kadoda11
JF-Expert Member
- Jan 6, 2011
- 21,453
- 20,755
Kitambulisho cha Taifa(Citizen Identity Card).
Nina wiki kama mbili tangu nikabidhiwe.Ambapo sasa ID hiyo sambamba na zingine,natembea nayo 24/7 kwa majivuno na kwa kujiamini kwenye Wallet yangu.
Kuna bandiko hapa Jf mwana-Diaspora mmoja anadai Kitambulisho cha Taifa hakina umuhumu wowote,kwamba hati ya kusafiria(Passport) inatosha kutambulisha Utaifa wake.Je ni kweli Vitambulisho vya Taifa havina umuhimu wowote?,au ni maneno ya mkosaji aliyeukana utanzania na kuzamia huko ughaibuni. Wakuu tupeane uzoefu kuhusu hili.
lawmaina78 tunajua huko ''kwenu'' hii kitu ''muko nayo'' miaka ''mingi''.embu mutupee uzoefu ''yenu'' tafadhari,ukizingatia kwamba kwa hapo nairobi unapo kutana tu na Karao(Askari),iwe Mchana ama Usiku,kauli ya kwanza ni ''embu onyesha sisi ID yako".
sitashangaa karao wa TZ watakapo geuza kosa la kutotembea/kutokuwa na national ID,mradi wa kuwapatia pesa ya bia na nyama choma. Time will tell. LOL
Najua kwa East Africa na kwa Tanzania bara tumechelewa kupata national ID,ila si vibaya tukajadili.
CC Nyugunyugu wa mama Matola Hute Mtimti et al
Nawasilisha.
NB:Wakuu samahani kwa ubora duni wa picha,nimetumia simu ya kichina.