Kitambi: Ugonjwa pekee wenye heshima katika jamii za kiafrika

Kuna baadhi ya nchi Duniani hapa ukiwa na kitambi sahau kupata mchuchu. Ukiwa na kitambi unaonekana mjinga mbele ya jamii, mpenda kubukanya (kula hovyo) na usiejali afya yako.
Tena afadhali Kitambi hicho uwe nacho mgeni walau wataogopa au watakunyooshea vidole kwa siri, ukiwa mwananchi ndio una kitambi utaishi kwa tabu sana, ukiumwa hata kidonda cha mguuni ukienda hospital tegemea kuchanwa ukimkuta doctor aliyepinda, kuwa kwanini umeuachia mwili mpaka uwe hivyo.
Kuna baadhi ya nchi watu wanene hasa uliotokana na kula kula wanaishi kwa shida sana mbele ya jamii zao.
Wanaposema tupo nyuma tupo nyuma kweli, kwetu jambo la kawaida kumkuta Daktari na kitambi, huku ughaibuni unaweza kutembea hospital zote mpaka miguu kutokea mabegani usimkute daktari wa namna hiyo.
Zamani kabla sijaja kuelimika huku nilikuwa naona kitambi mswano tu, nilipokuja huku na kuelimishwa madhara yake, nikajiona mjinga, hivi sasa hata iweje siwezi kukiruhusu kwenye mwili wangu.
Nchi gani hizo mkuu?...Japan na China usiziweke kwenye mfano wako lakini!!..
 
Ninavyohangaika kukitoa kitambi,laiti ningekuwa na uwezo,ningewatandika risasi wote wanaotudhihaki eti tunakula ovyo!Kuna watu wanakula ovyo mno naishi nao,lakini ni vimbau na hawana hata dalili ya unene.Kumbukeni kuna watu tumeumbwa hivyo na miili mikubwa hata ujinyime vipi!
 
Lakini heshima unayo kaka.Au unapenda kuwa hivi?
 
Attachments

  • IMG_0638.jpg
    IMG_0638.jpg
    11.3 KB · Views: 23

Similar Discussions

Back
Top Bottom