Wick
JF-Expert Member
- Dec 19, 2012
- 8,313
- 12,124
Nchi gani hizo mkuu?...Japan na China usiziweke kwenye mfano wako lakini!!..Kuna baadhi ya nchi Duniani hapa ukiwa na kitambi sahau kupata mchuchu. Ukiwa na kitambi unaonekana mjinga mbele ya jamii, mpenda kubukanya (kula hovyo) na usiejali afya yako.
Tena afadhali Kitambi hicho uwe nacho mgeni walau wataogopa au watakunyooshea vidole kwa siri, ukiwa mwananchi ndio una kitambi utaishi kwa tabu sana, ukiumwa hata kidonda cha mguuni ukienda hospital tegemea kuchanwa ukimkuta doctor aliyepinda, kuwa kwanini umeuachia mwili mpaka uwe hivyo.
Kuna baadhi ya nchi watu wanene hasa uliotokana na kula kula wanaishi kwa shida sana mbele ya jamii zao.
Wanaposema tupo nyuma tupo nyuma kweli, kwetu jambo la kawaida kumkuta Daktari na kitambi, huku ughaibuni unaweza kutembea hospital zote mpaka miguu kutokea mabegani usimkute daktari wa namna hiyo.
Zamani kabla sijaja kuelimika huku nilikuwa naona kitambi mswano tu, nilipokuja huku na kuelimishwa madhara yake, nikajiona mjinga, hivi sasa hata iweje siwezi kukiruhusu kwenye mwili wangu.