Kitendawili cha Mtandao wa OTEAS

Mwijumbe

Member
Mar 22, 2016
15
71
Tamisemi Mmetangaza kazi za ualimu ambapo mwisho wa maombi ni Tarehe 15 March 2019 na waombaji ni lazima waombe kupitia mfumo wa internete wakati mnajua fika kwamba: 1) Mfumo wenu ni dhaifu sana haufunguki kabisa 2) Kwa udhaifu wa Mfumo wenu wa internete hivi kijana alioko wilayani anaweza kuomba? au ni njia mojawapo ya kuhakikisha wanyonge hawaombi ili muweke ndugu zenu?

Waziri wa tamisemi tafadhali saidia vijana wanyonge na hii dhaluma, hii inafanyika kwa makusudi kabisa.
 
Kwa walio vijijini kwa kweli ni pasua kichwa, au hata mikoa ambayo miundombinu ya internet ni hafifu kwa kweli itakuwa ngumu. Hata hivyo mfumo ni kwamba unafunguka ukiwa kwenye internet nzuri na kwa watu ambao internet ni ya kusuasua ndo ngumu kufungua OTEAS. Na wahusika naamin wamesikia hilo kusaidia vijana ambao wapo katika mazingira hayo ya kukosa internet nzuri
 
Jaribu kwa sasa mtandao uko vizuri kabisa, baada ya malalamiko ya mwanzoni wameuboresha kwa kiasi kikubwa sana. Kumbuka kwamba mwisho ni kesho.
 
Back
Top Bottom