Kitendo cha RC Anthony Mtaka kubatilisha maagizo ya DC Bariadi si cha kawaida

GuDume

JF-Expert Member
Jan 18, 2015
6,652
14,261
Huwa nagombana na Moderator ambaye anajivika jukumu la kubadilisha heading pasipo kuwasiliana nami nikamwelewesha maana najua anakuwa hajaelewa.na simlaumu kwa kutokuelewa.alipaswa aniulize na si kubadilisha heading yangu.

Huyu Mh. Anthony Mtaka ni nani? Nina Mashaka na Uraia wake. Si Mtanzania.

Nimekuwa mara nyingi sana nikijiuliza kuhusiana na Mkuu wa Mkoa huyu. Nimegundua anaweza kuwa Mtanganyika au Raia wa nchi fulani.

Nimeshangaa inakuaje mtu wa aina yake anapewa nafasi muhimu kama hiyo ya Ukuu wa Mkoa? Mambo anayoyafanya Mheshimiwa Anthony Mtaka si ya Raia wa nchi yetu.

Nmeshtuka na kitendo chake cha kutokubaliana na maamuzi sahihi ya mkuu wa wilaya aliyesema kuwa wafanyakazi wakachangie Mashine iliyoibwa Hospital. Mbona haya ndo yalikuwa maamuzi sahihi ya watanzania waliopewa madaraka wa nchi hii?

Hawa wafanyakazi walishindwa nini kuwekeana zamu ya kulinda hiyo mashine?walishindwa nini muda wote kuwa wameizingira kuhakikisha haiibwi?kwanini hawakusitisha kazi nyingine na kukaa wakilinda hiyo mashine ya Ultra Sound?

Walipe tu kama alivyotokwa na maneno DC.nani anakuja kusema HAKATWI MTU HAPA? huu siyo uzalendo.tungeanzia hapo halafu turudi nyuma na zile pesa zetu zote zilizopigwa na wahuni mbalimbali nazo zichanqwe zirudishwe.

Naomba mheshimiwa Rais amwangalie Anthony Mtaka inawezekana si Raia wa Tanzania au basi anatumika na Mabeberu au Wapinzani. Tabia anazoonesha si za mbuzi jike hata kidogo.ni za kibeberu.

Huyu Mkuu wa Mkoa anapata wapi muda wa kutumia akili katika maamuzi yake?anapata wapi?anawezaje kufikiri kabla ya kunena au kutenda?maana yake hayupo busy kama wenzie ambao tunaona maamuzi yao. Huyu atenguliwe.hana sifa za Mwana CCM wa miaka hii.

Serikali chunguzeni uraia wa vizazi vyake hata vitano nyuma. Huyu hawezi kuwa Mtanzania, Hawezi kuwa Mwana CCM. Msije sema sikusema.
 
Huyo Mkuu wa mkoa ndiye mzalendo namba one kati ya wakuu wa mikoa wote nchini

Hivi umewahi ona wapi wafanyakazi wote wa hospitali wakatwe mishahara yao kutokana na ultrasound iliyoibiwa??

Hivi kwanini vyombo vya usalama havijachunguza tukio zima na kubaini "kibaka" huyo aliyeiba hiyo ultrasound??
 
Hata yule Evaristo Ndikilo wa Pwani na Martin Shigela wa Tanga nao nina shaka na uraia wao! Haiwezekani waonekane kwenye masuala yahusuyo maendeleo tu, mfano kwenye uzinduzi wa viwanda, bomba la mafuta, nk! Yaani wanashindwa kabisa kutengeneza hata kiki moja tu kama wenzao akina Makonda, Mwanri, Hapi, Chalamila, n.k ili kumfurahisha mkuu?
 
GuDume, ukiangalia sinema ya animation ya The Lion King, baada ya kifo cha King Mufasa, Scar akaichukua Nchi ya Pride Rock akiwa anasaidiwa na Mafisi watatu, mmoja wao akiitwa Shenzi.
Himaya ya Simba ikaingiliwa na Utawala wa mafisi.
Mafisi wakaharibu Nchi, njaa na dhidi vikaikumba Nchi.
Hata sisi tunatawaliwa na wageni ndio Maana hali ni mbaya, wana kopa mikopo mikubwa yenye riba kubwa ili waonekane wanajenga Nchi kumbe wanaiingiza Nchi kwenye zigo kubwa la madeni yasiyolipika huko siku za usoni.
Wanahubiri habari za viwanda, mazingira yanawafukuza wawwkezaji.
 
Mh.Antony Mtaka ni Mwananchi mzalendo,mwelevu,mchapakazi na uadilifu wake ni wa kutukuka.
Ikimpendeza Mh.Rais JPM ampangie majukumu mengine ya ili Watanzania wengine wapime uadilifu na mchapakazi wake.
Ndiye Mkuu wa Mkoa anayafanza kazi zake 24/7 na watendaji wake bila kuchoka,kama ni kulala basi hulala masaa 3-4.
 
Back
Top Bottom