Kitachompata Iran, kitaweka Historia

Kitachompata Iran, kitaweka Historia

Mkuu:
Ni vyema turejee ktk historia. Hivi Marekani ktk vita zote alizowahi kupigana nje ya nchi yake ni ipi aliyoshinda? (Anza na mfano wa Vietnam,Somalia nk..,).
Maaana ya kushinda ndio nn? Mfano Japanese mpaka wanapigwa nyuklia alishinda nani, libya mpaka Gaddaff anakufa alishinda nani?, Iraq mpaka anakufa Saddam kwa kunyongwa alishinda nani?, Afghanistan mpaka Osama anakufa kashinda nani?, Urussi anawekewa vikwazo vya kiuchumi mpaka uchumi wake unashindwa tanuka nani kashinda vita ya kiuchumi, China anabananishwa na Huwaei na anasanda mpaka projects 5G haijulikaniki tena nani mshindi,

Ugali Maharagwe umeharibu akili za watanzania
 
JAPAN Alishinda US Project Ya 5G pengne huijui ww 2 mkuu

kwengne kama kashnda mpka mbna vita hazikomi
 
kuwa makini na taarifa unazopitia mitandaoni na hata unazosoma kutoka kwenye vitabu, kuna alot of disinformation.

Ni sawa sawa na upotofu uliotapakaa mitandaoni kwamba machafuko yasiyoisha hapo harabuni yanasababishwa na mambo ya imani, tena ukristo na uislam.

ukifuatilia hata misingi ya wachangiaji wengi hapa jf juu ya mambo ya hapo arabia yamejikita kwenye imani zao, kitu ambacho ni upotofu mkubwa sana.

Kuhusu ugomvi ni Marais.
US na marafiki zake, hawatalala hata siku moja wamuachie mtu yeyote yule hata mzawa wa hayo mataifa yenye mafuta afikirie sawasawa. wao wanaamini kabisa kabisa yale mafuta ni yao, sababu waligundua uwepo wake wao.

Rais yeyote atakayejaribu kuweka kauzibe kwenye namna wanajifaidisha na mafuta hayo atasababisha raia wake wapoteze maisha kama atang'ang'ania madarakani.hawana ugomvi na hayo mataifa wanayatolea udenda.
Mkuu unajivuruga.
Mimi siendi huko uliko ww.
Na ninafaham nn chanzo cha machafuko hapo Arabuni.
Unapokua na chuki na mtawala wa taifa obviously kaka una chuki na taifa zima.
Kwasababu kiongozi anayetenda haki ambayo US na allies hawaipendi kwa raia wake lazima raia watakua wanampenda huyo kiongozi .
Mathalan Hassan Rouhani kwa jinsi anavyosimamia Iran wananchi wanampenda na kumuunga mkono rais wao,ikitokea US anamchukia Rouhani raia watasimama na vivyo hvyo ilivyo kwa US anachukia arab race nzima.
Ukienda tu kinyume naye anateketeza kila kitu.
 
Interests za USA Iraq nyakati hizo zilikuwa ni kuzuia expansion ya Soviet Union, wamarekani hawakuwa na interest ingine pale sababu hata mafuta tu walikuwa nayo kidogo sana.

Kumbuka baada tu ya vita na Iran ndio Sadamu alienda kushambulia Kuwait, Sadam alikwenda kuwait kujitwalia maeneo yenye mafuta sababu baada ya vita na iran uchumi wake ulikuwa umedorola sana na namna pekee aliona ya kuimarisha uchumi wake ni kupata mafuta, yanapatikana wapi harakaharaka, Kuwait, akaenda.

Na kwasababu Iraq haikuwa na umuhimu mkubwa sana wakati huo kwa marekani, ndio maana wakafurushwa vibaya sana kutoka Kuwait. hivyo kusema marekani alikuwa upande wa Iraq wakati wa vita.

Actually, kwa namna fulani kwenye vita ile marekani alikuwa anataka iraq ashindwe ili soviet union ionekane ya hovyo tu, japo alikuwa na interests zingine za kukomboa mateka wake.
Bro toka 1979 US alikua ana mpango wa regime change pale Iran,kivipi amsaidie Iran dhidi ya Iraq ??!!
 
Ukweli ndio ni kama wananchi wa Libya walivyokuwa hawapendi utawala wa Muammary Ghadaff
Nyote wawili mnajidanganya mnaropoka vilivyo.
HAKUNA RAIA WANAOPENDA SERIKALI YAO KM IRAN.NDIO MAANA USA ANAPATA WAKATI MGUMU KUIANGUSHA IRAN.KWASABABU WANANCHI WAKE WANA MSHIKAMANO.
LIBYA ILIKUA RAHISI KUWA BRAINWASH KWASABABU WALIKUA HAWAIPENDI SERIKALI YA GADDAFI,ILA KWA IRAN ONDOA HIZO FIKRA.
 
Maaana ya kushinda ndio nn? Mfano Japanese mpaka wanapigwa nyuklia alishinda nani, libya mpaka Gaddaff anakufa alishinda nani?, Iraq mpaka anakufa Saddam kwa kunyongwa alishinda nani?, Afghanistan mpaka Osama anakufa kashinda nani?, Urussi anawekewa vikwazo vya kiuchumi mpaka uchumi wake unashindwa tanuka nani kashinda vita ya kiuchumi, China anabananishwa na Huwaei na anasanda mpaka projects 5G haijulikaniki tena nani mshindi,

Ugali Maharagwe umeharibu akili za watanzania
Mkuu ebu tuliza mori.
1)Japan alikua anawapiga US vikali,yani watu walikua wanajitoa hadi muhanga wanajeshi wengi wa US navy walikua wanapukutika mpk huruma mpk majeshi yanarudi nyuma kukimbia ndani ya meli kujificha.
Ndipo US hakuwa na jinsi akaona bora apige nuclear bomb kwa raia sio wanajeshi bali raia wa Nagasaki na Hiroshima ili kuwatuliza Japan.Angelipiga wanajeshi ningelimuona mbabe ila kwa uoga kapiga raia ili serikali ili cease fire.
2)Libya kapata msaada kwa allies wake wa NATO na urahisi alopata ni kwasababu pia wananchi walishahamaki kumpindua Gaddafi.
Ila angesimama mwenyewe kingemkuta cha Somalia na Vietnam.
3)Saddam Hussein mpk kukamatwa mpwa wake ndiye aliyemsaliti la sivyo bado moto ungewaka.
4)Russia bado inaendelea kiuchumi japokuwa haiendelei kwa kasi kubwa kivile.
5)China kuhusu Huawei nadhani hukufuatilia vikwazo vya uchumi walivyowekeana US na China US alikua anaumia kumliko China na makampuni ya US yanayochukua raw materials kwaajili ya viwanda kutoka China yalishaanza kupiga kelele kuwa US iondoe vikwazo kwa China wanaumia.
Na 5G bado inawaka baba la baba wala haijapotea.

Bro toka 1979 US alikua ana mpango wa regime change pale Iran,kivipi amsaidie Iran dhidi ya Iraq ??!!
Kwani uvamizi wa Iraq ulikuwa na intention ya Regime change pale Iran?

Kuna wamarekani walikuwa wanashikiriwa mateka , na Iran ndio ilikuwa ina final say waachiwe au wasiachiwe. actually USA hakuwa hata anamsaidia Iran Vitani alikuwa ana interests zake tu sema wairan pia walikuwa na shida ya siraha, ndo maana biashara yenyewe ilikuwa ikifanyika kwa siri kubwa sana.
 
Mkuu unajivuruga.
Mimi siendi huko uliko ww.
Na ninafaham nn chanzo cha machafuko hapo Arabuni.
Unapokua na chuki na mtawala wa taifa obviously kaka una chuki na taifa zima.
Kwasababu kiongozi anayetenda haki ambayo US na allies hawaipendi kwa raia wake lazima raia watakua wanampenda huyo kiongozi .
Mathalan Hassan Rouhani kwa jinsi anavyosimamia Iran wananchi wanampenda na kumuunga mkono rais wao,ikitokea US anamchukia Rouhani raia watasimama na vivyo hvyo ilivyo kwa US anachukia arab race nzima.
Ukienda tu kinyume naye anateketeza kila kitu.
Marekani anaugomvi na Jordan? ana ugomvi na Oman? ana ugomvi na Iraq leo baada ya kuondoka Saddam? Ana ugomvi na Misri? au Yemeni amewahi kuwa na ugomvi nao? Saudi Arabia je? Au Kuwait

tusikuze mambo.
Hapo Uarabuni Marekani kwa sasa, narudia kwa sasa, ana ugomvi na Iran sababu viongozi wake wamekuwa vichwa ngumu, kabla ya mwaka 1989 Iran palikuwa kama sebureni kwa marekani, walikuwa na uswahiba mkubwa sababu walikuwa na rais hajielewielewi.

Haya mambo ya Nuclear ni uzushi tu, marekani ndio aliyewafundisha Iran mambo ya Nuclear mpaka alipoondoshwa shah, utasema marekani ana ugomvi na Taifa zima?

viongozi wa sasa wa Iran walikuwapo wakati wa utawala wa Obama, wakaingia makubaliano 2015 wingu la utulivu likashuka chini, kaja huyu kichaa you see what is happening, yaani hata kusema Taifa la Marekani linaugomvi na Taifa fulani ni uzushi pia.
 
In the Iran-Contra affair, the Reagan
administration secretly sold weapons to
Iran to effect the release of American
hostages held in Lebanon. Money from
the Iran weapons-sale then was used
to fund the Contras, a group of
guerrilla “freedom fighters” opposed to
the Marxist government of Nicaragua.
The Iran-Contra affair (article) | Khan
Academy
www.khanacademy.org
 
Mwaka 1979,mapinduzi ya iran yalimtoa shah,ambae alikuwa rais kibaraka wa marekani na nchi za magharibi,

iran ikataifisha visima vya mafuta kutoka kwa makampuni ya magharibi,wazungu hawakupenda na wakawa na kinyongo,
Iran ilipoona marekani bado anaunga mkono utawala wa shah,wanamapinduzi waliuteka ubalozi wa marekani nchini iran,
Ndani walikuwemo wamarekani 52,wakawa mateka,
wakati huo rais wa marekani alikuwa jimmy carter,
baada ya juhudi za kuitaka iran iwaachie mateka wa marekani kugoma,marekani walituma timu ya makomandoo toka katika kikosi cha GREEN BERET ili kwenda kuwaokoa mateka katika operation ilijulikana kama OPERATION EAGLE CLAW,
yaani operation makucha ya Tai,
tai kama ilivyo Twiga hapa kwetu ni nembo ya marekani,

ile operation ikafail na ilipatikana hasara kubwa sina kumbukumbu marekani walipoteza makomandoo kiasi gani
 
Baada ya operation kufail,ilibidi serikali ya marekani ianze mazungumzo na iran ili mateka waachiwe,
wakati huohuo uchaguzi wa marekani wa 1980 ulikuwa unakaribia,
tukirudi nyuma Rais Jimmy carter alikuwa kamuondoa kazini mkuregenzi wa CIA bwana George Bush na kufukuza kazi CIA operative karibu 700 katika juhudi za kulifanyia marekebisho hilo shirika baada ya scandal mbalimbali za matumizi mabaya ya madaraka,
kwa hiyo kukawa na kikundi cha wanausalama walioapa kuhakikisha jimmy carter anakuwa ni one term presdent,

kwa hiyo wakati kampeni zinaanza,Jimmy carter akajikuta anapana na Ronald Reagan wa chama cha republican,
ile timu ya maofisa usalama rogue wakawa upande wa Reagan ili kuhakikisha jimmy carter harudi madarakani
 
So bwana George Bush akawa ana spearhead mikakati ya kuhakikisha Reagan anakuwa rais wa marekani,
moja ya hiyo mikakati ilikuwa ni kuhakikisha kuwa Rais Carter asipate sifa za kisiasa kwa tukio la kuhakikisha mateka wa marekani waliokuwa wakishikiliwa iran wanaachiwa,
kwa hiyo Bush akaaongea na Ayatoolah na kumwambia ahakikishe wale mateka hawaachiwi kipindi cha kampeni ili Carter asijizolee sifa itayomwongezea kura,
kisha akina Reagan walipiga kampeni na kumlaumu Carter kwa kushindwa kuwakomboa wamarekani walioshikiliwa iran,
jimmy carter akaonekana rais dhaifu na kweli Reagan akampiga chini kwenye matokeo ya uchaguzi,

Rais Reagan akakamata usukani huku Bush akiwa makamu wa rais,
baada ya uchaguzi iran ikawaachia mateka wa marekani,

wakati huo iran na iraq ziko vitani,
kulikuwa na mateka wa marekani nchini Lebanon na marekani ilitaka waachiwe,
Reagan na bush washazoea kula deal za siri na iran,wakaongea na iran ili wamarekani walishikiliwa lebanon waachiwe,
iran ikatoa sharti kwamba marekani iwauzie silaha,
ndo chanzo cha IRAN-contra scandal,

operation ilisimamiwa na COLONEL OLIVER NORTH,
so utawala wa Reagan kwa siri ukaanza kuiuzia iran silaha,pesa zilizopatikana zikapelekwa kwa wapiganaji wa Contra waliokuwa wanapigana kumpindua General Manuel Antonio Ortega wa Nikaragua
 
Mwaka 1979,mapinduzi ya iran yalimtoa shah,ambae alikuwa rais kibaraka wa marekani na nchi za magharibi,

iran ikataifisha visima vya mafuta kutoka kwa makampuni ya magharibi,wazungu hawakupenda na wakawa na kinyongo,
Iran ilipoona marekani bado anaunga mkono utawala wa shah,wanamapinduzi waliuteka ubalozi wa marekani nchini iran,
Ndani walikuwemo wamarekani 52,wakawa mateka,
wakati huo rais wa marekani alikuwa jimmy carter,
baada ya juhudi za kuitaka iran iwaachie mateka wa marekani kugoma,marekani walituma timu ya makomandoo toka katika kikosi cha GREEN BERET ili kwenda kuwaokoa mateka katika operation ilijulikana kama OPERATION EAGLE CLAW,
yaani operation makucha ya Tai,
tai kama ilivyo Twiga hapa kwetu ni nembo ya marekani,

ile operation ikafail na ilipatikana hasara kubwa sina kumbukumbu marekani walipoteza makomandoo kiasi gani
Makomandoo wanane walifariki baada ya helcopter kugongana na dege lilikuwa likitumia kwenye operation hiyo kufanya refueling
 
Marekani alikua super power baada ya kutumia madhaifu ya wenzao waliongia vitani.
Sasa basi Marekani yupo makini sana kwenye maswala ya vita hawezi ingia vita itakayomletea madhara. Never
 
Marekani anaugomvi na Jordan? ana ugomvi na Oman? ana ugomvi na Iraq leo baada ya kuondoka Saddam? Ana ugomvi na Misri? au Yemeni amewahi kuwa na ugomvi nao? Saudi Arabia je? Au Kuwait

tusikuze mambo.
Hapo Uarabuni Marekani kwa sasa, narudia kwa sasa, ana ugomvi na Iran sababu viongozi wake wamekuwa vichwa ngumu, kabla ya mwaka 1989 Iran palikuwa kama sebureni kwa marekani, walikuwa na uswahiba mkubwa sababu walikuwa na rais hajielewielewi.

Haya mambo ya Nuclear ni uzushi tu, marekani ndio aliyewafundisha Iran mambo ya Nuclear mpaka alipoondoshwa shah, utasema marekani ana ugomvi na Taifa zima?

viongozi wa sasa wa Iran walikuwapo wakati wa utawala wa Obama, wakaingia makubaliano 2015 wingu la utulivu likashuka chini, kaja huyu kichaa you see what is happening, yaani hata kusema Taifa la Marekani linaugomvi na Taifa fulani ni uzushi pia.
Mkuu.
Ebu kamsome vema mmarekani nadhani humtambui vema.
Kabla ya hayo makubaliano 2015 je Obama alikua na uswahiba na Rouhani ?!!
Jibu laaah.
Obama mwaka 2011 alipeleka drone nne Iran kwa lengo lake baya lakini zikashushwa.
Akapeleka makomando wanamaji Iran wakakamatwa kabla hawajafanya uvamizi wa siri.
Je hivi ndivyo mataifa yanayokua na uswahiba yalivyo?!
Baada ya kuona ameshindwa kuiingia Iran huyo Obama wako akaona bora waingie mikataba ya amani sasa ya JCPOA.
Lakini kabla ya hapo walikua na uhasama vema tu.

US ana sera yake ya "no permanent friend no permanent enemy".
Yani hatokua rafiki wako wa kudumu na hatokua adui wako wa kudumu.
US ukifanya anavyotaka basi utakua na amani,yani atataka akuendeshe anyonye maliasili zako km wanavyofanyiwa hayo mataifa ulioyataja.
Lakini ukijielewa na kupingana nao umekwisha.
Nchi nyingi Afghanistan,Pakistan,Iraq kaziharibu yeye.
Hao Oman,Saudiarabia siku zao zinahesabika.

Halafu kama US ana ugomvi na kiongozi peke ake basi asingeiharibu Syria na Iraq kama vile.
Ukiwa na chuki kwa kiongozi wa taifa lenye kushikamana basi unalichukia ama una ugomvi na taifa zima.
 
Flashback-wakati wa mapinduzi ya 1979 huko iran,kabla yake iran ilikuwa ikiuziwa silaha na marekani,sasa baada ya tukio la mateka 52 wa marekani Jimmy carter aliiwekea vikwazo iran vya silaha,
kwahiyo wakati Iran inavamiwa na iraq,ilijikuta sasa ina silaha za marekani tupu lakini haina spare na wala ammunition stock ikawa inadeplete,

wakati huo Reagan sasa ndo Rais hiyo 1981,na Reagan ilibidi aendeelee na vikwazo vya silayakwa iran na nchi zingine duniani hazikutaka kumuuzia iran silaha kwa kumuogopa mmarekani,
sasa waajemi wakakuna kichwa wee,wakaona tusipoangalia hapahuyu saddamu atatia timu Tehran,kipindi hicho iran hana viwanda vya silaha,
so waajemi wakaamua kumcheza shere mmarekani,
Bwana mmoja anaitwa Akbar Hashem RAFSANJANI,ndo ilikuwa atumike kuwezesha irani kupata silaha,
basi wakatumia back channel na Hafsanjan akajifanya moderate na kuwa yuko agaisnt ayotolah khomein,
kipindi hicho sasa kuna mateka 7 wa kimarekani huko lebanon,

waisrael wakamwendea Reagan,wakamwambia wamechunguza na kuona kuwa huko iran kuna mtu anaeweza kuja kumrithi khomein na anaonekana ni moderate na anaweza kuja kuwa na mahusiano mazuri na wao,
wakamuapproach Rasfsanjani,nae akawa vizuri tu akawaambia wao watasaidia hezbollah kuwaachia wamarekani 7 in exchange,marekani wanatakiwa kuiuzia silaha iran,kwa kupitia israel ,
marekani kipindi hicho hakutaka iran iangukie kambi ya Soviet union na vilevile ilitaka wamarekani walioshikiliwa lebanon waachiwe na Rafsanjan akawahakikishia yeye ataongea na hizbullah na mateka wataachiwa bila tabu,

so marekani akaanza kusafirisha silaha akijifanya zinaenda israel kumbe final destination ni iran,
kila wakisafirisha silaha,hezbulah wanaachia mateka mmoja au wawili,
mpaka deal linatibuka 1986,baada ya iran kuanza kudai israel iondoke milima ya golan kule sysria ili Rafsanjan awahakikishie wamarekani kuwepo kwa uhusiano mzuri kati ya iran na marekani baada ya kufariki kwa Khomein kwani Rafsanjan ndo alionekana kuja kuwa mrithi wake,
baadhi ya maafisa katika serikali ya marekani ndo waliisanua hii scandal,
lakini tayari mda huo iran ilikuwa imeshaanza kujiundia silaha yenyewe na vita vya iran na iraq vilikuwa vikienda ukingon
 
Kwani uvamizi wa Iraq ulikuwa na intention ya Regime change pale Iran?

Kuna wamarekani walikuwa wanashikiriwa mateka , na Iran ndio ilikuwa ina final say waachiwe au wasiachiwe. actually USA hakuwa hata anamsaidia Iran Vitani alikuwa ana interests zake tu sema wairan pia walikuwa na shida ya siraha, ndo maana biashara yenyewe ilikuwa ikifanyika kwa siri kubwa sana.
Umebadilisha sasa kaka!?
Ulikua ukisema Iran alipata collabo US ndipo nilipokua nakinzana nawe.
 
Back
Top Bottom