa ardhi na kuwapa madalali wauze na hivyo kuwafanya wananchi kujisikia kuwa serikali yao haiwajali.

Tunakuomba utume watu utashangaa misururu ya watu kwa ajili ya kuonana na Mkuu wa kitengo ili kutaka kuondoa kero zao lakini hakuna mafanikio yoyote yale wanayotatuliwa.

Tunakuomba Mheshimiwa mtetezi wa wanyonge ingilia kati wananchi wako tunateseka sana na hawa wanaojimilikisha ofisi za umma kwa ajili ya kupora na kujilimbikizia viwanja vya wananchi wako wanyonge.

Tuliambiwa kuwa hata vibali vya kujenga vitachukua siku saba lakini kuna watu hapa wametembea kuja jiji zaidi ya miezi mitatu na hakuna walilofanikiwa, tafadhali sana wamulikwe na kushughukikiwa haswa.
 
Kama wengi wao ndio waliokua kwenye ile kampuni ambayo JPM aliifyekelea mbali ya CDA unategemea nini, kilichotakiwa ni kusafisha kabisa na kuajiri vijana wapya kutoka vyuoni na sio kutumia hao makapi ambao walizoea rushwa na kufanya maisha ya wananchi wa kawaida kuwa magumu.
 
Tena hasa yule Kamishna alie hamishiwa Dodoma kutoka Dar ... anaitwa Methew bwana yule anashirikiana na matapeli kupiga watu ama hakika ni uozo wenye kunuka
 
Ili lalamiko naona Lina mashiko CDA Ilivunjwa kutokana na ukilitimba wao ila hapo dodoma CDA imelundi pitia mlango wa nyuma ,kupitia hasa hayo makampuni yalioingia mikataba na jiji kupima viwanja,bahadhi ya makampuni KWA kushirikiana na madiwani wa kata za pembeni wamekua waporaji wa ardhi za wananchi mfano hapo CHAHWA Yani wanapima na kulazimisha chukua viwanja KWA kufidia gharama za upimaji why wasipime viwanja then wamkabidhi mpimiwa ili yeye afanye mahamuzi ya kulipia viwanja vyake au kuuza mwenyewe ili awalipe gharama zao,ila wao hulazimisha kuchukua viwanja.

Na taratibu zipo wazi kwamba kupima ,inabidi makampuni yashindane ili wananchi waridhie kampuni ambayo wanaona inafaa ,ila Hali sivyo ilivyo, kampuni zimekua zikipenyezwa katika sehem husika bila Hata wananchi kushirikishwa.

That's diwani aliekuepo kabla ya uchaguzi sijui Kama ndo yeye bado alikua anajitapa kuwa tajiri mkubwa hapo CHAHWA kupitia dhuruma za ardhi za wananchi
 
Hawa jamaa wamejitahidi sana japo wapenda fursa hawatakosekana. Nenda sasa kama una pesa Dodoma utapata kiwanja kilichopimwa bila mawaa. Wenye malalamiko ya kweli nafikiri ni wakazi wa asili ambao maeneo yao yanarasimishwa tena mengi kwa kutumia makampuni binafsi.
 
kuna wale dodoma jiji upande wa ardhi wanaohusika na kuidhinisha hati baada ya kuwa imepitishwa jiji (zamani CDA)...ni wasumbufu hatari, wanalazimisha sana mazingira ya kupewa rushwa.

mie waliniomba eti angalau laki moja ili hati yangu (HALALI) itoke haraka, miezi hii ilivyo tait nikawajibu we acha tu nitafa tatilia taratibu taratibu hata kama ni mpaka january mwakani!.
 
kuna wale dodoma jiji upande wa ardhi wanaohusika na kuidhinisha hati baada ya kuwa imepitishwa jiji (zamani CDA)...ni wasumbufu hatari, wanalazimisha sana mazingira ya kupewa rushwa.

mie waliniomba eti angalau laki moja ili hati yangu (HALALI) itoke haraka, miezi hii ilivyo tait nikawajibu we acha tu nitafa tatilia taratibu taratibu hata kama ni mpaka january mwakani!.
Usilalamike sasa tulia
 
Hii haikubaliki hata TAKUKURU waanze hata leo kufanyia kazi jambo hili.
 
Ni kweli Mkuu kama tabu ya huku Nzuguni tunavumilia nilichoamua kujijengea namsubilia huyo wa kuvunja,au kuroga mtu kwake na familia hasa yule Dada anayesumbua watu pale Nzuguni jina lake linaanzia na O aangalie sana,na hata huo mkurugenzi nae ni jipu tu.
 
Kuna maofisa hapo ni mabilionea kwa kuuza viwanja, kuna jamaa anaitwa somebody Kawinga ana kampuni yake ya upimaji achana naye anapiga hela hatari
 
Back
Top Bottom