Kitendo cha RC Anthony Mtaka kubatilisha maagizo ya DC Bariadi si cha kawaida

Nilikuwa namheshimu sana kwa uungwana wake,japo nilishangazwa kuvamiwa na silaha kama majambazi kina mama wa Chadema mchana kweupe katika ukumbi mjini Bariadi. Yeye kama mwenyekiti wa ulinzi na usalama mkoa alipaswa kuzuia upumbafu ule

Na hili kama ni kweli lilitokea na yeye akijua au ndie aliyeagiza iwe hivyo litatushangaza wengi tuliokuwa tunamtazama kwa matumaini.
Tafadhali, wenye ufahamu mzuri na taarifa hii ya "akina mama wa CHADEMA kuvamiwa" kwa maagizo ya Mkuu wa Mkoa huyu, tafadhali iwekeni ijadiliwe.
Kama hili alilifanya kwa sababu za kiushabiki tu wa kisiasa, heshima kubwa niliyomwekea huyu mkuu nitaiondoa. Ni mmoja wa watu wachache walioko huko CCM ninaoendelea kuwapa heshima kwa misimamo yao thabiti na kwa matendo yao.

Natarajia taarifa hiyo sio ya kweli, na kama akina mama walifanyiwa hivyo, pengine palikuwepo na sababu maalum.

Hii ndio maana tunawahimiza akina CHADEMA kuwa wanaweka kumbukumbu zao za matukio ya unyanyasaji kama haya vizuri ili inapotakiwa ushahidi uwepo bila ya upindishaji wowote.
 
N
Huwa nagombana na Moderator ambaye anajivika jukumu la kubadilisha heading pasipo kuwasiliana nami nikamwelewesha maana najua anakuwa hajaelewa.na simlaumu kwa kutokuelewa.alipaswa aniulize na si kubadilisha heading yangu.

Huyu Mh. Anthony Mtaka ni nani? Nina Mashaka na Uraia wake. Si Mtanzania.

Nimekuwa mara nyingi sana nikijiuliza kuhusiana na Mkuu wa Mkoa huyu. Nimegundua anaweza kuwa Mtanganyika au Raia wa nchi fulani.

Nimeshangaa inakuaje mtu wa aina yake anapewa nafasi muhimu kama hiyo ya Ukuu wa Mkoa? Mambo anayoyafanya Mheshimiwa Anthony Mtaka si ya Raia wa nchi yetu.

Nmeshtuka na kitendo chake cha kutokubaliana na maamuzi sahihi ya mkuu wa wilaya aliyesema kuwa wafanyakazi wakachangie Mashine iliyoibwa Hospital. Mbona haya ndo yalikuwa maamuzi sahihi ya watanzania waliopewa madaraka wa nchi hii?

Hawa wafanyakazi walishindwa nini kuwekeana zamu ya kulinda hiyo mashine?walishindwa nini muda wote kuwa wameizingira kuhakikisha haiibwi?kwanini hawakusitisha kazi nyingine na kukaa wakilinda hiyo mashine ya Ultra Sound?

Walipe tu kama alivyotokwa na maneno DC.nani anakuja kusema HAKATWI MTU HAPA? huu siyo uzalendo.tungeanzia hapo halafu turudi nyuma na zile pesa zetu zote zilizopigwa na wahuni mbalimbali nazo zichanqwe zirudishwe.

Naomba mheshimiwa Rais amwangalie Anthony Mtaka inawezekana si Raia wa Tanzania au basi anatumika na Mabeberu au Wapinzani. Tabia anazoonesha si za mbuzi jike hata kidogo.ni za kibeberu.

Huyu Mkuu wa Mkoa anapata wapi muda wa kutumia akili katika maamuzi yake?anapata wapi?anawezaje kufikiri kabla ya kunena au kutenda?maana yake hayupo busy kama wenzie ambao tunaona maamuzi yao. Huyu atenguliwe.hana sifa za Mwana CCM wa miaka hii.

Serikali chunguzeni uraia wa vizazi vyake hata vitano nyuma. Huyu hawezi kuwa Mtanzania, Hawezi kuwa Mwana CCM. Msije sema sikusema.
Napendekeza huyu RC awe mgombea urahisi mwaka 2020 kupitia CCM ili nchi yote ineemeke kwa akili na moyo wake mzuri.
 
Nilikuwa namheshimu sana kwa uungwana wake,japo nilishangazwa kuvamiwa na silaha kama majambazi kina mama wa Chadema mchana kweupe katika ukumbi mjini Bariadi. Yeye kama mwenyekiti wa ulinzi na usalama mkoa alipaswa kuzuia upumbafu ule.
Majambazi utayalindaje yakiwa yanaimba pipooooooos pawa
 
Kati ya watu vilaza ni wewe yaani unaweza toka kazini ukakuta remote haionekani ukaanza kupiga familia nzima.Hiyo ni roho ya unyanyasaji na uvivu wa kufikiri ambao umewazunguka vijana wa Lumumba
 
2020 wanadamu wa kweli watakaa pamoja na wale waliokuwa na matonge mdomoni wakidhania kula yao ni permanent watajuana
 
Antony Mtaka ni mtenda haki, Mkoa wa Dodoma, umebarikiwa sana, utatendewa haki. Na kwa vile Dodoma ndio makao makuu ya nchi, then, kuutendea haki mkoa wa Dodoma ni kuitendea haki nchi ya Tanzania na itabarikiwa, hongera sana Antony Mtaka kuwa RC wa Dodoma. Asante Rais Mama Samia, umeutendea haki uteuzi huu, umeutendea haki mkoa wa Dodoma, na umemtendea haki Antony Mtaka.

P
 
Antony Mtaka ni mtenda haki, Mkoa wa Dodoma, umebarikiwa sana, utatendewa haki. Na kwa vile Dodoma ndio makao makuu ya nchi, then, kuutendea haki mkoa wa Dodoma ni kuitendea haki nchi ya Tanzania na itabarikiwa, hongera sana Antony Mtaka kuwa RC wa Dodoma. Asante Rais Mama Samia, umeutendea haki uteuzi huu, umeutendea haki mkoa wa Dodoma, na umemtendea haki Antony Mtaka.

P
Nimefurahi kukuona hapa tena kaka
 
Back
Top Bottom