ni dalili hajafikishwa anapokwenda
atakuwa anaenda wapi vile? Lol
AshaDii kama ulikuwa kwenye mawazo yangu
hapo hakuna upendo hicho anachosingizia eti anamyima raha ya kupumua vyema eti anambana bana ni kujitetea ambako hakuna lolote
mafundisho ya ndoa ni ya muhimu sana aise maana kwa mwelekeo huu mume analalamika hataki kukumbatiwa au ahisi jote wala ukaribu wa mke ni issue
Mapenzi mchezo wa ajabu saana, tena ni mbaya ukiuchukulia kama mcheza kamali... Kutokuwepo upendo juu ya mkewe kumemfanya asione "UPENDO WA DHATI" wa mke ila kuona kero ambayo anapta tokana na yale ambayo hataki kufanyiwa.
Mie nawasihi sana kaka/baba zangu, kwa kiasi kikubwa nyumba na familia inajengwa na mke... Kama mke wako ana upendo wa dhati juu yako lakini akawa na madhaifu kama uvivu, kutojua kupika na the like; MWESHIMU sana huyo mwanamke... La sivyo utatumbukia mahala ambapo siyo kabisaaa! Ukawa na mwanamke bala wewe ukiwa kama kisima cha kumfikisha pale anapotaka na kile atakacho...
Bahati mbaya saana huwezi fukuza upepo, kama hupendi, hupendi... BUT walau mtu akikupenda heshimu hayo 'Mapenzi' anayokupa.
AshaDii ndo maana huwa nikikukosa humu jamvini napata shida sana (mhhh usifikirie vingine)
hakuna kitu kibaya kama unakaa na mtu unajua kuwa humpendi na mapenzi yameshuka ila humwambii na unamuona kero anapokuwa na wewe
Huna mapenzi naye wala humfeel ila kumwambia inakuwa ngumu
Huyo mtu ambaye unamsema kuwa akikukaribia unahisi kero ni mkeo sio mtu baki
Huyo mtu ambaye anajaribu kukuonyesha upendo na kukukumbatia may be anakupa asante kwa ulichomfanyia au kukuonyesha kuwa wewe ni ubavu wake then badala ya kurudisha upendo huo unamgeuzia mgongo na kumuona ni kero ipo siku utalitafuta hilo kumbatio ulikose
Au utamfanya aende mahali ambapo atakumbatiwa usiku mzima
Hebu geuka muonyeshe upendo kama anaokupa wewe tena kwa kumkumbatia hata kama ni usiku mzima kama kumbikumbi ni sawa kwake