Kitambi: Ugonjwa pekee wenye heshima katika jamii za kiafrika

banned do

JF-Expert Member
Apr 27, 2017
572
500
Pamoja na kuwa ni ugonjwa unaotokana na kuzidisha kula lakini jamii nyingi za kiafrika zimekuwa zikiutafuta kwa hali na mali ili kuweza kupata heshima kwenye jamii.Mtu mwenye ugonjwa huo hupewa kipaumbele na kuonekana bora kuliko wengine katika jamii.Wakati mwingine kitambi hutumika kama kipimo cha mafanikio ya mtu.

Watu wanaweza kukuona wa ajabu kama una mali lakini hauna ugonjwa huu ambao wakati mwingine huitwa utapiamlo au obesity.Unaweza kukosa hata mke na mambo ya muhimu kama haujabahatika kuwa na hilo gonjwa la kujaa mwili na tumbo.

Je watu hawajui kuwa kiambi ni ugonjwa au wanajitoa ufahamu?
 
Kalamzuvendi

JF-Expert Member
Sep 21, 2009
606
1,000
Kuna baadhi ya nchi Duniani hapa ukiwa na kitambi sahau kupata mchuchu. Ukiwa na kitambi unaonekana mjinga mbele ya jamii, mpenda kubukanya (kula hovyo) na usiejali afya yako.

Tena afadhali Kitambi hicho uwe nacho mgeni walau wataogopa au watakunyooshea vidole kwa siri, ukiwa mwananchi ndio una kitambi utaishi kwa tabu sana, ukiumwa hata kidonda cha mguuni ukienda hospital tegemea kuchanwa ukimkuta doctor aliyepinda, kuwa kwanini umeuachia mwili mpaka uwe hivyo.

Kuna baadhi ya nchi watu wanene hasa uliotokana na kula kula wanaishi kwa shida sana mbele ya jamii zao.

Wanaposema tupo nyuma tupo nyuma kweli, kwetu jambo la kawaida kumkuta Daktari na kitambi, huku ughaibuni unaweza kutembea hospital zote mpaka miguu kutokea mabegani usimkute daktari wa namna hiyo.

Zamani kabla sijaja kuelimika huku nilikuwa naona kitambi mswano tu, nilipokuja huku na kuelimishwa madhara yake, nikajiona mjinga, hivi sasa hata iweje siwezi kukiruhusu kwenye mwili wangu.
 
Mgodo visa

JF-Expert Member
Nov 1, 2016
3,244
2,000
Pamoja na kuwa ni ugonjwa unaotokana na kuzidisha kula lakini jamii nyingi za kiafrika zimekuwa zikiutafuta kwa hali na mali ili kuweza kupata heshima kwenye jamii.Mtu mwenye ugonjwa huo hupewa kipaumbele na kuonekana bora kuliko wengine katika jamii.Wakati mwingine kitambi hutumika kama kipimo cha mafanikio ya mtu.Watu wanaweza kukuona wa ajabu kama una mali lakini hauna ugonjwa huu ambao wakati mwingine huitwa utapiamlo au obesity.Unaweza kukosa hata mke na mambo ya muhimu kama haujabahatika kuwa na hilo gonjwa la kujaa mwili na tumbo.Je watu hawajui kuwa kiambi ni ugonjwa au wanajitoa ufahamu?
Kama ni UGONJWA basi BARA la AMERIKA na ULAYA wanaongoza kwa kuwa na WAGONJWA wengi.....

Dawa ikipatikana huko.....hata kwetu huku AFRIKA itafika....tena ianze kwa wagonjwa wa AFRIKA YA KUSINI maana nayo kuna idadi kubwa ya WAGONJWA (Wake kwa Waume)

Ila kama ni UGONJWA unao sababishwa na ziada ya CHAKULA.

Naona ni Ugonjwa wa KUJIVUNIA.
 
barafu

JF-Expert Member
Apr 28, 2013
6,676
2,000
Tena watu wakikuona na kitambi,utasikia "Bro naona mambo yako si haba,tugawane basi hizo za ATM"
Badala ya kumpa pole "mgonjwa",watu wanampongeza mgonjwa na ugonjwa wake.

Hii hali imehamia kwa wamama!!Siku hizi wadada wana vitambi mpaka unaogopa!!!Mi-bia,kitimoto,makuku ya kuloweka kwenye mafuta katika vijiwe vya chips,chips za mafuta ya Korie na transfoma nk.

Watu wanafikiri "junk foods" ndio ufahari na alama ya maisha bora
 
LUBEDE

JF-Expert Member
May 7, 2013
4,237
2,000
huo kama kweli ni ugonjwa basi ni janga la dunia nzima sio afrika tu!
 
Mgodo visa

JF-Expert Member
Nov 1, 2016
3,244
2,000
Mkuu kinapatikana vipi kitambi
Uwe na uhakika wa KULA milo mitatu HEAVY (ya Nguvu kabisa)...

Alafu ujenge TABIA ya kula "UBUGE" Vichopochopo ambavyo utahakikisha njaa kwako inakuwa ni HADITHI...

Unaisikia tu kwa WENZAKO.

Yaani kula kwako kunakuwa ni kwa kutimiza RATIBA tu.

Ukimudu hilo (maana yake linahitaji FEDHA ya ziada)

Utatuletea mrejesho...!!
 
banned do

JF-Expert Member
Apr 27, 2017
572
500
Kuna baadhi ya nchi Duniani hapa ukiwa na kitambi sahau kupata mchuchu. Ukiwa na kitambi unaonekana mjinga mbele ya jamii, mpenda kubukanya (kula hovyo) na usiejali afya yako.
Tena afadhali Kitambi hicho uwe nacho mgeni walau wataogopa au watakunyooshea vidole kwa siri, ukiwa mwananchi ndio una kitambi utaishi kwa tabu sana, ukiumwa hata kidonda cha mguuni ukienda hospital tegemea kuchanwa ukimkuta doctor aliyepinda, kuwa kwanini umeuachia mwili mpaka uwe hivyo.
Kuna baadhi ya nchi watu wanene hasa uliotokana na kula kula wanaishi kwa shida sana mbele ya jamii zao.
Wanaposema tupo nyuma tupo nyuma kweli, kwetu jambo la kawaida kumkuta Daktari na kitambi, huku ughaibuni unaweza kutembea hospital zote mpaka miguu kutokea mabegani usimkute daktari wa namna hiyo.
Zamani kabla sijaja kuelimika huku nilikuwa naona kitambi mswano tu, nilipokuja huku na kuelimishwa madhara yake, nikajiona mjinga, hivi sasa hata iweje siwezi kukiruhusu kwenye mwili wangu.
Kabisa mkuu
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom