Kitenge na ushabiki wa yanga

kama ningekuwa mtangazaji nisingekuwa nasema YANGA akifungwa natangaza magoli ya kufungwa kwa simba tu. UNAZI MUHIMU NA NAICHUKIA SANA SIMBA NATAMANI INGESHUKA DARAJA HATA LEO NA IPOTEE KABISA.

:smile-big::smile-big::smile-big::smile-big::smile-big:
 

Sasa kwatanzania hata mshabiki wa netball anamapenzi ya hizi team hizi mbili,sijaona shabiki wa kagera sugar ,mbeya city,wala Toto Africans,kwa hilo itakuwa ngumu ndomana mara nyingi TBC mechi kama ya jpili huwaweka watangazaji wasimba na Yanga
 

Cheki kumbukumbu zako vizuri, Mkuu! Juma Nkamia ni Simba na nadhani aliwahi kuwa mshikapembe (Katibu Mwenezi) wa hako katimu!
 
Cheki kumbukumbu zako vizuri, Mkuu! Juma Nkamia ni Simba na nadhani aliwahi kuwa mshikapembe (Katibu Mwenezi) wa hako katimu!

Hapa nilitaka kumuelekeza mtoa mada kuhusu unazi wa watangazaji wa soka,zahiri shahiri nalijua yakuwa Nkamia nikati ya wanazi namba moja wa Simba,nakumbuka kuna mechi moja alisha wahi kuwa tukana sana wachezaji wa Yanga n kumlau,u refa kwanini hatoi card eti wanacheza rafu zisizo na maana,niliumia sana wakati hiyo mechi nili kuwa naishuhudia live na mpira ulikuwa uleule rafu za yanga ndo zilezile za Simba(mmpira wa kukamiana)
 
Ushabiki tu upungue kwa watangazaji maana pale yupo kazini na hajatumwa kwenda kushabikia timu anayopenda au kuponda timu asiyoipenda. Mimi hilo tu.
 
Ethics za Journalism hawazifuati na Wanakubali Hisia Ziwazidi Uwezo na hatimaye Wanashindwa Kuzificha ila Je lini Umegundua Kama Charles Hillary ni Arsenal Damu na wa Kutupwa? Na Ni nani Asiyejua Kuwa Sali Kikeke ni Mau United Damu? Jaribu Kuwafuatilia haswa Wakiwa Wanatangaza Hiyo Mipira Kamwe Hutogundua Kuwa Wana Timu Zao Wanazozishabikia. Hapa Bongo Waandishi Wanaishi Kwa Mazoea na Wengi pia Wanaajiriwa Kwa Magumashi na Uroda na Je Unategemea Nini Hapo? Kaka Vyuoni Kuna Majanga na Elimu Ya Tanzania bado ipo ktk Content( Knowledge ) based Wakati Vyuo Karibia Vyote Vilivyopo Ulaya Vingi ni Vya Competency based na Nadhani Utaona ni Jinsi gani Wazungu Walivyo na Fikra Endelevu na Wanavyofanikiwa.
 

Umefunguka sana tu mkuu
 
... SIMBA NATAMANI INGESHUKA DARAJA HATA LEO NA IPOTEE KABISA.
Mkuu, yaani mechi ya juzi imekufanya uichukie Simba kiasi hicho? Hapo katika kushuka daraja, nadhani utakuwa unaiogopa Simba, sio kwamba eti unaichukia tu
 
Haya yote ukimueleza mtu kama Ma Ulidi, bado hatakuelewa kwani hata upeo pia unahusika!
 
kama ningekuwa mtangazaji nisingekuwa nasema YANGA akifungwa natangaza magoli ya kufungwa kwa simba tu. UNAZI MUHIMU NA NAICHUKIA SANA SIMBA NATAMANI INGESHUKA DARAJA HATA LEO NA IPOTEE KABISA.
Mkuu huna haja ya kuichukia simba namna hiyo, sisi washabiki wa simba tunaipenda yanga sana tu kwa maana tunauwezo wa kuwafunga au kurudisha magoli mliyotufunga jinsi tunavyopenda..
 
Mkuu, yaani mechi ya juzi imekufanya uichukie Simba kiasi hicho? Hapo katika kushuka daraja, nadhani utakuwa unaiogopa Simba, sio kwamba eti unaichukia tu

sijawahi ipenda simba toka nimezaliwa mkuu
 
Mkuu huna haja ya kuichukia simba namna hiyo, sisi washabiki wa simba tunaipenda yanga sana tu kwa maana tunauwezo wa kuwafunga au kurudisha magoli mliyotufunga jinsi tunavyopenda..
mi siipendi simba hata rangi zake za bendera
 
Mnawalaumu bure tu hawa. Hivi Mmeshafanya Fanya Utafiti mdogo tu ktk Vyuo vyao tena Maarufu vya hapa Jijini? Kama tu Wakuu wao wa hivyo Vyuo hawako Serious na Muda wote Ukiwakuta Ofisini Mwao Wapo tu Facebook, Hawapo Creative, hawana Vision na Siyo Innovative Je Unategeme Walimu wa hivyo Vyuo Watakuwaje? Wavulana Wanahonga Pesa ili Kupata Vyeti na Dada Zetu ndiyo Usiseme Wanaliwa na Hao Wakuu na Mpaka Walimu Kisha Wanapewa Marks za Bwerere, Je hapo Mnategemea Nini? Tunahitaji tuwe na Bodi Maalum Ya Kuzingatia Vigezo na Sifa za Mwandishi wa Habari bora Kama ilivyo Kwa Wenzetu Wahasibu na Bodi Yao, Wanasheria na Shule Yao Ya Sheria na Uwakili na Makandarasi na Wahandisi na bodi zao za ERB na CRB. Bila hivyo Mtazidi tu Kuwalaumu akina Kitenge na Wengineo ila Ugonjwa Mkubwa Unaanzia ktk Vyuo vyao na Haswa vya Ilala Shariff Shamba na Sishangai hata Baraza Lao la Habari Tanzania MCT hivi Majuzi tu Limevipa Onyo Vyuo hivyo Kutokana na Kutokidhi Vigezo Kuanzia Kwa Walimu hadi Vifaa au Vitendea Kazi.
 
mi siipendi simba hata rangi zake za bendera

huipendi simba kama team...au hupendi rangi za jezi ya simba?...kwa hiyo hta yanga wakibadili rangi wakatumia nyekundu nao utakuwa huwapendi?

Kumbuka..hakuna yanga bila uwepo wa simba....na hakuna man u bila uwepo wa liverpool..na hakuna real madrid bila uwepo wa barcelona....unaipenda yanga kwa sababu huipendi simba..isingekuwapo simba usingeipenda yanga.
 

Nakuunga mkono kwa 100%. Nilikuwa chuo nikawa napiga story na dada mmoja aliyekuwa anasoma masomo hayo ( journalism) aliniambia darasan kwao paper likiwaona wanaomba majibu kwa Lecturers wao. tukawa tunashangaana sisi kubanwa kwa sana na wao kwa kuachiwa kwa sana.
 

Nakuunga mkono kwa 100%. Nilikuwa chuo nikawa napiga story na dada mmoja aliyekuwa anasoma masomo hayo ( journalism) aliniambia darasan kwao paper likiwaona wanaomba majibu kwa Lecturers wao. tukawa tunashangaana sisi kubanwa kwa sana na wao kwa kuachiwa kwa sana.
 
mi siipendi simba hata rangi zake za bendera

Ndio maana hata elfu kumi huzipendi!Maskini pole sana!Sijui ungeipendaje Yanga bila kuwepo Simba?Mi siipendi Yanga kweli kweli hata icheze na shetani tamshabikia shetani kuliko shabikia timu ya magazetini,ila rangi zake ziwezi kuzikwepa!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…