Kitendo cha wewe kuiangalia electron kinaibadilisha tabia

Kitendo cha wewe kuiangalia electron kinaibadilisha tabia

P h a r a o h

JF-Expert Member
Joined
Mar 25, 2024
Posts
993
Reaction score
1,882
‎ilikunaaminika na pia ni obvious kabisa kwamba mwanga ni wave. Einstein akasema tusahau kama mwanga ni wave na tufikirie kama ni particle.
‎electron ambayo inafahamika ni particle tukaja kuikuta ni wave pia.

‎experiment ilifanyika hivi: kuna ukuta umetobolewa matundu mawili. upande mmoja wa ukuta kumewekwa screen, upande mwingine wa ukuta tupo sisi.
‎tuna rusha electon ambapo zitapita kwenye yale matundu mawili, zitaenda kugonga kwenye screen alafu screen ndo itatuonyesha zilipita kwenye tundu lipi.


‎sasa baada ya kuachilia electron za kutosha, screen inaonyesha hivi 👇🏾

buildup-interference-pattern-individual-particle-260nw-2215154071.jpg


‎hii parten inatengenezwa na kitu chenye sifa ya wimbi, wakati zinapita kwenye matundu mawili zina interfere inatengeneza trough na crest kwaiyo ukiona hii parten, jua umeona wave.

‎Sasa hapa ndo mwanzo ambao tutaanza kuona jinsi elecron inavyotuacha mdomo wazi...

‎tunarudia experiment lakini sasa hatupitishi elecron nyingi kwa pamoja tunapitisha electron moja baada ya nyingine.

‎matokeo yake yakawa hivi: kwenye screen inaonekana zinatua randomly lakini baada ya kua nyingi inaonekana zimetengeneza tena ile parten ya interference ya wave ( je zilikua zina interfere na nani wakati tulipitisha moja moja )

screen inaonyesha hivi angalia kianzia a,b,c na d 👇🏾

electron-interference.jpg


‎sasa tunarudia experiment lakini tunaweka kifaa kichunguze yale matundu ili tujue electron imepita kwenye tundu lipi hasa kwanini itoe wave parten?.

‎matokeo yake inaonyesha kabisa imepita kwenye tundu fulani na sasa screen inaonyesha hivi 👇🏾

40610f11-acac-4418-b8f5-e8d448602f73.png


‎hii ni pattern ya particle

‎cha kushangaza ni kwamba tukiichunguza kwanama yoyote imepita wapi ? inakua Particle.
‎ila tukiipitisha bila kuchunguza ? inakuwa wave.

‎hii experiment imerudiwa mara nyingi sana na matokeo yake ndio haya haya, ukicha ipite kwenye screen bila kuiangalia inakua wave, ila ukiangalia imepita wapi inapita kawaida na inakuwa particle.


‎pia kuhusu mwanga experiment iliyo kuja kubadilisha mtazamo ilikua hivi:
‎wengi tunajua ile ukusugua kitu cha plastiki kwenye nywele kinapata charge na kinakua kinaweza kuvuta kitu kingine kama karatasi,

‎sasa kwenye hii experiment kitu kinawekewa electrostatic charge ili kipate nguvu ya kunata sehemu

‎tunachukua tochi yenye mwanga mwekundu na kumulika kwenye hichokitu, matokeo yake hamna kitu kinatokea,
‎tunaongeza mwanga mwekundu uwe mkali sana.... pia bado hamna kinachotokea.
‎Sasa tunachukua tochi yenye mwanga wa blue kumulika, kilekitu kitapoteza charge na kuanguka chini.

‎hiyo ndo iliitwa photoelectric effect. kwanini mwanga mwekundu hata ukiwa mkali kiasi gani hauna effect ila mwanga wa blue hata kidogo una leta effect ?

‎aliyekuja kuielezea hii ni Einstein ndo kitu kilichompa tuzo ya nobel. Einstein akasema tusahau kama mwanga ni wave bali tujue kua ni particle na umeundwa na particle ndogo kwaiyo mwanga mwenkundu ambao una infrared nyingi particle zake ni nyepesi ila mwanga wa bluu ambao una ultraviolet nyingi particle zake ni nzito na zinauwezo wa kugonga na kuziondoa zile charge ndo maana tulivomulika kwa mwanga wa blue charge ziliondoka
 
aliyekuja kuielezea hii ni Einstein ndo kitu kilichompa tuzo ya nobel. Einstein akasema tusahau kama mwanga ni wave bali tujue kua ni particle na umeundwa na particle ndogo kwaiyo mwanga mwenkundu ambao una infrared nyingi particle zake ni nyepesi ila mwanga wa bluu ambao una ultraviolet nyingi particle zake ni nzito na zinauwezo wa kugonga na kuziondoa zile charge ndo maana tulivomulika kwa mwanga wa blue charge ziliondoka
Kuzungumzia photoelectric effect bila kuzungumzia concept za threshold frequency na intensity of radiation ni kuinajisi physics.

Pia photon ni massless sasa unaposema mwanga wa blue una particles nzito huo uzito ni upi?
 
Back
Top Bottom