"Ndugu" ni kundi la kipekee sana na very confusing katika jamii za Kiafrika

Eli Cohen

JF-Expert Member
Jun 19, 2023
1,310
4,017
Ndugu wa Bongo ni wa kipekee sana. Naongea haya kwa maana hata nyie wadau mna ushuhuda juu ya ndugu mlio nao.

Ndugu zetu hawa ni aina ya watu ambao wanatembea na fikra ya kuwa wao ndio kiungo muhimu kwa jili yako katika maisha haijalishi ni namna gani unavyowachukulia wao au wanavyokuchukulia na pia regardless ya afya ya mahusiano mlionayo baina yenu.

Ni aina flani ya watu kutokana na umuhimu waliojijengea juu yako sasa wanajiona wao ndio washauri wakuu, wenye kushikilia hatma yako na muda mwingine watoa maamuzi wakuu wa masuala nyeti ya maisha yako.

Lakini bado hao hao ndugu wenye kutembea na hulka ya umuhimu kwako ndio wa kwanza hao hao kukuharibia muelekeo wako kwa sababu ya hila na wivu, then utapopata madhara kutokana hila na husda zao, wao wao ndio wa kwanza kukupa pole bila ya msaada wa maana then siku umekufa au mwanafamilia yako kufa ndio wa kwanza kujichanga kununua ng'ombe na mbuzi za shuguhuli ya msiba.

Na usiombe utoke katika familia yenye mali lukuki alafu ndugu wa kukuzunguka wakawa chini kimali. Yani hio familia yako ndio inakuwa point of discussion kwa kila kitu. Mtaandamwa, mtaharibia ili mpitie tabu kama wanazopitia.

Nyie tazameni visa vyingi huko jamii zenu, kwa kila kisa utakuta ndugu yule tena wa karibu ndio engineer wa mkasa mzima wa mahangaiko ya mtu fulani.

MUNGU ATULINDE DHIDI YA NDUGU HATARI.
 
Back
Top Bottom